Msaada: Ni namna gani ninaweza kupata "fully funded scholarship" nje ya nchi, mbali na kufaulu vigezo vyao?

d coy++++

Member
Jan 1, 2016
20
45
Habari zenu wakuu,

Mwaka jana niliona fursa za kusoma nje nkaamua nijaribu kuomba, ila sikupata, pamoja na kuambatanisha vigezo vyote na documents kamili zilizohitajika.

Mfano mzuri ni hizi 'full funded international scholarship' nyingi zinazokuwa chini ya mashirika na taasisi, mfano UNICEF, World bank, ecowas na embacy kadhaa.

Nataka niombe tena za mwaka huu ila nawaza ni kwanini mwaka jana nilikosa, nilifeli wapi?. Mimi nahitaji hizi 'full funded' kwa masters, maana sina uwezo wa kwenda mwenyewe pia mitaji hapa bongo inazingua nataka nkajiongeze huko kwa wenzetu.

Natumai hapa kuna waliopitia hizi njia au wenye uelewa juu ya kupata hizi "full funded international scholarships", naombeni sana msaada wenu wa kimawazo wakuu, maana kimsingi maisha mtaani yamenikaba sana.

Ahsanteni
 

Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Top Bottom