Msaada: Nimeandika barua ya kuacha kazi naambiwa natakiwa nimlipe mwajiri

Akili Sina

JF-Expert Member
Jan 18, 2018
301
2,218
Habarini wakuu,

Nimeandika barua ya kuacha kazi, naambiwa sheria inasema natakiwa nimlipe mwajiri mshahara wa mwezi mmoja kwavile sikumpa notice.

Nikajitetea kuwa mkataba wangu ulishaisha toka 2018 na sijasaini mwingine, naambiwa sheria inasema kama mkataba wa kwanza umeisha na hamjaingia mkataba mwingine basi ule ulioisha unajirenew automatically.

Pia mbali na likizo zako, je ni benefits gani nyingine naweza kupata? Nimefanya kazi miaka 3.

Msaada kwa wanaojua hizi sheria please

Sent using Jamii Forums mobile app
 
We itakuwa umesubmit hiyo barua kwa mwajiri wako ikionesha unataka kuacha kazi under 24hrs notice Yaani ndani ya masaa 24. Hapa inapaswa wewe ndio umlipe mwajiri wako basic salary ya mwezi mmoja kwasababu umemshtukiza na hakujianda kwa replacement ya gafla uliyoisababisha.
Kama barua yako ikionesha kuwa unaacha kazi baada ya siku 28 maanaake kwamba umempa muda wa kutosha mwajiri wako ili atafute replacement wako, kwa njia hii hutamlipa chochote zaidi ya yeye mwisho wa mwezi kukulipa stahiki zako zote
 
Vipi kama huku specify kama ni 24hrs or 28 days

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Mwenzio mimi mkataba uliisha kama leo, kesho nika kiamsha zangu kitaa kucheki madili mengine, maana nilisha pachoka hata hivyo. Wakapiga simu mchana mbona hujaja kazini leo, nikasema mkataba ulisha ishaga kuanzia leo nimejiajiri. HR na wakurugenzi wake hadi leo hawataki kujua hata kama nilifanya clearance ya vtu walivyokua wamenipa
 
Habarini wakuu,

Nimeandika barua ya kuacha kazi, naambiwa sheria inasema natakiwa nimlipe mwajiri mshahara wa mwezi mmoja kwavile sikumpa notice.

Nikajitetea kuwa mkataba wangu ulishaisha toka 2018 na sijasaini mwingine, naambiwa sheria inasema kama mkataba wa kwanza umeisha na hamjaingia mkataba mwingine basi ule ulioisha unajirenew automatically.

Pia mbali na likizo zako, je ni benefits gani nyingine naweza kupata? Nimefanya kazi miaka 3.

Msaada kwa wanaojua hizi sheria please

Sent using Jamii Forums mobile app

Hili jambo linategemea zaidi namna ambavyo umeandika barua yako. Katika barua ya mwajiriwa kuacha kazi ni muhimu sana kuainisha wazi kabisa ni siku gani ndio itakuwa mwisho wako wa kufanya kazi. Sheria ya kazi imeweka wazi kwamba unatakiwa kutoa notisi ya mwezi mmoja unapoandika barua ya kuacha kazi, kama hutotoa notisi ya kipindi hicho basi itakulazimukumlipa mwajiri kiasi cha pesa ambacho ni sawa na mshahara wako wa mwezi mmoja kama ungefanya kazi.

Kitu kingine kuhusiana na mkataba ni kwamba, ikiwa mkataba wako wa kazi utakuwa umefikia ukomo na mwajiri pamoja na wewe mwenyewe mlikaa kimya bila kugusia suala la kuhuisha (renew) huo mkataba, basi yale yote yaliyokubaliwa katika mkataba uliopita yataendelea kutumika mpaka pale ambapo mtaamua kuingia mkataba mwengine mpya. Naamini katika suala lako ni kwamba kutoka mwaka 2018 mwajiri aliendelea kukulipa stahiki zako zote,hivyo basi na vigezo na masharti vilivyokuwa vinaongoza ajira yako vitaendelea kutumika.

Mbali na malipo yako ya likizo ambazo zilikuwa bado kuchukuliwa, kitu kingine unachostahili kupata ni pamoja na kiinua mgongo ambacho ni sawa na mshahara wa siku saba kwa kila mwaka mmoja wa ajjira, hii ina ukomo wa miaka kumi. Pia mwajiri atatakiwa kukupatia Cheti cha Huduma (Certificate of Service). La muhimu zaidi ni kuhakikisha mwajiri wako ameingiza michango yako yote katika mifuko ya jamii (social security), hii unaweza fanya kwa kuchukua fomu maalumu toka mfuko wako wa jamii ambayo mwajiri atatakiwa ajaze michango yote aliyokuwekea katika kipindi chote ulichofanya kazi na namba ya risiti zilizotolewa baada ya kuwasilisha michangoo hiyo.
 
Pole sana hapo cha kukusaidia Andika barua ya kuacha kazi mwezi ujao ila huu mwezi endelea kufanya kazi
 
Back
Top Bottom