Msaada: Ni wapi ninapoweza kununua engine kamili ya 1HZ na iliyo katika hali nzuri?

Complex

JF-Expert Member
Mar 20, 2013
4,113
4,741
Habari zenu wadau.

Kama kichwa cha habari kinavyoonyesha. Ni wapi naweza pata engine ya 1HZ iliyo katika ubora mzuri. Pamoja na swala hilo la ununuzi, pia ningependa kufahamu mambo yafuatayo juu ya hiyo engine.

1. Bei yake inaweza range kiasi gani?

2. Ni vitu gani vya kuzingatia katika ununuzi wa engine ili nisiuziwe engine ambayo ni janjajanja iliyotokana na magari yaliyokufa hapa Tanzaniayakachinjwa?

3. Ikipatikana engine iliyo katika hali nzuri, inaweza fanya kazi kwa muda gani bila kuanza usumbufu?

Kama kuna yeyote mwenye idea na wazo la wapi naweza kifanikisha hili nitamshukuru sana.
 
Complex,
Ukiagiza bei ipo juu kidogo endapo utanunua ambayo ni low mileage pamoja na kuisafirisha na kodi mpaka nchini.

Na kama unataka used kutoka Japan nenda Ilala bei inaanzia million 9. Ukienda Tandale unaweza ukapata kuanzia hata million 6 ila inakuwa imetumika kutoka kwenye gari zilizopata ajali na kukatwa hapa inabidi uende na fundi akague Cylinder head, maana cylinder head yake ni bei ghali kama 3 million. Akague kwa kuifungua cylinder head,piston,sleeve, pump na gear box.

Au unaweza ukaenda Tunduma kuna jamaa huwa anaenda Zambia kuchukua gari zilizopata ajali na kuzikata kama sikosei anaitwa Michael. Huyu anaweza akakutafutia engine iliyosimama kwa bei poa.

Engine ya 1Hz usiiogope haina magonjwa ya ajabu na inauvumilivu mkubwa pia spea zake zipo.

Ukiinunua ikiwa katika hali nzuri na kuitunza utatumia wewe mpaka wajukuu zako.
1HZ the best diesel engine of Toyota.
 
Offshore Seamen,

Asante sana kaka kwa msaada wako. Ningependa pia unisaidie katika haya chini.

Kuagiza toka japan engine ambayo ina low mileage inaweza fika kiasi gani ukijumuisha na kodi.?

Je used toka Japan inaweza fika kiasi gani kwa ilala.? Na vipi reliability yake, hawana uhuni wa kuvua spare genuine na kureplace na OEM spares.?

Vipi huyo michael wa tunduma bei zake zimekaaje.? How good engine zake zipo.?

Engine yenye low mileage unaijuaje..?

Nitangulize shukran.
 
Complex,
Kwa engine ya 1HZ usihangaike sana kutafuta low mileage kwa watu wa Ilala watakuongezea bei tu. Kama ukiagiza mtandaoni utaona wameandika km ilizofanya kazi.

1HZ haina mambo mengi wewe usiumize kichwa kwa kutaka yenye low mileage. Kama una connection na watu wanaonunua gari za bima zilizopata ajali watafute watakuuzia engine ya 1HZ iliyofungwa kwenye Coaster au Land Cruiser.

Kama unaweza Uganda kule Kampala engine ya 1HZ unaweza ukaipata kwa bei nzuri kwenye maduka ya spare wanaagiza used kutoka Dubai.
 
Complex,
Used toka Japan bei inaanzia million 9. Ilala kuna maduka ni waaminifu watakupa ofa ya guarantee kwa kipindi fulani na ikiharibika unaruhusiwa kurudisha na wakakubadilishia.

Engine ya low mileage kwa macho kuijua ngumu maana watu ni wajanja engine inasafishwa na kupigwa rangi ukiambiwa hii ilitumika km 50,000 wewe huwezi kubisha.
 
1HZ kuwa makini sije wakakupa toleo la zamani zile zenye mfumo wa Heater au Pre heater hizi zilitoka na Land Cruiser Series 75 (HZJ75). Ambazo kabla ya kuwasha lazima uchome heater ndio uwashe gari.

Hizi usumbufu wake ni Heater ikifa gari husumbua kuwaka na kila sehemu ya Piston kuna heater 1 kwaiyo inakuwa na Heater 6.
 
Mzee uko vzr kwenye mamb ayo

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Asante, Waweza nipatia recomendation ya baadhi ya hayo maduka yenye uaminifu.?
 
Mkuu naona umenongea vizuri sana ila nadhani 14B engine nazo zipo vizuri sana wengine wanasema ni bora kuliko 1hz.. nini maoni yako ya kitalaam.

Sent using Jamii Forums mobile app
Ni engine nzuri pia ila kwa mimi hii naona inafaa katika biashara ya daladala katika Coaster maana ni ulaji wake wa mafuta upo kawaida na haina magonjwa ya ajabu.

1HZ ina cc kubwa na ni 6 cylinder ila ulaji wa mafuta ni kawaida. 1HZ anakuwa bora kwa kuwa na speed na nguvu zaidi iyo 14B inachelewa kuchanganya.
 
Upo sahihi mkuu, ndio maana watu wa daladala wotewanakwambia ingine bora ni 14B.
Ni engine nzuri pia ila kwa mimi hii naona inafaa katika biashara ya daladala katika Coaster maana ni ulaji wake wa mafuta upo kawaida na haina magonjwa ya ajabu.

1HZ ina cc kubwa na ni 6 cylinder ila ulaji wa mafuta ni kawaida. 1HZ anakuwa bora kwa kuwa na speed na nguvu zaidi iyo 14B inachelewa kuchanganya.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
1HZ kuwa makini sije wakakupa toleo la zamani zile zenye mfumo wa Heater au Pre heater hizi zilitoka na Land Cruiser Series 75 (HZJ75). Ambazo kabla ya kuwasha lazima uchome heater ndio uwashe gari.

Hizi usumbufu wake ni Heater ikifa gari husumbua kuwaka na kila sehemu ya Piston kuna heater 1 kwaiyo inakuwa na Heater 6.
Kweli mshua alikuwa na liji land cruiser hardtop la Long time, nahisi ndio hilo HZJ75 la miaka ya 80 huko! Ilikuwa nikiliwasha lazma niweke kwenye ACC taa ya heater ikizima ndio napiga.
🤣🤣🤣🤣🤣 kumbe ni generation ya kizamani ile.
 
Back
Top Bottom