Msaada nimekua na hasira sana ni stress tu au kuna kingine?

Oct 22, 2018
35
95
Habari wana mmu natumai mko salama na mnaendelea vyema kulijenga taifa la viwanda mimi ni kijana wa miaka 28+ ambae bado naishi kwa wazazi wangu, najua kuna watu wataponda ila sioni sababu ya kutoka maana inanisaidia sana kupunguza matumizi na kuongeza savings ukifika muda sahihi nitatoka na sihitaji ushauri hapa bali kwa jambo jingine la hasira zangu.

tatizo hili nimeligundua kama miezi miwili iliyopita kuna siku mzee alikua ananioelekeza kitu kwa ukali kidogo nilimjibu kiufupi tu we mzee naomba uniache, nilijishangaa snna sijawahi kumjibu mtu mzima hivi na hasa mzee ambae naamini alistahili kutajwa kwenye uzi wa wazee wakaksi siku nyingine boss wangu aliniuliza hiyo kazi umefanyaje mbona haieleweki nikamuuliza kwa dharau boss usinifundishe kazi najua ninachokifanya hapo nilikua nagonga meza kwa nguvu sana leo nimetoka kumjibu kaka yake baba wewe mzee acha use*** wako.

Hiyo ni mifano michache tu na kwa kweli huwa najutia sana kufanya vitendo hivyo sasa nimejaribu kukisia vitu vinavyoweza kuwa vimenipelekea kuwa hivyo cha kwanza ni kuwa situmii kilevi cha aina yoyote, cha pili nimekua sina mahusiano kwa muda wa mwaka mmoja na miezi miwili sasa mpenzi wangu wa mwisho tuliachana kutokana na mimi kuchelewa sana kupata ajira japo huwa nashiriki zinaa kwa wadada zetu wa berbershop wabarikiwe kwa kweli, cha tatu kazi nayofanya nakua busy sana sina muda wa kupumzika maana naingia saa moja na nusu kutoka saa 12 jioni kila siku kasoro jumapili tu kwa maana ni kampuni binfsi.

Je ndugu wana mmu inawezekana kuwa moja ya matatizo nayoyahisi ndiyo yanasababisha hasira au ni kitu kingine tu na je nifanyeje niondokane na hali hii ambayo siipendi nakaribisha ushauri kebei nasaha na mapendekezo kwa wataalamu wa fasihi naomba mnisamehe siyo muandishi mzuri asante.
 
rikiboy

JF-Expert Member
Feb 19, 2017
13,800
2,000
Nimenunua kiwanja na nmewekeza kwenye biashara nyingine nyingine ipo bank, mpango wa kuhama nyumbani ni mwakani sio sasa hivi
Hilo ndo linakupa stress maana Ukikaa kwenu kubali kuwa treated Kama mtoto sasa wewe unataka Uhuru kama upo kwako na hicho ndo kinakupa stress Sana yani kila unaeongea nae unahisi anakudharau kumbe kawaida tu...!! Kuhama kwenu sio mpaka ujenge nyumba yakoo...Hama nenda kapangee mkuu
 
manizzle

JF-Expert Member
Apr 29, 2015
3,436
2,000
Kama unasavings kidogo chukua likizo hata ya wiki moja tafuta demu nenda nae popote pale iwe ndani au nje ya nchi kama kipato chako kinaruhusu. Ukiwa huko usifanye kitu chochote kile zaidi ya kula bata tu. Itasaidia kupunguza msongo wa mawazo
 
Oct 22, 2018
35
95
Nilitaka kuhama as soon as I had my first job mzee mwenyewe ndo alinambia hiyo hela ya pango heri uwe unamtumia mdogo wako pocket money shule nikaona ok nikaja kupata kazi yenye maslahi kidogo ila nipo busy sana kupata muda wa kuhama home ila ninejipanga mwakani mwezi wa tano natoka hapa nyumbani
Hilo ndo linakupa stress maana Ukikaa kwenu kubali kuwa treated Kama mtoto sasa wewe unataka Uhuru kama upo kwako na hicho ndo kinakupa stress Sana yani kila unaeongea nae unahisi anakudharau kumbe kawaida tu...!! Kuhama kwenu sio mpaka ujenge nyumba yakoo...Hama nenda kapangee mkuu
 
Oct 22, 2018
35
95
Kama unasavings kidogo chukua likizo hata ya wiki moja tafuta demu nenda nae popote pale iwe ndani au nje ya nchi kama kipato chako kinaruhusu. Ukiwa huko usifanye kitu chochote kile zaidi ya kula bata tu. Itasaidia kupunguza msongo wa mawazo
Asante mkuu japo company nayofanyia kazi ni private hawawezi kunipa likizo muda wote huo
 
ATRACURIUM

JF-Expert Member
Jul 2, 2018
722
1,000
Asante mkuu japo company nayofanyia kazi ni private hawawezi kunipa likizo muda wote huo

Hii itakuwa ni stress za kazini, unafanya kazi muda mrefu sana na hupati muda wa kupumzika vizuri, jaribu kuwa unajichanganya na watu tofauti tofauti au kwenda sehemu tofauti na nyumbani unapokuwa na mapumziko, halafu kapime Goitre huenda una "Hyperthyroidism" wakati hujijui kuwa wewe ni mgonjwa.
 
Kweli mkuu inawezekana maana hata marafiki zangu wengi sipo karibu nao na mawasiliano yamepungua kutokana na majukumu hivyo muda mwingi nakua kazini au nyumbani sababu situmii pombe. Kujichanganya kwangu na watu nibkibanda umiza tu kushangilia mane salah na firmino wanavyogawa dozi
 
amu

JF-Expert Member
Aug 8, 2012
15,281
2,000
Aisee wewe mbona nimshamba sana mshamba sana aliekuambia starehe pombe ukiwa hunywi unakaa ndani na marafiki huna nani? embu acha utindiga mimi naweza kula gambe non stop na wanywa pombe na nisinywe na nikaenjoy hasa na naweza nikaenda sehemu peke yangu nikaenjoy hasa as long as mfuko uko safi.
Wewe nimegundua ni mtindiga na mastress yatakuumiza

mwamgongo

JF-Expert Member
Jul 11, 2015
483
500
1.Huna pesa ya kukidhi mipango yako, unamipango mingi isiyoendana na kipato......weka mipango inayoendana na kipato taratibu utafika.
2.Tafuta mtu unaye mpenda sana muoe akupe penzi nzito kwani unahitajia penzi nzito.
3.Si kila jambo unalofanya au kumfanyia mtu lazima upate mrejesho chanya.
4.Punguza ujuaji kwani unaujuaji mwingi hivyo unajiona upo sahihi kwa kila jambo.
5.Kwasasa unaona wazazi ni kama watu wa kawaida, watakapo toweka utaona umuhimu wao.

Wasalam.
 
amu

JF-Expert Member
Aug 8, 2012
15,281
2,000
Unaenda kwenda hata coco beach ukale mihogo ya buku jero upepo ni mzuri kwa kutoa stress, unaweza nenda saadani kikubwa enjoy life unaishi kama mfungwa, demu mzuri huna, unanunua makahaba umri mkubwa bado uko kwa wazazi, huna hata mtoto wa kumuita ita, ukute pesa pia huna.
Embu acha kujifungia toka nje kaenjoy life.
 
Oct 22, 2018
35
95
Aisee wewe mbona nimshamba sana mshamba sana aliekuambia starehe pombe ukiwa hunywi unakaa ndani na marafiki huna nani? embu acha utindiga mimi naweza kula gambe non stop na wanywa pombe na nisinywe na nikaenjoy hasa na naweza nikaenda sehemu peke yangu nikaenjoy hasa as long as mfuko uko safi.
Wewe nimegundua ni mtindiga na mastress yatakuumiza
Asante mkuu ndio maana naonba ushauri kwenu maana najua jamiiforums kuna watu mbalimbali wanaoweza kunisaidia
 
simon baker

JF-Expert Member
Oct 5, 2017
444
1,000
Nimenunua kiwanja na nmewekeza kwenye biashara nyingine nyingine ipo bank, mpango wa kuhama nyumbani ni mwakani sio sasa hivi
Assume ni phase unapitia
Leta mrejesho ukisha hama nyumbani
Maana wewe huwezi ona wala kutuelewa tukikushauri uhame nyumbani ndo solution
You need space uweze ukatuliza kicwa chako
Advantage za kuhama home ni
-kwanza utajengeka moyo wa kuwamiss wazazi mana huwaoni mara kwa mara(hata wao watakumiss)
-utapata mda wakutafuta mwenzi wako maana maisha ya kibachela yana influence sana utafute partner..mana ukirud jion umechoka uanze kutafuta chakula mara kupika utaanza kusema bora niweke kadem ndan kawe kanapika nk
-wewe una stress kwasababu umri wako huo am sure kaz yako kubwa ni kuchanga tu maharusi ya wenzio afu ukijiona msindikizaji huna dira lazma stres upate
-jiwekee limit stress ziishie inner thoughts..kazi ngumu saiz ukipigwa chini kwakujidai unajua sana utajinyonga wew au kula sumu
 
Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Top Bottom