Msaada: Nifuate taratibu gani kuanzisha nchi huru kanda ya ziwa? | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Msaada: Nifuate taratibu gani kuanzisha nchi huru kanda ya ziwa?

Discussion in 'Habari na Hoja mchanganyiko' started by spencer, Mar 30, 2011.

 1. spencer

  spencer JF-Expert Member

  #1
  Mar 30, 2011
  Joined: Nov 25, 2010
  Messages: 2,792
  Likes Received: 1,337
  Trophy Points: 280
  GreatThinkers!

  Haya ni mawazo yangu, ndiyo maana si yako. Nipe mawazo yako ili mimi niyachambue.

  CCM imeitenga kanda ya ziwa, natamani bora iwe nchi huru. nipeni procedure!

  Tunatumika tuu,gw'endakulima na Kagongwa wanakula vumbi la Buzwagi uwekezaji wa viwanda unarundikwa Kibaha.

  Kwa nini Dar Cement iwe 14000/= na Geita iwe 18000/= wakati Shinyanga kuna uwezekano wa kuweka kiwanda?

  Bora iwe nchi huru, hakuna Chuo kikuu(Public) huku. MAR, MZA, SIMIYU, SHY, GEITA, TABORA hivi inawaingia kichwa kweli kila kitu kiwe kanda ya mashariki?

  Ukisikia madini ya dhahabu wanachimba hadi kijijni kwetu G'wendakulima-Buzwagi iko pale, Kakola,Tulawaka,Geita,Mwadui na hata North Mara-Nyamongo

  Mawazo yamefikia huko maana naona hawa CCM wana mpango mbaya nadhani hata mnaotoka kanda zingine mtaniambia.

  Nipeni taratibu, nimechoka na huu wizi wa kuhamishia utajiri mwambao, aliyewaambia kuwa mkiweka kiwanda Kiabakari(MAR) au Tinde(SHY) kuwa hakitazalisha ni nani?

  Nimechoka kukaa na duku duku, kuna kila dalili kuwa Kaliua (TBR) wanalima Tumbaku lakini vijana wa Tabora hata kiwanda hakuna.

  Nasema yote haya kwa sababu sioni Tanzania ya wajukuu chini ya CCM ukoo wa McKamba na ******, bora tujitenge!

  Niktafakali huku tulivo RELI - VIWANDA-MADINI-USAFIRI WA ANGA-USAFIRI WA ZIWANI-ZAHANATI/HOSPITALI-SHULE/VYUO nk naamini sie hatuko Tz

  Nipeni mawazo, Nchi mpya izaliwe. Muone kama hata haitakuwa kama Rwanda.
   
 2. kilimasera

  kilimasera JF-Expert Member

  #2
  Mar 30, 2011
  Joined: Dec 2, 2009
  Messages: 3,073
  Likes Received: 17
  Trophy Points: 135
  utafanywa libya
   
 3. U

  Uwezo Tunao JF-Expert Member

  #3
  Mar 30, 2011
  Joined: Nov 14, 2010
  Messages: 6,947
  Likes Received: 12
  Trophy Points: 0
  Kwenda tu kijijini mtu mpaka kugonga mipaspoti mara kibao.
   
 4. s

  sawabho JF-Expert Member

  #4
  Mar 30, 2011
  Joined: Feb 25, 2011
  Messages: 4,502
  Likes Received: 946
  Trophy Points: 280
  Huwezi kuanzisha nchi ndani ya nchi mpaka uitwe Mwasi kama wale wa Libya, sasa uko tayari kuitwa Mwasi na matokeo yake?
   
 5. spencer

  spencer JF-Expert Member

  #5
  Mar 30, 2011
  Joined: Nov 25, 2010
  Messages: 2,792
  Likes Received: 1,337
  Trophy Points: 280
  Sasa mnanishaurije? Hali ndiyo kama hiyo!

  Kwani hakuna njia ya kidemokrasia ili niitumie?
   
 6. Jidu

  Jidu JF-Expert Member

  #6
  Mar 30, 2011
  Joined: Mar 9, 2011
  Messages: 1,167
  Likes Received: 302
  Trophy Points: 180
  hivi hizo bei ni toka enzi za mwalimu ama umekosea?
   
 7. FaizaFoxy

  FaizaFoxy JF-Expert Member

  #7
  Mar 30, 2011
  Joined: Apr 13, 2011
  Messages: 58,107
  Likes Received: 22,149
  Trophy Points: 280
  Anzisha maandamno, uukubali na mkong'oto!
   
 8. M

  Mdondoaji JF-Expert Member

  #8
  Mar 30, 2011
  Joined: Mar 17, 2009
  Messages: 5,106
  Likes Received: 45
  Trophy Points: 145
  Mkuu maneno yako makali mno!! msamehe hajui afanyalo.
   
 9. KakaKiiza

  KakaKiiza JF-Expert Member

  #9
  Mar 30, 2011
  Joined: Feb 16, 2010
  Messages: 10,548
  Likes Received: 2,263
  Trophy Points: 280
  Usiogope Google Msven or P.Kagame watakupa jinsi yakuanzisha nchi mbona kitu rahisi JWTZ wenyewe wako likizo na wengi walikufa na mabomu mbagala na gongolamboto na zaidi mabomu hawana!!!yote yaliteketea zama mwituni hapo kati mitaa yatinde kwenda bulyanulu!!
   
 10. spencer

  spencer JF-Expert Member

  #10
  Mar 30, 2011
  Joined: Nov 25, 2010
  Messages: 2,792
  Likes Received: 1,337
  Trophy Points: 280
  Mnanishauri niingie msituni hapo ni kweli naona nitakuwa kama muasi, watanifanya mbaya nataka taratibu zilizo ndani ya sheria.
  au nifungue kesi, Wapi?
   
 11. spencer

  spencer JF-Expert Member

  #11
  Mar 30, 2011
  Joined: Nov 25, 2010
  Messages: 2,792
  Likes Received: 1,337
  Trophy Points: 280
  Katiba yetu inasemaje kuhusu hili?

  Je mabadiliko ya katiba yanaweza kuwa tiba na jibu ya hili tatizo.

  Nilizaliwa katika kibanda cha nyasi, nimekulia katika nyasi, nilisoma katika mzambarau hadi leo kule kijijini hakuna kitu. madarasa hayajaezekwa wala madawati hakuna.

  inaonekana sitaenda mbali maana hata kujenga kijumba kwa wazazi ni shida, Msharaha wangu TGSD laki tatu, kazini natumia nauli 900kila siku. matumizi yangu hayanipi salio kabisa.

  Bado ni tatizo, wazazi nawahurumia pia.
   
 12. M

  Mkwele JF-Expert Member

  #12
  Mar 30, 2011
  Joined: Nov 23, 2010
  Messages: 206
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 0
  Subiri CDM ikingia madarakani utapata suluhisho, Be patient.
   
 13. spencer

  spencer JF-Expert Member

  #13
  Mar 30, 2011
  Joined: Nov 25, 2010
  Messages: 2,792
  Likes Received: 1,337
  Trophy Points: 280
  YAP!!
  Unamaanisha kutakuwa na na utawala wa majimbo?:teeth:
   
 14. Ndibalema

  Ndibalema JF-Expert Member

  #14
  Mar 30, 2011
  Joined: Apr 26, 2008
  Messages: 10,916
  Likes Received: 131
  Trophy Points: 160
  Na watu wa Lindi, Tunduru na Namtumbo nao muda si mrefu wataomba mawazo.
   
 15. m

  msosholisti Member

  #15
  Mar 30, 2011
  Joined: Feb 17, 2011
  Messages: 60
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  tena MARA ndiko alikozaliwa MWL nyerere. Vipi tena? wenyewe mnajisahau mkififika dar mnatafuta kujenga kimara bonyoka,mbezi msakuzi, halafu unalalamika. Turudi makwetu jamani? hata kama kijijini nenda kajenge hukohuko.
   
 16. T

  Thadeus JF-Expert Member

  #16
  Mar 30, 2011
  Joined: Nov 24, 2007
  Messages: 267
  Likes Received: 18
  Trophy Points: 35
  Tangaza nchi huru kwenye Radio Free Africa!!
   
 17. PakaJimmy

  PakaJimmy JF-Expert Member

  #17
  Mar 30, 2011
  Joined: Apr 29, 2009
  Messages: 16,236
  Likes Received: 309
  Trophy Points: 180
  Kweli watu wamemchoka mkwerekwere....jamani!
   
 18. AirTanzania

  AirTanzania JF-Expert Member

  #18
  Mar 30, 2011
  Joined: Mar 17, 2011
  Messages: 1,127
  Likes Received: 678
  Trophy Points: 280
  Na sisi kwetu Tanga tunataka kujitenga na serikali ya Kik wete, haina maana yoyote imeua viwanda vyetu vyote.
   
 19. Shomari

  Shomari JF-Expert Member

  #19
  Mar 30, 2011
  Joined: Mar 8, 2008
  Messages: 1,107
  Likes Received: 3
  Trophy Points: 135
  duh! maneno yako yanatia uchungu sana ukizingatia ni mkanda wa Ziwa, nahisi kutokwa machozi, unayosema ni kweli kabisa, atakayekupinga atakuwa hana uwezo mzuri wa kufikiri, Labda uende UN, Nyerere si ndio alianzia huko kudai uhuru wa Tanganyika? akatoa hotuba na kila kitu.
   
 20. p

  punainen-red JF-Expert Member

  #20
  Mar 31, 2011
  Joined: Nov 18, 2010
  Messages: 1,735
  Likes Received: 11
  Trophy Points: 0
  Heshima sana ndugu! Kama unatania au la sijui. Ila tu ujue tupo wengi tunaowaza namna ya kufanya, siku chache zilizopita nikiongea kwa simu na rafiki yangu nikashangaa ananiuliza swali hilo hilo! Naamini kwa sababu tuko watu kadhaa tunaowaza hilo tutapata njia tu.
   
Loading...