Msaada: Nimelizua kwa mama watoto ,kapewa taarifa nimelala na mwanamke ghetto ,nipeni mbinu za kijajusi nimfahamu mgombanishi/mpeleka taarifa

Azoge Ze Blind Baga

JF-Expert Member
Mar 8, 2019
366
1,379
Wakuu salama!?

Mi naishi mbali na wife ambaye nimezaa nae watoto wawili ,mmoja wa miaka 7 na mwingine ana miezi 5

Na nipo na huyu mwanamke since 2011

Yeye anafanyia kazi mkoa mwingine nami mkoa mwingine ingawa sio ya mbali,yeye kaajiriwa ajira ya kudumu ila mm napiga tu mishe private sector

Sasa January nlikutana na binti Fulani tukaanza mahusiano ,siku ya kwanza nikamleta home nikamla,kanitembelea kama Mara 3

Hapo home kuna wamama wawili wasio na kazi wao wanashinda tu home kusubiri waletewe

Sasa Leo yule mchepuko wangu kaniibukia ghafla bila taarifa mida ya asubuhi na kama mnavyojua weekend home palikua na wapangaji wengine ,sasa kuna binti ndugu wa mpangaji mwenzangu alimwona yule mchepuko anaingia na mida ya kutoka alimwona pia

Mi sikua na wasiwasi na mtu kwa kuwa hii sio Mara ya kwanza kwa huyu demu kuniibukia home

Sasa mida hii nimekaa nashangaa Simu ya wife inaingia napokea nakutana na matusi ya kutisha ananituhumu kwamba nimelala na demu na hadi sasa nipo nae ndani jambo ambalo sio la kweli sijalala na demu ila demu alikuja akasepa

Mpaka sasa ananitukana bado sijamjibu ila nimemkatalia na kumwambia aache kusikiliza maneno ya watu

Sasa wakuu nishaona kuna mtu anataka kuniharibia kwa kupeleka umbeya kwa wife ,so nipeni mbinu za kijasusi niweze kumbaini huyo mchonganishi nilale nae mbele.

Azoge

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Kwahy ni ile "sogea tuishi" ndo unayofanya? Kisheria uyo ni sio mwanamke wako ni wife pia.
 
Back
Top Bottom