Msaada, ni utaratibu gani wa kufuata ili kupata mirathi?

jjs2017

JF-Expert Member
May 25, 2019
2,023
4,213
Habari za wakati huu,

Naombeni mnisaidie ni taratibu zipi zinafuatwa wakati wa kufatilia suala zima la mirathi( yaani niende ofisi gani na gani).

Natanguliza shukrani.
 
Unafatilia mirathi kwa mara ya kwanza? muda tu baada ya kumpoteza marehemu au ni ya zamani ni malalamiko ya utekelezaji wa mirathi ?

Km ni issue mpya anza na kikao cha family then ukoo , mteua msimamizi, peleka mahakamani.

Km ni malalamishi nenda mahakama waliposajili hiyo mirathi
 
Cha kwanza ni Kikako cha familia/ukoo kumchagu mtu mmona ambaye ndio atakua MSIMAMIZI WA MIRATHI.

Hatua ya Pili ni kwenda Mahakamani ambapo utasajili mirathi na kuna muda unawekwa kama utapokea mapingamizi.
(Hapa kuna fast track ila siwezi andika hapa)

Tatu, kama sikosei mtakua na kikao cha mgawanyo wa mali. Kisha muhtasari utakua submitted mahakamani.

Mahakama itaziandikia barua benki, taasiisi, mwajiri kuwasilisha stahiki za marehemu.

Zikifika mtaitwa warithi wotw kuchukua cheque zenu as per ule mgawanyiko wa mali mlioandika.

(Ni zamani sana nilisimamia, nakumbuka kwa uchache, na hii ni provided familia haina migogoro)
 
Hapo kwenye cheque naomba ufafanue kidogo, nani atakuwa anawalipa cheque ?
Pesa yake ya benki na PSPF ilikua.

Hizo cheque zilikuja kwa amount based on percentage ya kila mtu anayerithi kama ilivyoandikwa kwwnye muhtasari na fomu fulani ya mgawanyo wa mali za marehemu.
 
Back
Top Bottom