Msaada: Nifanyeje ili kumrudisha mpenzi aliyeniacha au avutiwe tena na mimi siku akiniona?

Kifaru86

JF-Expert Member
Apr 22, 2017
1,734
3,802
Tangu nimeachwa na mpenzi wangu nimekuwa nikipitia wakati mgumu kidogo kila nikifikiria sababu zilizimfanya mpenzi wangu kuniacha ambaye tuliwekeana malengo.

Ukweli ni kwamba huyu mdada bado ninampenda sijui nifanye nini ila nawaza ni jinsi gani ninaweza kumrudisha mpenzi wangu aliyeniacha nifanye nini?

Au ikitokea siku tumeonana au tumekutana nataka niweje ili aweze kuvutiwa na mimi akiniona ajione kama alifanya makosa kuniacha au apate wazo la kunirudia mimi
 
haipo hiyo brother
Labda umuwekee limbwata(kidding)

Mungu kama alikupangia awe wako basi uwe na hakika atakuwa tu!, regardless of the situation you're passing through.
Tulia,omba,akuonyeshe yapi ni makusudi ya mahusiano hayo...
Hii ni kwa wale wenye mlengo wa mahusiano yanayopelekea ndoa tu!
Kama ni yale ya kudate for fun basi usihangaike kufuata huu ushauri.
 
Kwa uzoefu nilio nao mwanamke akikuacha kwa sababu anazozijua mwenyewe kuna njia kuu tatu za kumrudisha

Njia ya kwanza tafuta pesa huu na anza kufanya vitu vya kimaendeleo hii ni njia ambayo wanawake huvutiwa sana

Njia ya pili ni badili muonekano wako uanze kuvaa vizuli na kupendeza lakini pia ubadili mwonekano wako akikuona moyoni

Njia ya tatu ni kumuombea mabaya atayempata baada ya wewe waachane kwa ugomvi au huko alipo penzi liwe limefeli
 
Kwa uzoefu nilio nao mwanamke akikuacha kwa sababu anazozijua mwenyewe kuna njia kuu tatu za kumrudisha

Njia ya kwanza tafuta pesa huu na anza kufanya vitu vya kimaendeleo hii ni njia ambayo wanawake huvutiwa sana

Njia ya pili ni badili muonekano wako uanze kuvaa vizuli na kupendeza lakini pia ubadili mwonekano wako akikuona moyoni

Njia ya tatu ni kumuombea mabaya atayempata baada ya wewe waachane kwa ugomvi au huko alipo penzi liwe limefeli
Naona unamfundisha mwanaume mwenzio uchawi haswa kipengele cha tatu hicho
 
Kama amekuacha kwa sababu za msingi na wewe umesababisha kama vile umeoa mke mwingine, amekufuma umecheat na matatizo ya kifamilia. Usilazimishe.

Hii inatoka na yeye kutokuwa single kwa maana atakuwa kwenye mahusiano tiyari na mtu mwengine.

Ushauri wangu kama wewe ndo umezingua mpaka akasepa basi ana haki ya kuondoka lakini kama yeye ndo aliyumba pia ana haki ya kurudi au kuondoka pia. Tambua mapenzi haya lazimishwi
 
Bado haujakubali uhalisia, hiyo ni moja tu ya stage baada ya kuachwa.

With time utaukubali ukweli na utakuwa vizuri.

Tulia tu, acha muda ukuponye wala hautahangaika kumrudisha.
 
Yaani demu akiniacha siwezi kurudiana naye hata iweje..Yaani haiwezekani

Fanya maisha yako mzee,watoto wakali wapo kibao tu mzee as long as upo determined na life lako
 
Kapige jiwe kama la laiser... hatokuacha daima na milele kufa na kupona kwenye raha...
 
Hivi msela una shughuli rasmi kweli? Kama huna jibidiishe upate kitu cha kuku keep busy hata kama ni kujitolea au ku tag ubavu golini kwa mtu!

Af mademu wanaozinguaga wahuni huwaga "vitoko" tu! Unakuta demu mmbovu kisefenge ila unamlilia stop that my friend. Hakuwa real nawewe huyo qooma,,,mpotezee man!

We ni wa thamani kuliko yeye ndio maana akajiengua. Tia hilo akilini af songa mbele mzee. Siku unapata demu mwengine mkali kinoma huyo mbuzi atajirudisha speed akiwa analia umsamehe. Wala usitumie nguvu we kauka tu! Mambo mazuri yako mbele af kaza kamba.

Kama ni mpenzi wa kujisomea tafta makala za Dan Bacon google ujifunze how to be a Man! Utasahihisha makosa yako na next time utajua uishi vipi na mwanamke ili asilete uxenge big time. Naona kuna makosa mengi ulishayafanya but ishi humo. The Modern Man ndio website ya jamaa. Thank me later! MSELA WA MANZESE
Naona umeamua ku mpump mwenzio. 😂😂😂 😂😂 eti wewe ni wa thamani
 
mahusiano ya kimapenzi mara zote hutumia fomula ifuatayo "kuna wakati unapaswa kumuacha unaempenda ili umpate anaekupenda" kwa hiyo usiumize sana kichwa mkuu.

nb: kumrudisha mtu unaempenda inawezekana kutegemea na mlivyo achana, kama ulikua ukimhudumia vizuri mahitaji yake na chumbani ulikua fit basi fanya yafuatayo kumrejesha...

andaa text nzuri zenye malalamiko ya kihisia juu yake then set alarm ifikapo usiku wa manane amka umtumie, text ijikite kueleza namna unavyoteseka kihisia juu yake hata ukawa unakosa usingizi usiku wa manane daily, fanya zoezi hili walau kwa wiki1 taratibu hisia zake zitarejea kwako na pia atakuona upo serious na hapo ndo utaibuka mshindi wa kinachokutesa.
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom