Msaada: Ni vigezo vipi vinahitajika ili kuwa Mkufunzi wa Chuo?

braity

JF-Expert Member
May 24, 2020
354
442
Naomba msaada wa mawazo ndugu zangu wana JF. Mawazo yenu yana faida kubwa sana. Ni mara ya pili naandika uzi unaofanana na huu lakini mara ya kwanza niliambulia patupu. Sikupata mchango wenu kabisa. Niliumia kidogo lakini nina desturi ya kutokukata tamaa.

Nakwenda moja kwa moja kwenye mada. Mimi ni mwalimu Grade A nimehudumu kwa muda wa miaka mitano kazini. Mungu mwema nimefanikiwa kupata shahada.

Nia na madhumuni yangu ni kurudi kukitumikia chuo nilichosoma grade A kama mkufunzi nitoke huku niliko. Matokeo yangu si mabaya sana kwani GPA yangu ni upper second 4+.

Kwa waliofanikiwa shida kama hii ya kwangu naomba msaada wa mawazo ni hatua zipi ambazo zitaniwezesha nifanikishe ndoto yangu. Natambua humu tupo watu wa kila aina wakufunzi wapo, viongozi wapo na wataalam mbalimbali wa Elimu. Naheshimu mawazo yenu.

Sent from my TECNO F3 using JamiiForums mobile app
 
Public University mahitaji ni:-

GPA 3.8 Undergraduate

GPA 4.0 Postgraduate
Mkufunzi kwa kiingereza ni Trainer, Universities hazina Trainers ila zina wahadhili, kwa kiingereza ni Lecturers! jibu lako laweza kuwa sahihi kama anataka kuwa Muhadhiri, na kinachozingatiwa zaidi ni GPA ya Undergraduate, Postgraduate sio sana hasa kama unaomba kuanza kama Assistant Lecturer au Tutorial Assistant!
 
Ukiwa na shahada ya kwanza utaajiriwa kama "Tutorial Assistant" kwenye vyuo vikuu (Universities) kwa GPA ya kuanzia 3.8 out of 5. Ukiwa na shahada ya pili utaajiriwa kama "Assistant Lecture" kwa GPA ya 4.0 out of 5. Ukiwa na PHD (hapa sijui huwa wanahitaji GPA ya ngapi), utaajiriwa kama "Lecturer". Wengi huwa wanaajiriwa wakiwa na shahada ya kwanza kisha wanajiendelea ili kupata sifa za kuwa Assistant Lecturer na Lecturer, na baadaye unakuwa Professor.​

Kwenye hivi vyuo vikuu vya kati (Coleges) e.g Colege of Business Education, na Taasisi za Mafunzo (Training Institutions) e.g Institute of Financial Managaement, ukiwa na GPA ya kuanzia 3.5 out of 5 wanakuchukua vizuri tu.

Kwa GPA yako ya 4+ na background yako ya ualimu utapata kazi kwa urahisi kabisa, labda wewe tu ushindwe kujibu maswali kwenye interview! Pia unaweza kuanza kujitolea kwenye chuo unachopenda kufundisha ili ajira zikitoka wakupe kipaumbele.
 
Shukrani kwa maelekezo yako mazuri Mungu akubariki sana ndg yangu. Lengo langu kubwa lilikuwa ni namna naweza pata nafasi katika vyuo vya diploma au certificate vya serikali. hata hivyo mimi ni muajiriwa tayari hivyo nilitaka nifahamu kama kuna mtu anaweza nipa maelekezo njia za kufuata niache huku nihamie sehemu Collage. Ahasante

Sent from my TECNO F3 using JamiiForums mobile app
 
Nenda kaongee na mkuu wa chuo unachotaka kuhamia kama anayo nafasi basi andika barua ya kuhamia pale itapitia kwa muajiri wako wa sasa
Kwa maelezo mfuate mkuu wa chuo atakuelekeza
 
Ili Kuwa Mkufunzi wa Chuo cha Ualimu sharti la kwanza unatakiwa uwe na cheo cha Muundo kinaitwa MWALIMU DARAJA 11 C na daraja la mshahara liwe TGTS E na Elimu uwe na Bachelor degree ila ukiwa na Masters ni vizuri zaidi kwan Masters ni (added advantage) . Sasa baada ya kuwa na sifa hizo unaandika barua ya kwanza kwa KARIBU MKUU Wizara ya Elimu ikipitia kwa DED(Mwajiri wako), DEO au DSEO (Afisa Elimu Sekondari au Msingi) then Mkuu wa Shule wako au Mwalimu Mkuu kwa shule za msingi. Hio barua itakua na KICHWA YAH: OMBI LA NAFASI YA UKUFUNZI KATIKA CHUO CHA UALIMU unaandika sifa zako humo na kuambatanisha barua zako za daraja la sasa (ambalo litaonesha upo na cheo cha Mwalimu Daraja 11 C au zaidi na ngazi ya mshahara TGTS E au zaidi) Hii barua inabidi uipeleke wewe mwenyewe Wizara ya Elimu ili kuwa na ufuatiliaji wa karibu maana watu wengi wanaandika hizo barua za maombi kama hayo ni vyema ukawaona maafisa wahusika ili ujieleze wakusaidie kuliko kuiacha tu masjala. Ukifanikiwa hapo watakuandikia barua ya kukujibu kuwa kuna nafasi na nafasi hio watasema kua unachukua nafasi ya nani kama ni Mtumishi aliyestaafu au kufariki au kuhama kada wakitaja na check namba yake huyo mtu. Wakikupa hio barua sasa ndio unaandika barua sasa kwa KATIBU MKUU MENEJIMENTI YA UTUMISHI WA UMMA ikiwa na kichwa YAH: OMBI LA KIBALI CHA KUHAMIA KUWA MKUFUNZI KATIKA VYUO VYA UALIMU WIZARA YA ELIMU barua hio kama nilivyosema utamwandikia KATIBU MKUU MENEJIMENTI YA UTUMISHI WA UMMA NA UTAWALA BORA itapita DED (Mwajiri wako) , DSEO au DEO , then Mkuu wa Shule wote hawa inabidi waipitishe . Utaandika humo ndani kuwa unaomba kibali cha kuhamia Wizara ya Elimu kuwa Mkufunzi katika Chuo cha ualimu na ukitaja sifa zako na nafasi uliopata kua utachukua nafasi ya mtu huyo unamtaja halafu katika barua hio unambatanisha barua ya nafasi, CV. vyeti, na barua ya cheo cha sasa na ikiwa imepitishwa kwa hao watu niliowataja ndio unaituma kwa KARIBU MKUU MENEJIMENTI YA UTUMISHI WA UMMA DODOMA . Kule ikiwafikia hua wanamfumo wao na namba zao za simu za huduma kwa wateja za bure kwa ajili ya kuwapigia utakuwa unawapigia ili kujua progress ya barua yako mpaka itakapotoka then kibali kikitoka wanatuma kwa Mwajiri wako (DED) Then unafungasha data zako na kuhama .
Ni hivyo tu nakutakia kila la Kheri katika mchakato huo ( unaweza kuniemail katika e-mail yangu majurayo@gmail.com kama utakua Bado hujaelewa vizuri.
 
Maelezo yaliyojitosheleza kabisa Ubarikiwe sana Kiongozi
 
Back
Top Bottom