Mashine ya kilimo cha umwagiliaji

Kamakabuzi

JF-Expert Member
Dec 3, 2007
2,859
1,301
Naoma msaada wenu wadau.

Nina mpango wa kuanzisha kilimo cha umwagiliaji, natakiwa kusukuma/kuvuta maji kwa umbali wa mita 250 (hakuna mwinuko mkubwa) halafu niyapandishe juu urefu wa mita 6 ili yaingie kwenye simtank, tayari kwa umwagiliaji.

Eneo langu linweza kufikia eka 6. Je ninunue mashine yenye ewezo gani (HP), kama kuna anayejua aina nzuri ya mashine naoma anisaide pamoja na bei pia upatikanaji wa spares ni muhimu.

Asanteni
 
Mkuu una mawazo sawa na ya kwangu. Ebu jaribu kwenda kwa watu wa idara ya maji wanaweza kukupa ushauri mzuri maana wao ni fani yao, hata mimi nina mpamgo wa kuwatafuta
 
Wewe unapatikana wapi? kama uko Dar es salaam tuwasiliane kupitia 0655746067
 
Naoma msaada wenu wadau.

Nina mpango wa kuanzisha kilimo cha umwagiliaji, natakiwa kusukuma/kuvuta maji kwa umbali wa mita 250 (hakuna mwinuko mkubwa) halafu niyapandishe juu urefu wa mita 6 ili yaingie kwenye simtank, tayari kwa umwagiliaji.

Eneo langu linweza kufikia eka 6. Je ninunue mashine yenye ewezo gani (HP), kama kuna anayejua aina nzuri ya mashine naoma anisaide pamoja na bei pia upatikanaji wa spares ni muhimu.

Asanteni

Natumia nchi mbili ila haina pressure kubwa sana,kupandisha maji juu ya tanki.unafanya umwagiliaji kwa njia drips?
 
Hapana, nataka kumwagilia kwa kutumia mipira ya kawaida au ikiwezekana sprinklers, Sababu ya kutaka kuyapandisha kwenye tanki juu, ni kupunguza uwezekano wa kuwasha mashine kila unapotaka kumwegilia (tank linakuwa kama storage fulani, yakiisha ndio nasukuma mengine)
Bila shaka nimeeleweka; naomba ushauri wako
 
Natumia nchi mbili ila haina pressure kubwa sana,kupandisha maji juu ya tanki.unafanya umwagiliaji kwa njia drips?
Kama hiyo inchi mbili haina pressure sana, itaweza kuyapandisha kwenye tank?
Nafikiria labda ninunue ya inchi tatu ivute kutoka kwenye chanzo, halafu pale kwenye outlet nifunge reducing socket itakayopunguza diameter toka inchi tatu hadi mbili ili kupata pressure kubwa zaidi - yaani bomba la kusafirishia maji liwe inchi mbili wakati mashine ni inchi tatu, Wasiwasi wangu hapo ni labda pressure inweza kuwa kubwa na ikapasua mabomba.
Mabomba nataka kunua HDPLE pipes class C.
 
Mkuu unaweza kujua bei yake inaanzia ngapi.
Pia tujulisha upatikanaji wa spares, maana mashine nyingi za kijapan spares ni shida, angalia kwa mfano pikipiki honda XL 125s, Spares za shida sana
 
Habari zenu ndugu wapiganaji wenzangu!!
Nataka kununua mashine kwa ajili ya kilimo cha umwagiliaji, naomba ushauri wenu ni mashine ipi itanifaa..na pia ni vitu gani ambavyo inabidi niviangalie kabla ya kuamua kuwa ni mashine ipi niitumie!!
asante.
 
Habari yako ndugu,
Ndugu swahili lako halijajitosheleza inaweza ikawa ngumu kupata msaada.

1.Ili kujua usaidiwe vipi nipazima kujua chanzo chako cha maji, namaana hayo maji unayotegemea kutumia kwa kilimo unayatoa wapi? Sababu pump unayoweza kutumia kutoa maji mtoni au kwenye bwawa tofauti na pump ya kisima cha kudumbukiza.

2. Angalia umbali kutoka chanjo cha maji.
3. Nishati gani utatumia kuendeshea pump hiyo. ( umeme, mafuta, soral nk)
4. Mfumo gani gani unatumia kwa kumwagia but hilo sio muhimu sana.

Utakaporudi na majibu ya haya tunaweza kumushauri vizuri zaidi.
 
Habari zenu wadau, nataka kununua mashine ya kumwagilia nina shamba la ekari mbili (2). Naomba mnijuze Aina nzur, size, na horse power ngapi na vingine vya muhimu. Asante
 
Ndugu maelezo yako hayajajitosheleza. Inamaana unahitaji pump? Kama ndio kuna aina 2 za pump ya juu ya ardhi na chini ya ardhi ili kuzitofautisha pump hizi nilazima tujue chanjo cha maji kwenda shambani.

Kama utakuwa unatumia chanzo cha maji kama bwawa, rambo, mto au kisima kisichozidi kina cha 8 mpaka 10 unaweza kutumia pump za kawaida tu ambazo kariakoo zipo kaushiki, honda na nk, ambapo ukienda dukani mara nyingi watakuuliza ni nchi moja nanusu au nchi 2.

Hapo kuna namna mbili unaweza ukatumia moja kwa moja wakati wakati unavuta maji ukamwagia kwa wakati huo huo. Nawengine wanatumia njia hii kwenye mfumo wa drip irrigation.

Njia yapili kama unatumia mfumo wa drip irrigation kwanjia ya gravit itakulazimu hayo maji yatakapokuwa yanatolewa kwenye chanzo kwenye matank yalio juu usawa wa mita 3 mpaka 4 kutegemeana na ukubwa wa eneo la umwagiliaji ili utakapotaka kumwagilia maji yashuke kwa gravit.

Pump nyingine ni pump za chini ya ardhi hizi hutumika kwenye vyanzo vya maji vilivyo chini ya ardhi ninamana visima virefu. Hapa sina maelezo sana sababu maelezo yake nikama hayo mengine niliotoa huku juu.

Ndugu nimekupa mwanga kidogo utakaporudi tena kufafanua vizuri unachohitaji. Pia watakuja wajuzi zaidi kukupa maelezo yakutosha na kunirekebisha au kunikosoa pale nilipokosea.

Nakutakia kila lakheri na mafanikio.
 
Nipe pesa nikuuzie ninayo mkuu nimeinunua mwaka jana nikaitumia kulima misimu miwili ya tikiti basi.
 
Asante kwa maelezo, Nataka pump ya katoka kwenye mto kuja shamba
 
Back
Top Bottom