Msaada: Nimemlipia mtu mwingine road license

patrickkkkky

JF-Expert Member
Feb 17, 2014
468
286
Wiki iliyopita nilikua natoka Dar na gari yangu kuelekea Arusha nikapita pale Mbezi mwisho kulipia road license maana ilikua imeisha. Nakumbuka kumpa dada aliyekua stationary kadi ya gari na fedha ili anlilipie kupitia MAX MALIPO

Baada ya kumpa huyo dada alivipeleka kwa mmama ambaye alikua naye, huyo mama aliishia kumfokea kwamba inakuaje huyo dada hajajifunza kazi yoyote tokea amuajiri. Basi yule dada akachukua mashine ya max malipo akalipia kisha akanipa risiti na kadi ya gari.

Jana naenda TRA kuchukua sticker kushtuka naambiwa sticker mbona nishapewa. Kuangalia vizuri risiti yule dada alijaza dbl baada ya dee kwenye plate no. Tra hapa Arusha wananiambia hawana msaada wowote licha ya kuwasumbua sana.

Any lead wadau nifanyeje???
 
Wakusaidie kumpata mwenye hiyo gari coz data watakua nazo ili uwasiliane nae umpatie stiker akupe mpunga wako naamin hatokataa
 
Wakusaidie kumpata mwenye hiyo gari coz data watakua nazo ili uwasiliane nae umpatie stiker akupe
mpunga wako naamin hatokataa
Sticker ashachukua mkuu ila nahisi kama hiyo gari imefanyiwa double payment ila tra hawataki ku counter check
 
Hapo ndo nliposhangaa kabisa. Afu sikuhakiki maana sikua na hofu anaweza kukosea plate no. Na njiani nlikua nawapa traffic officers ile risiti

andika barua kwa TRA kuwaambia umekosea gari no fulani na ulitaka kulipia no fulan mbona inatokeaga sana hiyo na wanabadilisha!
 
Wiki iliyopita nilikua natoka dar na gari yangu kuelekea arusha nikapita pale mbez mwisho kulipia road license maana ilikua imeisha. Nakumbuka kumpa dada aliyekua stationary kadi ya gari na fedha ili anIilipie kupitia MAX MALIPO

Baada ya kumpa huyo dada alivipeleka kwa mmama ambaye alikua naye, huyo mama aliishia kumfokea kwamba inakuaje huyo dada hajajifunza kazi yoyote tokea amuajiri. Basi yule dada akachukua mashine ya max malipo akalipia kisha akanipa risiti na kadi ya gari.

Jana naenda tra kuchukua sticker kushtuka naambiwa sticker mbona nshapewa. Kuangalia vizuri risiti yule dada alijaza dbl baada ya dee kwenye plate no. Tra hapa arusha wananiambia hawana msaada wowote licha ya kuwasumbua sana

Any lead wadau nfanyeje???
Nenda hapo walipokulipia wao wataongea na maxmalipo, maxmalipo wataandika barua tra itarudi kwao mapema tu, ila waliokupa hiyo waķulipie wao ndo watarudishiwa
 
Sticker ashachukua mkuu ila nahisi kama hiyo gari imefanyiwa double payment ila tra hawataki ku counter check
HAwa TRA hovyo kabisa. Kama Wamegundua kuna doble payment ni kweli hawawezi kufanya chochote hata siamini!
 
Hapo ndo nliposhangaa kabisa. Afu sikuhakiki maana sikua na hofu anaweza kukosea plate no. Na njiani nlikua nawapa traffic officers ile risiti
Alopofokewa na bosi wake ilikuwa ni sababu tosha ya kuhakiki utendaji wake
 
Back
Top Bottom