Msaada: Ni mwezi wa tatu sasa Mke wangu haoni siku zake na anahisi maumivu chini ya mbavu

Hash-baz

Member
May 26, 2020
5
2
Mke wangu haoni siku zake inakaribia miezi mitatu, analalamika kuhisi maumivu chini kidogo ya mbavu changa, kama kuchomwa na sindano.

Hii inaweza kuwa dalili ya tatizo gani ? Wapi naweza pata msaada mzuri zaidi, kwa maana ya hospitali!
 
Kupata maumivu chini ya mbavu changa ni dalili za magonjwa yafuatayo
1.Mimba ya nje ya kizazi
2.Uvimbe kwenye ovaries
3.Maambukizi katika mirija ya uzazi

Hivo nashauri kwanza apime yafuatayo
1. mimba kwa kile kipimo cha mkojo
2.Afanye ultrasound tuone nini tatz


Hivyo vipimo vitato majibu hasa

Kukabiliana na tatizi ya maumivu atumia dawa hii

Mefenamic acid PO 500mg tds 5days
 
Kupata maumivu chini ya mbavu changa ni dalili za magonjwa yafuatayo
1.Mimba ya nje ya kizazi
2.Uvimbe kwenye ovaries
3.Maambukizi katika mirija ya uzazi...

Daktari, asante. Umefafanua kuhusu maumivu vipi kuhusu kukosa hedhi, kunaweza sababishwa na hayo mambo mengine mawili ukiacha mimba nje ya kizazi ?
 
Daktari, asante. Umefafanua kuhusu maumivu vipi kuhusu kukosa hedhi, kunaweza sababishwa na hayo mambo mengine mawili ukiacha mimba nje ya kizazi ?
yaaah inawezekana, ila Mara chache, Mara nyingi uvimbe kwenye ovaries unasababisha kutokwa na damu nyingi au kupata mzunguko usioeleweka au kupata damu ya kidogo kidogo(spoting) sisi wataalamu tunamsemo unaitwa magonjwa hayasomi vitabu kwhy dalili ya kukosa hedhi ni uwezekano wa kuwa na uvimbe zaidi ya mmoja (polycystic ovarian syndrome)
 
Back
Top Bottom