Msaada: Nimelipa PAYE kubwa zaidi ya kiwango kinachotakiwa kwa miaka miwili

J33

JF-Expert Member
Jun 11, 2014
1,552
1,512
Kutokana na ufahamu mdogo wa boss wangu na wangu pia katika masuala ya kodi nimejikuta nalipa kiasi kikubwa zaidi cha kodi katika mazingira yafuatayo;

1.Boss wangu amekuwa akitumia kitabu cha kodi cha mwaka 2011~2012 wakati kodi imekuwa ikipungua kila mwaka hivyo kujikuta nalipa zaidi.

2. Boss wangu amekuwa akipiga hesabu vibaya, yani anapigia mahesabu basic salary wakati kulingana na muongozo wa TRA kiasi kinachohesabiwa ni baada ya kukata PPF michango ya pensheni.

Nataka kujua kama naweza kudai pesa hizo TRA au kukaa kwa muda bila kulipa kodi ili kufidia deni hilo ninalowadai?

Duc In Altum.
 
Mmh!!! TRA wanarudisha pesa ikishaingia? Nadhani hiyo imetoka mkuu. Sidhani kama utapata hiyo fedha.
 
Itakuwa hasara kubwa, na mm sio lazima warejeshe ila wakubali wasinikate kodi hadi hiyo niliyozidisha iishe maana ni pesa nyingi sana.

Duc In Altum.
 
Kutokana na ufahamu mdogo wa boss wangu na wangu pia katika masuala ya kodi nimejikuta nalipa kiasi kikubwa zaidi cha kodi katika mazingira yafuatayo;

1.Boss wangu amekuwa akitumia kitabu cha kodi cha mwaka 2011~2012 wakati kodi imekuwa ikipungua kila mwaka hivyo kujikuta nalipa zaidi.

2. Boss wangu amekuwa akipiga hesabu vibaya, yani anapigia mahesabu basic salary wakati kulingana na muongozo wa TRA kiasi kinachohesabiwa ni baada ya kukata PPF michango ya pensheni.

Nataka kujua kama naweza kudai pesa hizo TRA au kukaa kwa muda bila kulipa kodi ili kufidia deni hilo ninalowadai?

Duc In Altum.
Peleka hesabu zako na bank statement, ikiwezekana na mkataba wako wa ajira, kikubwa uweze kuthibitisha madai yako bila shaka yoyote utapigiwa hesabu ya kiasi ulichozidisha na either utarudishiwa or hutakatwa kodi hadi deni lako liishe. Wafanyabiashara wengi wanaogopa kwenda kudai pesa zinazozidi kwa sababu ni wakwepa kodi wakubwa. Kila la kheri mkuu usisahau kuleta mrejesho ili wengine wajifunze.
 
Nitafanya ivyo na boss kaniambia atanipa document zote alizokuwa analipia tangu mwanzo, ndan ya week hii nitaenda na nitaleta mrejesho hapa.

Vema mkuu, serikali yetu sio matapeli, kwa kuongezea tu unawezabeba noti yoyote ile ukawaonesha kale kaneno "kwa malipo HALALI ya shilingi"
 
TRA wanarudisha pesa usiwe na shaka. Tena kampuni yako ingedai na kisha kupunguza kodi wanaopeleka tra ingekuwa rahisi zaidi
 
Itakuwa hasara kubwa, na mm sio lazima warejeshe ila wakubali wasinikate kodi hadi hiyo niliyozidisha iishe maana ni pesa nyingi sana.

Duc In Altum.
Nenda kawaone mkuu usikate tamaa kabla hujawaeleza. Nenda na evidence nadhani wanaweza kukurudishia.
 
Peleka mkataba wa ajira,payslip zote,kama anapayroll summary etc.Hawatakurefund as a cash ila watajumlisha ile tofauti na hautakatwa kodi kwenye mshahara wako mpaka mpaka deni liishe.TRA watampa mwajiri wako barua ya kumuinstruct asikukate kodi mpaka kiasi unachowadai kitimie
 
Huo ndio ukweli wa mambo!!!

Duc In Altum.
Kama ndio hivyo,kabla ya kupeleka hizo document TRA tafuta mshauli wa maswala ya kodi akupe ushauri kwa mujibu wa sheria za kodi,kupeleka documents TRA pekee kunaweza kuibua mambo mengine zaidi kati ya mwajiri wako na TRA kwa sabab mmekua hamfanyi external audit ambayo kisheria mnatakiwa kufanya kila mwaka wa fedha wenu unapoisha.
 
Ila jaribu kwenda tu TRA usikie watakujibu nini. Usifikie tu mahitimisho ya moja kwa moja bila kuhakikisha kwanza
 
Kama ndio hivyo,kabla ya kupeleka hizo document TRA tafuta mshauli wa maswala ya kodi akupe ushauri kwa mujibu wa sheria za kodi,kupeleka documents TRA pekee kunaweza kuibua mambo mengine zaidi kati ya mwajiri wako na TRA kwa sabab mmekua hamfanyi external audit ambayo kisheria mnatakiwa kufanya kila mwaka wa fedha wenu unapoisha.
Hiyo si kazi ya external auditing. Auditing ni opinion based and mostly is based on sampling.
 
Kazi ya external Auditor ni pamoja na kutoa ushauri wa masuala ya kodi na kushauri kadiri sheria ya kodi inavyosema!! Opinion ni hitimisho ya alichokiona,katika process nzima ya auditing,!!
 
Inaonekana kuna tatizo kubwa katika idara ya uhasibu kazini kwa mleta mada kiasi cha kushindwa kujua miongozo ya kodi specifically PAYE kwa kadri inavyokuwa inatolewa.

Na kwa jinsi inavyoonekana si yeye pekee yake ambaye makato yake ya PAYE yamekosewa hivyo kuna uwezekano kuwa kuna staff wengine ambao nao watakuwa wamelipa PAYE kubwa zaidi ya inavyotakiwa. Kwa haraka haraka najiuliza yafuatayo:

(i) kama PAYE iliweza kukosewa na kuwa kubwa hakuna uwezekano makosa ya aina hiyo yakafanyika kwa staff wengine baadhi wakawa wanalipa PAYE pungufu na hivyo kuikosesha serikali mapato?

(ii) Je huko TRA hakuna uhakiki makini unaofanyika ili kuhakikisha kuwa PAYE zinazolipwa na watumishi ndiyo zile zinazotakiwa kulipwa bila makosa ya kuzidisha au kupunguza?
 
Auditing haukagui kila kitu. Labda special auditing. Auditing kazi yake si detection of errors na frauds. Kwahiyo kusingizia external auditing ni makosa hapo.
 
Baada ya jana kupata ukweli nimewashirikisha wenzangu ni wote tumeadhirika maana boss alikuwa anatumia muongozo wa zamani na alikuwa anakata bila kuweka pembeni pesa ya PPF.

Duc In Altum.
 
Auditing haukagui kila kitu. Labda special auditing. Auditing kazi yake si detection of errors na frauds. Kwahiyo kusingizia external auditing ni makosa hapo.
Kasome vizuri majukumu ya external auditor kwa mteja wake,kisha ulinganishe na wajibu wake kwa TRA ndio utaelewa ninachosema,
 
Back
Top Bottom