Msaada: Nawezaje kupata bible ya kiswahili softcopy

Kama unatumia samsung ingia Google market hapo utaipata free
(Play store )
 
Android phone kama walivyosema wengine
nenda Play store halafu search pale andika
Swahili Bible free download unapata ni nzuri.
 
Wadau kwa anaye fahamu anijuze link ambayo naweza kupata bible ya kiswahili. nawsilisha
Chukua kitu HAPA mkuu usipate shida tena kinatumika kwenye computer au simu yoyote yenye uwezo wa kufungua html files NB. Hakuna haja ya installation ni standalone file. Pia hii kitu inafunguka vizuri kwenye mozila na opera.
 
mimi ninatafuta yenye vile vitabu vinne vya ziada ambavyo havipo kwenye biblia nyingine
 
wandugu nashukuru kwa kuniwezesha kupata hiyo bible ila ilivyopangiliwa inatakiwa kukariri kitabu kipi kipo namba gani,
anyway nimehitaji softcopy bible kwa sababu nauwezo mzuri sana wa kusoma softcopy, kwenye printout huwa nasinzia upesi sana. mbarikiwe
 
Kuna software iko inapikwa H-Kitchen na itakuwa released beta miezi ya mwishoni mwa mwaka huu.
Kwa sasa tumeweka nguvu katika Studio. Nitaweka few shots baadaye ina Biblia ya kiswahili searchable na mengine mengi tu!
 
Neno.png

One shot of app!
 
Chukua kitu HAPA mkuu usipate shida tena kinatumika kwenye computer au simu yoyote yenye uwezo wa kufungua html files NB. Hakuna haja ya installation ni standalone file. Pia hii kitu inafunguka vizuri kwenye mozila na opera.
Daaah,wee mkali yaani haraka kupita maelezo imefunguka!!
 
Tumia hiyo hutasinzia. Kumbuka maneno ya Yesu aliyomwambia Petro kwamba, utakapoongoka waimarishe ndugu zako. Luka 22:31-32
 
cheki na kanumba atakutumia
Mkuu umenijibu kwa dharau na ukorofi hadi umeniharibia siku. Kama ulikuwa hauna au hauijui hiyo biblia si ungekaa kimya?Si vyema kila jambo kulifanyia utani. mimi nilimaanisha biblia yenye vitabu vya DEOTEROKANONI ambavyo vipo kwenye biblia ya wakatoliki na wanaamini makanisa mengine waliviondoa kwenye biblia.vitabu hivyo ni:
1.Tobiti
2.Yudith
3.Kitabu cha Wamakabayo 1
4.Kitabu cha wamakabayo II
5.Hekima
6.Yoshua bin sira
7.Baruk
 
Back
Top Bottom