Msaada: Nilijigonga kwenye ugoko, nikijaribu kukimbia naanzisha ugonjwa upya

Melancholic

JF-Expert Member
Oct 12, 2018
1,830
3,059
Habarini za wakati huu wakuu. Kwanza tumshukuru Mungu kwa kutuamsha salama.
Pili niende moja kwa moja kwenye mada, binafsi huwa nina kawaida ya kufanya mazoezi kila asubuhi ikiwemo joging na mazoezi mengine ya viungo.

Pia huwa ninapenda sana kukimbia mara nyingi huwa natoka Kijitonyama mpaka Mwenge sometime naenda mpaka Lugalo.

Sasa mwezi wa nane nikiwa home nilijigonga maeneo ya ugoko kukatokea nundu nikachukulia poa sikupachua wala nini nikawa naendelea kufanya zoezi kama kawaida ila nilikuwa nikitoka zoezi nasikia maumivu kama ya misuli kuvuta upande ule ule wa mguu niliojigonga halafu kunakuwa na nundu pia maumivu kiasi, nimeendelea hivyo mwisho nikashindwa hata kukimbia nikikimbia basi wiki nzima nakuwa natembea kwa shida.

Nimejaribu kutumia madawa ya kuchua ni kweli yamenisaidia mpaka nikakaa sawa hata kutembea nikawa natembea vizuri nilivyoona hivyo nikajua tayari nimepona basi nimekaa kama wiki nikajiona sasa nipo tayari kuanza zoezi kuna siku majira ya jioni nikaamua kukimbia kutoka Kijitonyama to Mwenge mpaka Mlimani city ila wakati narudi nilianza kuhisi maumivu ya misuli inakuwa kama inavuta hivi, Basi nimefika maeneo sayansi maumivu yakazidi kuwa makali nikakimbia kwa shida mpaka nikarudi home nikalala maana ilikuwa usiku.

Kesho yake nimeamka sikuweza kutembea wiki nzima nikawa nachechemea nikanunua dawa ya kuchua inaitwa Volin nimeitumia wiki mbili nikakaa sawa. Nikawa natembea vizuri kabisa tena mwendo mrefu na maumivu yakawa yameisha basi nilivyoona hivo jana majira ya jion nimejaribu kukimbia kutoka kijitonyama to makumbusho nimerudi fresh ila leo nimeamka na maumivu makali ya misuli siwez tena kutembea ndugu zangu.

Kama kuna wataalamu humu wa masuala ya afya mnaweza kunisaidia je hili ni tatizo gani na nitumie nini kupata ufumbuzi maana nikitumia madawa ya kuchua nakuwa sawa na kutembea natembea mwendo mrefu tu na sihisi maumivu ila nikijaribu kukimbia basi nakuwa naanzisha ugonjwa upya. Yani siponi moja kwa moja maana nikijaribu kukimbia tu tatzo linajirudia

Mniwie radhi nimewachosha na uzi mrefu ila nimejaribu kuwaelezea kwa kina ili muelewe na niweze kupata msaada maana sasa ni karibia miez mitatu nasumbuliwa na hili tatzo ahsanteni na karibuni.
 
Nenda hospitali mkuu wakakucheck naona kama operation inakuhusu mkuu.
 
Nadhani hospital ni mahala penye ushauri sahihi zaidi ya hapa...Nenda hospital kubwa sio vituo vya afya hiyo issue Ni serious
 
Sasa kjn tayar una kovu , achan na zoez la kukimbia Tembea tuu ,

Maan ata ukiend hospital wakakutib kama kwa operation ndio hutotakiw kukimbia Tena
 
Sasa kjn tayar una kovu , achan na zoez la kukimbia Tembea tuu ,

Maan ata ukiend hospital wakakutib kama kwa operation ndio hutotakiw kukimbia Tena
Sina kovu lolote mkuu yani ni misuli ndio inauma sasa sijui hiyo operation itakuwa inahusus nini
 
Nenda hospital ufanyiwe uchunguz wa kina

Then upme njia zao za kukutibu ila kama operation jarbu kuulza utapon kbsa na utakuw na uwezo wa kutembea kwa muda mrefu na kukimbia
Ahsante mkuu nitazingatia ushauri wako
 
Nenda hospital ufanyiwe uchunguz wa kina

Then upme njia zao za kukutibu ila kama operation jarbu kuulza utapon kbsa na utakuw na uwezo wa kutembea kwa muda mrefu na kukimbia
Ahsante mkuu
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom