Msaada: Nawezaje kujimilikisha mali yangu kabla ya kuoa?

Adolph Jr

JF-Expert Member
Nov 5, 2016
5,518
8,538
Ni miaka mitatu tangu nikutane na mchumba (single mother). Ninaishi naye kinyumba kwa muda wote huo bila kwenda kwao kujitambulisha, ila nafsi inanisuta, nataka kwenda kujisalimisha mwakani.

Shida ni kuwa kwa muda wote huo sijaridhika na mienendo ya huyu bidada kwani licha ya kuwa msaada mkubwa kwangu kunipikia na kusafisha nyumba, ananitisha na kupenda sana kwenda kwao bila limit, tena kwa kujiamulia na ukimuuliza "vipi mbona bila kuaga?" tunakosana naye.

2. Nilimfungulia biashara ya duka ikamshinda.

3. Kuna wakati akiondoka hadi nimfuate kwao zaidi ya mara 5.

Hiyo nimeona ni ishara ya hatari kwangu nataka nijilinde au kujihami mapema nisije kuwa naenda kwao kulipia milipuko baada ya wiki adai tugawane vitu.

Kiukweli alinikuta na godoro tu nalala juu ya mkeka hadi Sasa tunamiliki nyumba. Licha ya kuwa ni mama wa nyumbani ila ni msaada sana kwangu kwa masuala ya nyumbani.

Shida yangu ni je nawezaje kujimilikisha nyumba hiyo na vitu vyote kabla ya kulipia posa kwao?

Naomba kuwasilisha.
 
Kisheria huyo ni mkeo tayari na umesema alikukuta na godoro hivyo mali yote mliyochuma pamoja mnagawana.

By the way umesema hujawahi kwenda kwao lakini akiondoka unamfuata kwao, amazing.
 
Kwanini asiende kwao sasa wakat haujamuoa jaman muache apumue kumbe mengine unajitakia
 
Kamilisha kwanza kila hatua ya kumuita mkeo ndio uanze kukasirika juu ya hio tabia. Kwa sasa hauna hio haki.
 
Kiukweli alinikuta na godoro tu nalala juu ya mkeka hadi Sasa tunamiliki nyumba.

ushasema kakukuta unalala juu ya godoro na mkeka,saivi unadai eti uambiwe jinsi ya kujimilikisha mali zako,mali zako zipi? mali zako ni godoro na mkeka tu

vingine vyote ni vyenu vyote,ukitaka msaada wambie mods wabadilishe title uzi andika

"msaada wa kumdhulumu mke wangu mali tulizotafuta wote"
 
yani majibu yako tu me hoi
 
Punguza sauti mkuu
Kama hivi
tapatalk_1569926034616.jpeg
 
Ni miaka mitatu tangu nikutane na mchumba (single mother). Ninaishi naye kinyumba kwa muda wote huo bila kwenda kwao kujitambulisha, ila nafsi inanisuta, nataka kwenda kujisalimisha mwakani.

Shida ni kuwa kwa muda wote huo sijaridhika na mienendo ya huyu bidada kwani licha ya kuwa msaada mkubwa kwangu kunipikia na kusafisha nyumba, ananitisha na kupenda sana kwenda kwao bila limit, tena kwa kujiamulia na ukimuuliza "vipi mbona bila kuaga?" tunakosana naye.

2. Nilimfungulia biashara ya duka ikamshinda.

3. Kuna wakati akiondoka hadi nimfuate kwao zaidi ya mara 5.

Hiyo nimeona ni ishara ya hatari kwangu nataka nijilinde au kujihami mapema nisije kuwa naenda kwao kulipia milipuko baada ya wiki adai tugawane vitu.

Kiukweli alinikuta na godoro tu nalala juu ya mkeka hadi Sasa tunamiliki nyumba. Licha ya kuwa ni mama wa nyumbani ila ni msaada sana kwangu kwa masuala ya nyumbani.

Shida yangu ni je nawezaje kujimilikisha nyumba hiyo na vitu vyote kabla ya kulipia posa kwao?

Naomba kuwasilisha.

Hii inaitwa Prenuptial agreement....japo sidhani kama sheria zetu zinaruhusu
 
Nilivutiwa na title. Muktadha ukawa tofauti na matarajio yangu.

Labda niulize tu: kisheria mtu unawezaje kujimilikisha mali ulizochuma mwenyewe kabla hujaingia kwenye mahusiano/ndoa na mtu?

Mfano leo hii mimi nina mali kadhaa na nipo single. Nikiamua kuwa na mtu, mali hizi mgawanyo wake utakuwaje endapo tukashindwa kuendelea kuwa pamoja?

Siku hizi tunaviziana sana. Kuna wajasiriandoa wanaojitegesha kwa mtu ili kunufaika na mali.

Huu mtego unakwepeka?
 
ushasema kakukuta unalala juu ya godoro na mkeka,saivi unadai eti uambiwe jinsi ya kujimilikisha mali zako,mali zako zipi? mali zako ni godoro na mkeka tu

vingine vyote ni vyenu vyote,ukitaka msaada wambie mods wabadilishe title uzi andika

"msaada wa kumdhulumu mke wangu mali tulizotafuta wote"

"msaada wa kumdhulumu mke wangu mali tulizotafuta wote"
 
Wanasheria hapa mnapotosha!
Kisheria huyo ni mkeo tayari na umesema alikukuta na godoro hivyo mali yote mliyochuma pamoja mnagawana.

By the way umesema hujawahi kwenda kwao lakini akiondoka unamfuata kwao, amazing.
 
Nilivutiwa na title. Muktadha ukawa tofauti na matarajio yangu.

Labda niulize tu: kisheria mtu unawezaje kujimilikisha mali ulizochuma mwenyewe kabla hujaingia kwenye mahusiano/ndoa na mtu?

Mfano leo hii mimi nina mali kadhaa na nipo single. Nikiamua kuwa na mtu, mali hizi mgawanyo wake utakuwaje endapo tukashindwa kuendelea kuwa pamoja?

Siku hizi tunaviziana sana. Kuna wajasiriandoa wanaojitegesha kwa mtu ili kunufaika na mali.

Huu mtego unakwepeka?
Hata mimi nilitamani kujua kama wewe,
 
0 Reactions
Reply
Back
Top Bottom