Msaada: Ni vigezo vipi vinahitajika ili kuwa Mkufunzi wa Chuo?

braity

Senior Member
May 24, 2020
163
250
Naomba msaada wa mawazo ndugu zangu wana JF. Mawazo yenu yana faida kubwa sana. Ni mara ya pili naandika uzi unaofanana na huu lakini mara ya kwanza niliambulia patupu. Sikupata mchango wenu kabisa. Niliumia kidogo lakini nina desturi ya kutokukata tamaa.

Nakwenda moja kwa moja kwenye mada. Mimi ni mwalimu Grade A nimehudumu kwa muda wa miaka mitano kazini. Mungu mwema nimefanikiwa kupata shahada.

Nia na madhumuni yangu ni kurudi kukitumikia chuo nilichosoma grade A kama mkufunzi nitoke huku niliko. Matokeo yangu si mabaya sana kwani GPA yangu ni upper second 4+.

Kwa waliofanikiwa shida kama hii ya kwangu naomba msaada wa mawazo ni hatua zipi ambazo zitaniwezesha nifanikishe ndoto yangu. Natambua humu tupo watu wa kila aina wakufunzi wapo, viongozi wapo na wataalam mbalimbali wa Elimu. Naheshimu mawazo yenu.

Sent from my TECNO F3 using JamiiForums mobile app
 

Kilembwe

JF-Expert Member
Aug 19, 2009
1,518
2,000
Public University mahitaji ni:-

GPA 3.8 Undergraduate

GPA 4.0 Postgraduate
Mkufunzi kwa kiingereza ni Trainer, Universities hazina Trainers ila zina wahadhili, kwa kiingereza ni Lecturers! jibu lako laweza kuwa sahihi kama anataka kuwa Muhadhiri, na kinachozingatiwa zaidi ni GPA ya Undergraduate, Postgraduate sio sana hasa kama unaomba kuanza kama Assistant Lecturer au Tutorial Assistant!
 

Mshua's

JF-Expert Member
May 22, 2013
731
500
Ukiwa na shahada ya kwanza utaajiriwa kama "Tutorial Assistant" kwenye vyuo vikuu (Universities) kwa GPA ya kuanzia 3.8 out of 5. Ukiwa na shahada ya pili utaajiriwa kama "Assistant Lecture" kwa GPA ya 4.0 out of 5. Ukiwa na PHD (hapa sijui huwa wanahitaji GPA ya ngapi), utaajiriwa kama "Lecturer". Wengi huwa wanaajiriwa wakiwa na shahada ya kwanza kisha wanajiendelea ili kupata sifa za kuwa Assistant Lecturer na Lecturer, na baadaye unakuwa Professor.​

Kwenye hivi vyuo vikuu vya kati (Coleges) e.g Colege of Business Education, na Taasisi za Mafunzo (Training Institutions) e.g Institute of Financial Managaement, ukiwa na GPA ya kuanzia 3.5 out of 5 wanakuchukua vizuri tu.

Kwa GPA yako ya 4+ na background yako ya ualimu utapata kazi kwa urahisi kabisa, labda wewe tu ushindwe kujibu maswali kwenye interview! Pia unaweza kuanza kujitolea kwenye chuo unachopenda kufundisha ili ajira zikitoka wakupe kipaumbele.
 

braity

Senior Member
May 24, 2020
163
250
Shukrani kwa maelekezo yako mazuri Mungu akubariki sana ndg yangu. Lengo langu kubwa lilikuwa ni namna naweza pata nafasi katika vyuo vya diploma au certificate vya serikali. hata hivyo mimi ni muajiriwa tayari hivyo nilitaka nifahamu kama kuna mtu anaweza nipa maelekezo njia za kufuata niache huku nihamie sehemu Collage. Ahasante

Sent from my TECNO F3 using JamiiForums mobile app
 

Doubleg Mwamasangula

JF-Expert Member
Feb 17, 2017
1,330
2,000
Nenda kaongee na mkuu wa chuo unachotaka kuhamia kama anayo nafasi basi andika barua ya kuhamia pale itapitia kwa muajiri wako wa sasa
Kwa maelezo mfuate mkuu wa chuo atakuelekeza
 

Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Top Bottom