Msaada: Nimehitimu form four na nimepata alama hizi je, kuna uwezekano wa kuchaguliwa form five ya kiaerikali,private ama chuo?

Hakuna advance unayofiti. Iwe government au private.
Nakushauri nenda vyuo vya utumishi kachukue certificate ya record management.
 
Kuna MTU kaniambia uwezekano Wa kwenda advance ya serikali upo kwa mchepuo Wa HKL ,ikichagizwa na sifa ya ufaulu Wa CCD , je ,yawezwkana mtu mwenye ufaulu Wa division four kuchaguliwa advance ya kiserikali?? Mchango wakuu!!
Ni kweli ana CCD lakini kwenda Advance unatakiwa uwe na Credit tatu katika masomo yako, uwe na point zisizo zidi 25 na wewe una 26. Hii ndio inayokuzuia kuchaguliwa. Na vigezo hivyo ni kwa shule zote za binafsi na serikali. Kama ni lazima uende F5 basi rudia mtihani vinginevyo fikiria diploma nyingi zinahitaji D nne nawe unazo na zaidi.


Chuo sahau walishasema nilazima upite ADVANCE LEVEL kabla ya chuo Sent using Jamii Forums mobile app
Mkuu hii sikweli issue sio kusema kwani wanasema mengi ukweli hakuna muongozo wowote unao onyesha hilo na TCU Admission guidelines ziko wazi.
 
Unaenda.

Kuna mdada fulani, alienda na akapata Div 11 Points 10 HKL kutoka Div 4 Points 26.

Jambo la msingi uwe na CREDITS tatu ( Yaani C au zaidi ) na usiwe na F pia kwenye Combination unayotaka kusoma.
Anaweza Kupokelewa Ndio, Ila Hawezi Fanya Pepa La Six, Arisiti Somo Moja
 
Awali ya yote Nikiwa kama member Wa jf nawasalimu nyote, na nawasilisha mjadala kama ifuatavyo;
Mimi ni muhitimu Wa form four na nimepata wastani Wa Division four ya 27 (4:27) ikiwa na alama zifuatazo za masomo;
Civics D,
History C,
Kiswahili D,
English C,
Geography D,
Biology D, na
Math's F
Kuna MTU kaniambia uwezekano Wa kwenda advance ya serikali upo kwa mchepuo Wa HKL ,ikichagizwa na sifa ya ufaulu Wa CCD , je ,yawezwkana mtu mwenye ufaulu Wa division four kuchaguliwa advance ya kiserikali?? Mchango wakuu!!
Mkuu hiyo division four huwezi kuchaguliwa kwa gvt schools coz hata hao wenye 3 tha mwishoni sio ote watachaguliwa ila private unaweza pata hapo mkuu

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Nadhani hii ndiyo current authority
1548576967709.png
 
Ushauri wangu tuliza kichwa. Achana na chuo au form six. Nenda VETA chagua kozi nzuri. Hutajutia ila uwe determined na maisha yako. wengi wanakimbia huko ila ndo kuzuri
 
Back
Top Bottom