Naomba msaada wa mawazo ndugu zangu wana JF. Mawazo yenu yana faida kubwa sana. Ni mara ya pili naandika uzi unaofanana na huu lakini mara ya kwanza niliambulia patupu. Sikupata mchango wenu kabisa. Niliumia kidogo lakini nina desturi ya kutokukata tamaa.
Nakwenda moja kwa moja kwenye mada. Mimi ni mwalimu Grade A nimehudumu kwa muda wa miaka mitano kazini. Mungu mwema nimefanikiwa kupata shahada.
Nia na madhumuni yangu ni kurudi kukitumikia chuo nilichosoma grade A kama mkufunzi nitoke huku niliko. Matokeo yangu si mabaya sana kwani GPA yangu ni upper second 4+.
Kwa waliofanikiwa shida kama hii ya kwangu naomba msaada wa mawazo ni hatua zipi ambazo zitaniwezesha nifanikishe ndoto yangu. Natambua humu tupo watu wa kila aina wakufunzi wapo, viongozi wapo na wataalam mbalimbali wa Elimu. Naheshimu mawazo yenu.
Sent from my TECNO F3 using JamiiForums mobile app