Msaada: Nilibakwa na majambazi nimepata ujauzito

hesalieyo

JF-Expert Member
Jul 18, 2012
378
378
Jamani naomba mnisaidie,

Nitumie dawa gani ili niweze kutoa ujauzito wa mwezi mmoja na wiki? Nimefikia uamuzi huo baada ya kugundua nina ujauzito na siko tayari kuzaa na mtu nisiyemjua.

Iko hivi:

Ni mwezi sasa umepita tulivamiwa sehemu niliyopanga, sijui kama na wenzangu iliwatokea ila wezi hao waliingia vyumba vinne tofauti na changu kikiwemo, waliingia kwangu walihitaji hela nasikitika na mmoja wao aliniingilia kimwili, sikua na jinsi kwasababu walikuwa na silaha.

Hivyo naombeni mnisaidie, siwezi kuzaa na mtu nisiyemjua jamani.
 
Kweli haya uyasemayo?Ama umefanya kwa hiari ndo unahangaika kuua.

Naomba uamini nisemayo, sijawahi kufikiri kutoa mimba ata siku moja, nahata ningekuwa namjua baba mtoto hakika nisingefikia uamuzi huu
 
Kama kweli haya ni ya kweli inauma sana na emtionaly ina sababisha maumivu makali( torture of emotion).
Pili ni kwamba haya ni moja ya matatizo ambayo yamekuwa yakileta mchanganyo wa makubaliano( contradiction) ktk swala la kutoa mimba.

Wengine wanakubali kutoa na wengine kwa misingi ya dini wanabaki kichwa kinauma. Kiukweli hakuna jibu la moja kwa moja na hapa niseme tu uamuzi ni wako.

Hata hivyo(kama fundisho kwa wengine) ulipaswa kwenda kwa daktari mara tu baada ya tukio ili akufanyie tiba sahihi maana huu n ubakaji na unaweza kuwa ktk hatari ya maradhi ya ukimwi na magonjwa ya zinaa na pamoja na uja uzito. Kama ukiwahi kwa dr( sio mwaka) unaweza kupata kinga ya maradhi na mimba pia.

Kuhusu kutoa mimba nakushauri ufanye kama nafsi yako inavyokutuma. Utaitolea wapi mimi sijui ungekuwa karibu nami ningekuonesha cha kufanya.
 
Usitoe mimba tafadhali kuwa na baba au laa sio sababu ya ww kutoa mimba hebu muombe mng
 
Mie sio noma. Huwa najaribu tu kuwa very well informed. Kitendo cha kubakwa na kaka jambazi kingenipata, na kama angefanikiwa kabla sijamuua ama kuniua yeye; ningeenda kwa best counselor in the country. Na by the time hiyo mimba inajulikana basi tungeifanyia maamuzi pamoja.

Kumlea mtoto ambae ni product ya kubakwa? Sijawahi kuwaza aisee.
Marie Stopes....mhhhh....wewe noma
 
walikuwa vibaka au majambazi??
kutoa mimba ni dhambi, zaa tu huwez jua akaja kuwa obama wa Tz.
"lear nakuombaaaa, usitoe mimba yangu".......
mungu akileta mtoto, huja na sahani yake...
kwa utafiti wangu mdogo maprofesa wengi,
marais wengi,
watalaam wengi.
hawakuzaliwa ndani ya ndoa wengi wao ni nje ya ndoa namaanisha baba tofauti na alieoa mhusika.
dont kill, huyo atakuwa super ginious na atakutunza na kukupenda km mama yake kuliko hao utakaobeba mimba zao kwa hiari yako.
 
Kama kweli haya ni ya kweli inauma sana na emtionaly ina sababisha maumivu makali( torture of emotion).
Pili ni kwamba haya ni moja ya matatizo ambayo yamekuwa yakileta mchanganyo wa makubaliano( contradiction) ktk swala la kutoa mimba.

Wengine wanakubali kutoa na wengine kwa misingi ya dini wanabaki kichwa kinauma. Kiukweli hakuna jibu la moja kwa moja na hapa niseme tu uamuzi ni wako.

Hata hivyo(kama fundisho kwa wengine) ulipaswa kwenda kwa daktari mara tu baada ya tukio ili akufanyie tiba sahihi maana huu n ubakaji na unaweza kuwa ktk hatari ya maradhi ya ukimwi na magonjwa ya zinaa na pamoja na uja uzito. Kama ukiwahi kwa dr( sio mwaka) unaweza kupata kinga ya maradhi na mimba pia.

Kuhusu kutoa mimba nakushauri ufanye kama nafsi yako inavyokutuma. Utaitolea wapi mimi sijui ungekuwa karibu nami ningekuonesha cha kufanya.

Kwanini uwe na wasiwasi wa, yeye kuambukizwa na huyo jambazi na sio yeye ndiye labda anaweza kumuambukiza huyo jambazi magonjwa ya zinaa?
 
Daaah, Mimi sikushauri hata chembe kuitoa hiyo mimba, japo inaweza kuwa vigumu kuilea peke yako, lakini jitahidi tu..

USITOE MIMBA.. USITOE TAFADHALI
 
It may be a parental accident but not divine accident.
Keep the baby, don't get down to your rapper level. You are not a killer. Give God all your pains and everything, He will take care of that.

What if after abortion you won't be able to concieve again?

Do you think the incident will go away after abortion? Nope you will have a double load I assure you.

Just pray ili Mungu akupe nguvu. Mtihani ulionao ndio utakaopeleka kwenye ushindi mkubwa maana unakuvusha kutoka kwenye watu wa kawaida kama mimi na kuwa mtu mwingine.

Mungu akusaidie.
 
Kwanza pole sana kwa yaliyokukuta Mpendwa
Ila mimi sikushauri kuua.Hebu fikiria tena
Kitu unachokutana nacho kwa bahati Mbaya katika Maisha yako,ndiyo kitu kinachokuwa na Msaada zaidi kwako.

Mungu anazidi kushughulika na wewe, bado kidogo utakuwa muhubiri mkubwa.
Ubarikiwe sana
 
Pole bibie kwa yaliyokukuta!
Ungewahi hospital mara baada ya tukio tuu wangekusaidia mengi,kuna Copper Intrauterine device ambayo ungeitumia ingezuia mimba hata cku 5 baada ya tukio
Kwa sasa utafute appointment ya daKtar kwa ushauri na uchunguz zaidi km una wazo la kutoa mimba akutoe kwa njia salama
 
Similar Discussions

Back
Top Bottom