Msaada ndoto zinanifanya na kuwa hofu

habari ya hapa

JF-Expert Member
Dec 20, 2012
12,791
8,743
Heshima kwenu mabibi na mabwana, bila kupoteza muda km mada tajwa hapo juu inavyosomeka ni kwamba, Mara nyingi nimekuwa nikiota ndoto baada ya muda kuna tukio lina tokea japokuwa huwa siletewi picha moja kwa moja ila mazingira ya ndoto na baada ya tukio halisi kutokea ndipo hupata picha kamili.

Ukweli sipendi hii hali kwani imenijengea hofu na woga mwingi, kwa Mara nyingine tena wwkati nimelala usiku wa kuamkia leo nilipata kuota ndoto, niliposhtuka sikupata tena usingizi hata kulipokucha, nilijiuliza maana yake nn ile ndoto lkn sikupata majibu, nikaishia kujifariji tu nakuendelea na shughuli zangu, ilipofika mchana nilipata simu toka kwa ndg yangu mmoja kuwa anatatizo, kwa vile sikuwa mbali na alipo nilimwambia anisubir, kufika pale hali mazingira niliyomkuta nayo na maneno aliyokuwa akinambia tayari nikaikumbuka ndoto niliyoota usiku, sitaki kusema kwa undani sana,

Nifanyeje nisiwe naota, kwani nimekuwa nikiota misiba na kweli inatokeA, au kuna MTU ataumwa na inakuwa, sipendi hii hali inanifanya nakuwa ktk mazingira magumu,
 
Mimi sidhani kama kuna shuda kwenye hili, kuna wito fulani kwako kwaajili ya kusaidia watu, kaa chini tafakati, pata muda wa faragha alone, talk to your inner person, tafuta kujua kusudio la hizi ndoto ni nini. Angalia history ya maisha yako tangu utotoni, je kuna maagano yoyote yaliyofanywa na wazazi wako juu yako.
Naomba mumuite mshana hapa kwa ajili ya hili,
 
Mkuu shida inakuja pale nipoota kuna kifo kitatokea ktk familia na kweli baada ya siku kadhaa anaondoka mzazi, au kaka, mjomba nk, hapa tu ndo panifanya nikose aman,
 
Kabla ya baba kufariki niliona wiki moja kabla nika puuza, ikatokea tena kwa bibi, mjomba, kaka na inaendelea, inanipa wakati mgumu sana
 
Heshima kwenu mabibi na mabwana, bila kupoteza muda km mada tajwa hapo juu inavyosomeka ni kwamba, Mara nyingi nimekuwa nikiota ndoto baada ya muda kuna tukio lina tokea japokuwa huwa siletewi picha moja kwa moja ila mazingira ya ndoto na baada ya tukio halisi kutokea ndipo hupata picha kamili.

Ukweli sipendi hii hali kwani imenijengea hofu na woga mwingi, kwa Mara nyingine tena wwkati nimelala usiku wa kuamkia leo nilipata kuota ndoto, niliposhtuka sikupata tena usingizi hata kulipokucha, nilijiuliza maana yake nn ile ndoto lkn sikupata majibu, nikaishia kujifariji tu nakuendelea na shughuli zangu, ilipofika mchana nilipata simu toka kwa ndg yangu mmoja kuwa anatatizo, kwa vile sikuwa mbali na alipo nilimwambia anisubir, kufika pale hali mazingira niliyomkuta nayo na maneno aliyokuwa akinambia tayari nikaikumbuka ndoto niliyoota usiku, sitaki kusema kwa undani sana,

Nifanyeje nisiwe naota, kwani nimekuwa nikiota misiba na kweli inatokeA, au kuna MTU ataumwa na inakuwa, sipendi hii hali inanifanya nakuwa ktk mazingira magumu,
Mkuu wewe Ni Mganga WA Kienyeji ajaye!
 
Ndoto ni taarifa kamili ya kiroho juu ya jambo lililombele yako au jamaa zako na linatakiwa litokee kimwili. lengo la ndoto ni kukupa taarifa ili uchukue hataua, hivyo hutakiwi kuogopa bali shukuru kwa kuwa wewe ni mlango wa kuokoa wengine katika familia yako. ukiwa unaota ndoto juu yako na watu wengine ujue wewe ndiye mwenye majibu yao, rohoni wewe ni lango la kuwafungulia wengine au kuwafungia mambo yao.

Mungu akipitisha ndoto mbele yako, ujue unahitajika kuijua ndoto hiyo na kuhakikisha unaupata ujumbe halisi ndani yake na kuufanyia kazi, na kushinda .Yaweza kuwa onyo ujirekebisha, shambulizi umbambane, taarifa ujiandae, ujumbe umpeleke mtu, fursa ujipange kuichukua na nk

Kikawaida ndoto inaweza kuwa ya KIMUNGU au kishetani, yaani ni MUNGU anakupa ujumbe au shetani anakupa ujumbe lakini hakuna ndoto ya bure, yaani ndoto isiyo maana, Kitabu kitakatifu cha biblia kinathibitisha kuwa ndoto nyingi zilizootwa kama ujumbe wa MUNGU kwa watu, lakini ni marachache mtu huota kwa sababu ya mihangaiko yake ya maisha. Hivyo usidharau ndoto.

Ndoto inayokutisha mara nyingi ni msukumo wa rohoni kuwa jambo hilo lipo karibu na litatokea, ukiota ndoto inakusumbua kila mara maana yake chukua hatua jambo hilo lipo linakuja, au anaota ndoto hiyo hiyo zaidi ya mara moja, usidharau chukua hutua.

Unachukuaje hatua,
Kwasababu ndoto ni jambo la rohoni, then ili uwe mjuzi wa mambo hayo lazima uwe mzuri rohoni, yaani uwe na nguvu zakiroho za KIMUNGU au uwe na maarifa ya kutosha rohoni. waweza kupata kwa kusoma vitabu vitakatifu kama biblia, kusilikiza mafundisho ya Mungu na jambo hili sio la kupata mara moja utakuwa mahili kadili ya juhuhi yako

Pia omba MUNGU akupate maarifa hiyo na nguvu ya kujua tafsiri za ndoto hizo utapewa na utaanza kujua.

Ukishindwa waone watu walitangulia rohoni yaani tayari wanayo hiyo maarifa, biblia inasema mtu akiota ndoto na hajui maana aipeleke kwa makuhani wamsaidie kujua naye atende sawa sawa na atakavyo ambiawa.
 
Ubarikiwe sana mkuu, Kwa masuala ya rohoni nahitaji kufunzwa sijui chochote mkuu, nitachukuaje hatua nimeota utapata ajali, kuumwa hata kifo nitakufikishiaje huo ujumbe ili nielewke kwako maana kumwambia mtu nimeota unaweza kufa hivi karibun unaweza itwa mchawi, nitachukuaje tahadhari kukunusuru
 
Sifa na utukufua apewe MUNGU atupendaye sana kuliko sisi wenyewe tunavyojipenda na tena ndiye atupaye hiyo maarifa ya kujua na kutafsiri ndoto.
Mungu hafanyi jambo lolote isipokuwa kwa neno, vyote viliumbwa kwaneno la MUNGU na Mungu pia ni neno, Ukitaka kujua mambo mengi ya MUngu lijue vizuri neno lakila eneo la maisha yako, kwa maana nyingine uijue vizuri bible na maneno yaliyo ndani yake, maana huko ndiko zitokako chemichemi za maarifa, mfano Mungu anasemaje kuhusu elimu, au anasemaje kuhusu ndoa, au anasemaje kuhusu kifo, au anaesemaje kuhusu wewe kumiliki mali na nk.

Ndoto zinafumbuliwa na maneno ya Mungu ongeza mazingira ya ndoto, mfano umeota kifo, inawezekana unaambia mbele yako kuna roho ya mauti, either ya roho yako, au ya mwili wako au vyote viwili, au kuna jambo lako la muhimu kimaisha litakufa au utapata hasara, au jambo unalolitegemea litaharibika, au cheo chako kitakufa au mzizi wa matumaini yako itakufa, ndiyo maana ukichanganya mazingira ya ndoto au juu ya jambo la hitaji lako ulilomuomba Mungu au jambo linalokutatiza sana itakuwa rahisi kujua hiyo maana.

Vilevile kupata ajali, sio lazima iwe ajali ya vyombo vya usafiri, japo inaweza kuwa, lakini inaweza kumaanisha kikwazo cha maisha. Na ukiota ndoto inayo muhusu mtu, kwa mfano umeota ndugu yako amekufa, sio lazima kuwa atakufa kimwili japo inaweza kuwa rejea maelezo ya juu, lakini lengo kuu la MUNGU ni kuwa wewe upo kwenye nafasi nzuri ya kumsaidia kuliko yeye, na ndiyo maana hakumwambia yeye na kwa maana hiyo wewe tafuta majibu na tatua shida hiyo bila hata yeye kujua maana aliyekuambia wewe hajamwambia yeye wakati yupo. Hivyo usijidai kwenda kumwambia kwani unaweza kumua kwa shinikizo na hofu. Ispokuwa kama Mungu atakupa msukumo wa kwenda kumwambia kwa sababu anaweza kukupa msukumo huo. kama hukupi komaa tafuta majibu na toa suluhu.

Kwahizo ndoto ulizoota tumia kama siku tatu Muombe mungu akusaidie kujua maana au akupe mtumishi atakaye kusaidia kujua zaidi na huo utakuwa mwanzo wako wa kujua maana za ndoto soma haya kujenga msingi.
Farao (Mwanzo 41:1)
Nebukadreza (Daniel 4:4-5)
Mkewe Pilato Mathayo (27:17-19)
Kornelio (Matendo 10:1-4).

Ukiota ndoto mbaya sana nayakutisha mfano, unakula nyama za watu, unafanya mapenzi na wanawake au wanaume usiku, unakimbizwa, unafukuzwa na nyoka, unatumbukia kwenye shimo la kutisha na nk, mara nyingi hizi ni kazi ya kishetani na uchawi lakini zina kuonyesha kuwa unashambuliwa na nguvu za giza. Kwa maana nyingine nguvu zako za KIMUNGU zinadhohofishwa usiweze kutenda matenda ya KIMUNGU na nguvu za kishetani zinaimariswa ili utende ushetani zaidi kwa maana nyingine umuasi MUNGU zaidi ili usifaidi matunda ya wewe kwenda kwenye nyumba za ibada kuomba na kumuuadudu MUNGU wako, zinakaribisha mikosi, nuksi na mabo kadhaa wa kadhaa ya kiovu.

Hapa nikukemea na kumuombaMUNGU akuokoe, Biblia inasema mkariieni Mungu, Mpingeni shetani naye atawakimbia, hivyo jisogeze kwa MUNGU na kemea hayo madudu sure yatakuacha.
 
Kuna Mmoja katika familia yenu anawechezea atakuwa ni mtu anae kufahamu vizuri undani wako,sasa ame disturb spirit yako kwa upande wa pili nnavyo faham hofu ikikuanza tu na ikawa cronic kila muda una hofu basi jibu ni hilo.
 
Ukiota ndoto mbaya hakikisha asubuhi na mapema unamwambia mtu hata kama hatokuwa yule muhusika uliemuota basi inaaminika kwa kufanya hivyo ndoto ile haitoweza kuja kuwa kweli ila ukikaa kimya itakuwa kuwa kweli...Na wakati huohuo ukiota ndoto njema ama nzuri hakikisha haumwambii mtu ili ije kuwa kweli..
 
Nilipokuwa mdogo nikawa natamani sana kwamba, laiti ningeishi miaka ya manabii wa Biblia, kwamba nami huenda ningekuwa naongea na Mungu. Sasa nilipokuwa mkubwa pasipo kutarajia, nikaanza kuota matukio mbalimbali, ambayo kweli huwa yanatokea. Kama mdau alivyoshauri hapo juu, yawezekana kuna agano ulifanya au lilifanywa na wazazi wako juu yako. Yawezekana walikukabidhi mbele za Mungu ukiwa mdogo, na Mungu sasa anakuandaa kufanya kazi yake kwa njia hiyo.
 
Hupendi kuota???na ilihali yote unayoota yana ukweli ndani yake, labda hujakua na huelewi maana ya ndoto nakushauri kabla hujaaribu nyota yako tafuta mzee wa busara ambaye una uhakika ni mwelewa ila asiwe mchawi atakufundisha mengi kuhusiana na elimu ya unajimu
 
Back
Top Bottom