Msaada ndani ya rasmu ya katiba (wenye maswali mengine mwaweza tupia hapa ili twende pamoja)

bnf

JF-Expert Member
Oct 13, 2012
218
195
ukipitia vipengele vyote

zanzibar inatambulika kama jamhuri ya watu wa zanzibar

tanganyika inatambulika kama jamhuri ya tanganyika

swali ni kwamba mbona tanganyika aijitambulishi kama jamhuri ya WATU wa tanganyika?

nini kimejificha hapo?

au zanzibar ni mali ya wanzanzibari na tanganyika ni mali yetu sote?

au hapa ndo pamejificha hoja ya mtanganyika hutaruhusiwa kuwa na ardhi zanzibar?

kwa nini moja iwe jamhuri ya watu na nyingine iwe jamhuri inayoelea?

Naombeni hoja zenu wakuu
 
Fenento

JF-Expert Member
Oct 21, 2010
320
225
Mimi sinatatizo la hilo jina, isipokuwa tunatakiwa na kuwa na katiba ya Tanganyika ambayo haina tena huruma juu ya hawa wenzetu, ninamaanisha, kama tunaenda zanzabari kwa kutumia passport basi na wao kuja Tanganyika iwe hivyo hivyo, na maanisha jino kwa jino hakuna msamaha hadi kieleweke kwa sababu haya wameyataka wenyewe.
 
MFUKUZI

JF-Expert Member
Mar 1, 2011
934
1,000

Naungana na wewe kiongozi hayo ni majina!!. Lakini kwa hadhi ya Utanganyika na Uzanzibari katiba imeweka usawa kila mtu anahaki ya kwenda popote kwa hiyo lile katazo la kuwazuia wabara kununua ardhi Zanzibar limeondolewa,,,... Mimi nadhani iko poa sana... Sema sasa mchakato wa kupata Katiba ya Tanganyika kwa maana ya Bunge, Mahakama na Serikali ya Tanganyika unatakiwa uanze faster ili kuokoa rasilimali zetu... Na ukiangalia kwa makini hoja ya CHADEMA juu ya Kanda inaelekea kuwa na mashiko
 
peche luke

JF-Expert Member
Sep 8, 2013
365
0
Suala la uraia waTz linatakiwa liwe mwanzoni kama lilivyo suala la mipaka ya nchi na nchi yenyewe ya Tz.
 
JF-MBUNGE

JF-Expert Member
May 1, 2012
421
0
Kimsingi sioni mantiki ya serikali tatu...kama ni muungano basi tuwe na serikali moja ya muungano na imetosha, then rais awe mmoja wengine wawe makamu inatosha.

Sioni mantiki hata chembe ya nchi yetu masikini kama hii kuwa na serikali tatu na ma rais watatu.

Kwanza istoshe maelezo ya katiba zetu hii mpya na hata iliyopita ni mazuri sana kwa kuyasoma tatizo lipo kwenye utekelezaji je yaliyomo yanafatwaa..????????

Hivyo hata katiba inayokuja iwe na maneno ya kutia moyo kiasi gani kama nidhamu na mambo ya msingi yanayodidimiza nchi kiuchumi hayachukuliwi hatua stahiki kama katiba inavyosema ni kama kupiga deki bahari.

Mie napendekeza serikali mojimbi mawili zanzibar na tanganyika ..kama haiwezekani basi silikari mbili kila nchi kivyake that is workable.
 
Mbona unakiririshwa vibaya? Aliyekwambia Serikali tatu itakuwa na gharama kubwa kuliko liserikali la sasa lenye Mawaziri karibu 60, wakuu wa mikoa 25, wakuu wa wilaya 120, Makatibu Wakuu karibu 65 nani.... Akili za kuambiwa changanya na za kwako, hiyo hoja ilikuwa ni ya CCM kutaka kuhahalisha utawala wao wa kifisadi ambao umeshindwa kuwaondolea matatizo watanzania kwa zaidi ya miaka 50.

Katiba ya sasa inapendekeza Serikali ya Muungano itakuwa na Mawaziri wasiozidi 15... Wabunge 75 kwa hiyo ukipiga mahesabu ya Serikali ya Muungano haitakuwa na watumishi zaidi ya 120 (Mawaziri, Makatibu Wakuu na Wabunge) Ukija kwa upande wa Tanganyika Katiba yake itasema kama ni kuendelea na majimbo yaliyopo au la... lakini suala la Wakuu wa Mikoa na Wilaya limeshazikwa...
 
ANT JAY

Member
Dec 31, 2013
34
0
xawaaa mkuuu nakubaliana na mchango yenu kuunda katiba je? inatekelezwa kama inavyo stahiki?
je! wanaoenda kinyume na katiba wachukuliwa hatua mathubut?

hebu naomba 2sichangie maoni ya kuunda rasimu ya katiba halafu wanaoenda kinyume mnawavumbia macho et ooh cjui ndugu, cjui maraf 2angilie kwa hil
 
Crashwise

JF-Expert Member
Oct 23, 2007
22,220
2,000
Mbona unakiririshwa vibaya? Aliyekwambia Serikali tatu itakuwa na gharama kubwa kuliko liserikali la sasa lenye Mawaziri karibu 60, wakuu wa mikoa 25, wakuu wa wilaya 120, Makatibu Wakuu karibu 65 nani.... Akili za kuambiwa changanya na za kwako, hiyo hoja ilikuwa ni ya CCM kutaka kuhahalisha utawala wao wa kifisadi ambao umeshindwa kuwaondolea matatizo watanzania kwa zaidi ya miaka 50.

Katiba ya sasa inapendekeza Serikali ya Muungano itakuwa na Mawaziri wasiozidi 15... Wabunge 75 kwa hiyo ukipiga mahesabu ya Serikali ya Muungano haitakuwa na watumishi zaidi ya 120 (Mawaziri, Makatibu Wakuu na Wabunge) Ukija kwa upande wa Tanganyika Katiba yake itasema kama ni kuendelea na majimbo yaliyopo au la... lakini suala la Wakuu wa Mikoa na Wilaya limeshazikwa...

mpaka hapo tuna pesa ya wakuu wa mikoa na wilaya na mashangingi yao..
 
Mshombsy

JF-Expert Member
Mar 15, 2013
372
0
Ni mbwembwe tu hizo jamhuri ni jamhuri ila tofauti ni muundo wa jamhuri kwa maana ya mgawanyo wa madaraka tofauti kati ya mihimili mitatu ya dola.

Vilevile unaangalia na uhuru wa taasisi za umma kama polisi nk.

Jamhuri hasa za kileo (mfano Marekani) zinatilia mkazo madaraka zaidi kwa wananchi.
 
Genekai

R I P
Feb 9, 2010
12,532
2,000
Kimsingi sioni mantiki ya serikali tatu...kama ni muungano basi tuwe na serikali moja ya muungano na imetosha, then rais awe mmoja wengine wawe makamu inatosha.

Sioni mantiki hata chembe ya nchi yetu masikini kama hii kuwa na serikali tatu na ma rais watatu.

Kwanza istoshe maelezo ya katiba zetu hii mpya na hata iliyopita ni mazuri sana kwa kuyasoma tatizo lipo kwenye utekelezaji je yaliyomo yanafatwaa..????????

Hivyo hata katiba inayokuja iwe na maneno ya kutia moyo kiasi gani kama nidhamu na mambo ya msingi yanayodidimiza nchi kiuchumi hayachukuliwi hatua stahiki kama katiba inavyosema ni kama kupiga deki bahari.

Mie napendekeza serikali mojimbi mawili zanzibar na tanganyika ..kama haiwezekani basi silikari mbili kila nchi kivyake that is workable.

Inawezekana huoni mantiki ya 3 ila watz wakiamua huna jinsi. Kuacha kufanya ya msingi kwa visingizio vya GHARAMA wala haikubaliki.

Huu mwaka mtahama nchi, 3 hazikwepeki!
 
mkandi

JF-Expert Member
Feb 28, 2012
281
250

Mantiki inatokana na mktadha wa sasa mkuu.
Wao hawataki 1, sie hatutaki 2.
Kina Warioba hawaruhusiwi kuvunja muungano (may be could be best option).
The only option available ni serikali 3.
 
Jul 19, 2013
48
95
Kama kawida JF MBUNGE uvivu wa kufikiri hasa kwa watanganyika ni tatizo kubwa wameachia mafisadi wawakaririshe manano kama yako eti nchi yetu bado changa ni masikini nanyi mnakariri hivyo hivyo bila kuongeza hata na akili yako ya ziada ya kuzaliwa nayo. Loh! maskini Tanganyikaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaa katika bara la Africa nchi hii ina utajiri hakuna mfano. ila akili za wananchi wake ndiyo maskini (eti hatuna uwezo kuendesha serikali 3) rasilimali yote wanabeba wageni mnaachiwa mahandaki tu wakati mnaendelea kuimba nchi yetu maskini. SERIKALI 3 LAZIMA
 
Nashukuru kwa kuandika kwa ushabiki bila hoja kwanza nikujibu we unaona nimekarilishwa lkn mie naona wewe ndio umekarilishwa ''nchi yetu ina rasilimali nyingi na sie ni matajiri lkn mafisadi na wageni ndio wanabeaba(nadhani ulitaka sema madini)...''..ninaposema nchi yetu masikini namanisha ni kweli ni masikini kwa kulinganisha na dunia ilivyo na hili sio swal la mjaddala kama hautaki siwezi kukusaidia maana umasikini haupimwi kwa natural resources tuu kama unavyofikiri.

Nije kwenye hoja yangu ya msingi kimsingi swala la serikali tatu kama nilivyosema halina mantiki kwa nchi yetu changa kwa maana kuwa nchi yetu in terms of level of development (physical, technological infrastructure&human resources bado ni za kimasikini hata statistics zinaonesha hvyo.

Nikuulize swali dogo wewe unayefikiria bila kukarilishwa niambie hizo serikali tatu unazoona ndio suluhu kweney nchi yetu uendeshaje wake nani anahudumia?...je mzigo huo wa uendeshaji wa serikali tatu unafikiri utabebwa na mafisadi unaowasemaa?....
 
JF-MBUNGE

JF-Expert Member
May 1, 2012
421
0
Mantiki inatokana na mktadha wa sasa mkuu.
Wao hawataki 1, sie hatutaki 2.
Kina Warioba hawaruhusiwi kuvunja muungano (may be could be best option).
The only option available ni serikali 3.

Yes mantiki kwa mazingira hayo inaeleweka lkn mie nimeenda mbali nimesema sioni mantiki ya serikali tatu-mzigo huu wa serikali tatu atabebeshwa nani?...ni mwananchi ..ndo maana nikasema kwangu mie serikali moja yatosha iwe kila upande na ya kwake au kwa muungano lkn serikali moja.

NB:kuongeza ukubwa wa serikali sio kkutibu matatizo ya mwananchi...mfano mzuri fanya tafiti kdg toka wizara zimeongezwa na serikali yetu kukua katika nyanja tafauti ni lipi kubwa ambalo unaweza sema tujajivunia kutokana na kukua kwa serikali.
 
JF-MBUNGE

JF-Expert Member
May 1, 2012
421
0
Inawezekana huoni mantiki ya 3 ila watz wakiamua huna jinsi. Kuacha kufanya ya msingi kwa visingizio vya GHARAMA wala haikubaliki.

Huu mwaka mtahama nchi, 3 hazikwepeki!

Subiri hizo serikali tatu kama utaona ndio suluhu ya matatizo unayopigia kelel kila siku zaidi utaona unalipa kodi zaidi na usilalame kwani hizo serikali zitajiendesha kwa bila kukutegemea wewe..poa kama hauogopi gharama sawa...na pia usishahau ukadhani serikali tatu ndio hakutakua kuna wajanja ..ah ahaahh tena watakua katika mafungu matatu
 
Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Top Bottom