MSAADA: Ni muda gani natakiwa kusubiri ili nianze kupata kadi na huduma NHIF?

Kwamteja mpya kwasasa Nikweli hadi siku 90 ndo apate kadi nakuanza kupata huduma mwanzo ilikua siku 30 kama sikosei ..wamegundua watu wengi wanakata bima baada yakuwa wagonjwa
 
Habari wanajamvi?

Kama nilivyokwishatangulia kuandika hapo juu,

Nisiwachoshe sana mojakwamoja niende kwenye mada ipo hivi;

Mimi nina mtoto (mwanangu) wa miaka miwili (2) mwezi wa tatu mwaka huu nilisafiri kwenda kwenye mizunguko yangu ya kibiashara nje ya mkoa.

Kutokana na changamoto za mtoto kuumwa mara kwa mara na mimi nikiwa safarini kutuma pesa muda mwngine huwa inakuwa changamoto, nikaona sio mbaya ili kuepusha usumbufu na kurahisisha mambo mengine hususani suala zima la afya ya mtoto nikaona nimkatie BIMA YA AFYA katika mfuko wa NHIF.

Hivyo majukumu yote nikwamwachia wife pamoja na pesa TSH 50,400/= akajaza fomu na kulipia tarehe 31/03/2020

Cha ajabu mpaka leo sijaona kadi yake na wala huduma hapati juzi ameumwa nimetoa pesa za matibabu kama kawaida na nikimuuliza wife ananiambia ameshalipa ila wamemwambia asubiri atapigiwa simu baada ya miezi mitatu kupita.

Hii imekaaje jamani au ndio utaratibu wao ulivyo hao NHIF? Au mke wangu ananiongopea? Au inakuwaje?

Kwa yeyote mwenye kufahamu katika hili naomba anifahamishe maana sijawaelewa hawa jamaa zetu wa NHIF
Kipindi cha nyuma ilikuwa unasubiri mwezi mmoja Ila kwa ss unasubiri miezi 3 boss

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Back
Top Bottom