Msaada: Naweza kupata wapi vifaa vya mazoezi kwa mtu aliyekuwa amepalarise kwa DSM

Chukwu emeka

JF-Expert Member
Jan 12, 2018
23,410
36,559
Habari Jf Doctor,

Nina Baba yangu wa hiyari,alipata stroke ya upande wa kulia kwa bahati nzuri alitibiwa pale Moi na kurudisha fahamu vizuri kabisa na hatimaye kuruhusiwa kutoka hospital.

Alikuwa akifanya mazoezi kwa siku 3 per week hapo njia panda ya kwa mzee wa Upako kuna kidispensary cha Wakorea,alifanya kwa muda kama 3weeks,hali yake imeimarika na amesafiri kurudi nyumbani changamoto mkoa na eneo alipo hakuna vifaa vya mazoezi kwenye hospital ya karibu.

Ombi,kama kuna mtu anavijua vifaa ambavyo anaweza kuvitumia akiwa nyumbani kama exercise bike na vingine,naomba anisaidie package ambayo itaweza kumsaidia na pia hata ushauri wa kitaalamu wa nini afanye au diet.

Kiufupi anaweza kutembea kwa kidogo kwa kushika ukuta au gongo na anakula vizuri na story kama kawaida na imebaki tu kutembea hana tatizo lingine.

Natanguliza shukrani.
 
Hellow.
Nakushauri umrudishe Dar aendelee na Physiotherapy sababu vifaa ni very expensive kuliko yeye kuendelea kuhudhuria physiotherapy.
Ununue hiyo Bike
Ununue Quadriceps triangle ya mazoezi ya mguu
Ununue Shouldre triangle ya mazoezi ya mkono
Labda kama umepata challenge ya Kulipia session.

Gharama ilikua shilling ngapi?
 
Kwa miaka ya sasa,tiba ya mazoezi ya viungo( Physiotherapy) ipo karibu hosptali zote za mikoa na chache za wilaya.Ingepaswa ujaribu kuulizia mkoa alipo mzee kwa sasa kama huduma ipo kwenye hosptali ya mkoa ili mzee aendelee na tiba ya mazoezi chini ya watalaam na unagalizi zaidi.Vifaa kuwa navyo binafsi bila mtaalam hapo utatengeneza tatizo zaidi( ulemavu wa viungo kwa mzee) na pia hautaweza kufanya tathmini ya hiyo tiba.
 
Back
Top Bottom