Entreprenuare
JF-Expert Member
- Aug 24, 2019
- 1,616
- 1,714
Nimeanza na ufugaji wa kuku aina ya kloiler, ninao 40, wa size tofauti tofauti. Sasa hii business nataka iwe ajira yangu,
Swali linakuja:
Je, nifanyaje, hii biashara iweze kunipa mafanikio ya kimaisha.. kama kujenga, kuwa na usafir binasfi etc.
Naombeni mawazo yenu, wataalam. Mm mgeni kwenye hii tasnia.
Ushauri wa wadau
Swali linakuja:
Je, nifanyaje, hii biashara iweze kunipa mafanikio ya kimaisha.. kama kujenga, kuwa na usafir binasfi etc.
Naombeni mawazo yenu, wataalam. Mm mgeni kwenye hii tasnia.
Ushauri wa wadau
Rudi mezani (mipango). Tengeneza malengo yako kisha hakikisha unayo yafuatayo;
1. Msukumo (drive)
2. Kujiamini (Confidence)
3. Maarifa (Know-how)
Pia kama uko serious sana na unataka uendelevu kwenye biashara hiyo basi yafuatayo ndiyo mihimi mikuu ya biashara yako;
1. Maendeleo ya biashara yaani business devt. Hapo utakuza biashara yako kwa kutatua matatizo makuu mawili;
I. Wateja wapya (new aquisitions)
II. Retention (hakikisha humpotezi mteja kirahisi)
2. Operations mgt. Hakikisha mipangilio sahihi ya shughuli zako kwenye ufugaji. Masuala kama chakula, chanjo, magonjwa, masoko, usafi, nk yapangiliwe vizuri. Vinginevyo muda wote utakuwa behind time.
3. Customer service. Uwe customer focused na siku zote tanguliza maslahi ya mteja kisha wewe ufuate. Hakikisha wateja unawahudumia vyema kama vile unavyohudumiwa ukipigaga simu customer care.
Mf, mteja anaulizia kuku na wewe huna. Usiishie tu kumwambia "kuku wameisha", bali mpe taarifa zaidi. Kwamba, " mimi sina ila waweza wapata sehemu flani, mimi nitakuwa nao baada ya mwezi hivi".
Mteja huyo usishangae akaahirisha kununua kuku mpaka pale wa kwako watakapokuwa tayari ikiwa halazimiki sana kununua kwa wakati huo, (true story).
4. Mwisho ni people management (HR). Hakikisha tangu mwanzo mwa mradi unachagua watu sahihi kuuzunguka mradi wako. Yaani wasaidizi pale utakapohitaji, wateja, washauri, wauzaji pembejeo, saplaya wa chakula, nk.
Ukifungamana na watu wasio sahihi mf wateja wasiokulipa au wafanyakazi wavivu, mradi wako utakwama na si unajua ng'ombe akikonda hachekwi yeye ng'ombe, unachekwa wewe mfugaji.
Kazi kwako.
Sent using Jamii Forums mobile app
Nakushauri. Nimefuga kuku kwa zaidi ya miaka 10. Gharama kubwa ziko kwenye chakula. Na bei huwa zinapanda sana na hazieleweki. Cha kwanza pata eneo la kutosha. Ifahamike kuwa sheria itakuja kuwabana wafugaji wa mijini kuhusu eneo la kufugia tafuta kuanzia hekari 5.
Pia utaweza kupunguza gharama za chakula kwa kuotesha baadhi ya vitu vinavyohitajika ikiwa ni pamoja ma majani kama mlonge au lukina au mulberry. Pia kama ni wa kienyeji utaweza kuwatoa nje wajitaftie.
Cha pili jenga banda ambalo litapunguza magonjwa na hivyo kukupunguzia matumizi ya madawa.
Cha tatu ili mradi wa kuku ukupe faida nono uunganishe na miradi mingine mfano mradi wa bustani na uzalishaji wa biogas au miradi mingine inayohusiana. Hapa nitaweka kiambatanisho cha kuonyesha mfumo wenyewe ukoje.
Chakula kinachukua asilimia kubwa sana hivyo ni vyema mfugaji akawa na stock ya kutumika muda mrefu au akaagiza moja kwa moja kutoka kiwandani ikiwa anafuga kwa kiwango kikubwa.
View attachment 1409082