Tatizo la kuwahi kufika kileleni kwa wanaume: Fahamu chanzo chake na namna ya kutibu tatizo hili

johnsonmgaya

JF-Expert Member
Oct 16, 2015
2,818
3,725
1587968698592.png


MASWALI YALIYOULIZWA NA BAADHI YA WADAU KUHUSU TATIZO HILI
Mambo vipi? Nina Tatizo la Kutoa shahawa mapema Sana ndani ya dakika 1 tuu then bao la pili napiga dakika 10 -- 15. Nimejaribu kutumia mazoezi ya level miezi 3..juisi ya tende miezi 2 juisi ya tikiti wiki 1 na tiba nyingi tuu nimefanya imiwepo mazoezi ya viungo hadi mbegu za maboga nimetafuna mwezi 1... Kasoro mkongo tuu sijatumia wala siutaki kabisaaa ... Sasa nishaurini nini cha kufanya ili niwe na angalau dakika 15 kabla ya kumwaga... Shukran

Sent using Jamii Forums mobile app
---
Mwenzenu Nina tatizo la kuwahi kufika kileleni hili limejitokeza baada ya kuwa single kwa muda wa miezi 10 na baada nikapata mchumba na kuingia nae golini kwa mara ya Kwanza na nikajikuta napata aibu.

Japo kipindi cha nyuma sikua hivyo nilikua nguli sana mpaka naulizwa baby Bado tu...!
Mnishauri niwe na wanawake (ninae mmoj kwa sasa) wangapi na niwe nafanya tendo mara ngapi maana nafanya kwa mwezi mara moja tu.

Msaada please.


UFAFANUZI NA USHAURI ULIOTOLEWA NA WADAU
Pre mature ejaculation ni nini?
Hii ni hali ambayo mwanaume anatoa mbegu mapema sana kipindi cha tendo la ndoa na mara nyingi huambatana na kushindwa kumridhisha mpenzi wake.

Tatizo hili limekua likiwapata wanaume wengi na kujisikia aibu mbele za wenzi wao pale wanaposhindwa kuendelea kabisa baada ya hali hii kutokea.
Kimsingi mwanaume anatakiwa achukue dakika nne mpaka nane kabla ya kutoa mbegu za kwanza lakini watafiti wanasema tatizo hili hugundukiwa mtu anapotoa mbegu ndani ya dakika moja au kabla ya dakika moja.

Tatizo hili huweza kutokea mara tu baada ya kubalehe,{primary pre mature ejaculation} mda mrefu baada ya kubalehe{secondary PE} au kutokana na aina ya mwanamke uliompata.{situational PE}

Chanzo ni nini?
Tatizo hili halina sababu za kitaalamu zilizofanyiwa utafiti zikakakubalika ila wanasayansi wanaamini sababu zifuatazo zinaweza kua chanzo kikuu cha tatizo hilo.

Kupiga punyeto au kujichua;
Mara nyingi watu wanaopiga punyeto hua wanafanya haraka kwa kujificha ili wasikutwe na mtu. tabia ile ya kulazimisha mbegu zitoke haraka huweza kuleta tatizo hili.

Kukaa muda mrefu bila kushiriki tendo la ndoa;
Kukaa muda mrefu sana bila kushiriki tendo la ndoa husababisha mkusanyiko mkubwa wa mbegu za kiume ambazo zinaleta msisimko mkubwa na ukichelewa sana kushiriki tendo la ndoa zitatoka kwenye ndoto nyevu. Kawaida mwanaume anatakiwa ashiriki tendo angalau mara nne kwa wiki.

Kuwa na wasiwasi wakati wa tendo la ndoa;
Mtu akiwa na historia ya kupata hali hii kabla, huwa hajiamini na kuwa na wasiwasi kwamba litatokea tena na matokeo yake hulipata kweli.

Madhara ya dawa zinazofanya kazi kwenye mishipa ya fahamu;
Baadhi ya dawa za usingizi, mawazo na zingine zinazofanya kazi kwenye mishipa ya fahamu huleta tatizo hili mfano amitriptyline.

Kurithi;
Baadhi ya koo au familia fulani hurithi vimelea vya kuwa na ugonjwa huu kwa vizazi mbalimbali vya familia husika.

Magonjwa ya mfumo wa uzazi wa mwanaume mfano prostatitis.

Diagnosis{ kuutambua ugonjwa]
Mwanaume yeyote ambaye anatoa mbegu chini ya dakika moja au mbili ni muhanga wa hili tatizo na anatakiwa apewe matibabu.

Matibabu
Matibabu ya ugonjwa huu yamegawanyika sehemu kuu mbili kulingana na ukali wa tatizo husika.

Non pharmacological treatment{matibabu yasiyo hitaji dawa}: Matibabu haya hupewa watu ambao wanahimili mpaka dakika tatu bila kutoa mbegu.

Pharmacological treatment{matibabu yanayohusu dawa}: Matibabu haya hupewa watu ambao hutoa mbegu ndani ya dakika moja baada ya kuanza kushiriki tendo la ndoa, watu hawa hushauriwa kutumia na mbinu zote mbili za matibabu.

Yafuatayo ni matibabu yasiyohitaji dawa.
Tumia condom:
Condom ni moja ya tiba nzuri ya tatizo hili kwani hufanya kazi kwa kupunguza hisia kali za mapenzi mtu anazozipata pale ambapo hatumii condom.

Kandamiza perineum kwa kidole:
Perineum ni eneo kati ya haja kubwa na korodani, ile sehemu ikikandamizwa na kidole huweza kuzuia kukojoa haraka wakati wa tendo la ndoa.

Punguza wasiwasi:
Hebu lifikirie tendo hili kama njia ya kujifurahisha sio njia pekee ya kutafuta kutoa mbegu, hii itakusaidia kuondoa mawazo ya kutafuta mbegu na kuchelewa kumaliza.

Fanya taratibu:
Picha za ngono zinadanganya sana watu kwamba kulala na mwanamke lazima ufanye kwa haraka haraka kama mbwa. HAPANA; ukifanya taratibu ndio njia nzuri ya kumfikisha mwenzako na wewe kuchelewa kufika kileleni.

Badilisha style:
Ile style ya zamani ya kumlalia mwanamke kwa juu{missionary position} inaleta msuguano mkubwa kwenye kichwa cha uuume hivyo itakufanya ufike haraka sana.

Tumia style ya wewe mwanaume kutangulia chini afu mwanamke juu au kulala kwa upande wote mnaangalia upande mmoja hii itakusaidia sana kuchelewa

Toa mawazo kwamba unafanya ngono:
Hebu jaribu kufikiria mambo mengine ya kikazi au masomo wakati unafanya tendo hilo, hii itakupunguzia hisia kali za mapenzi na kuchelewa kufika.

Fanya na kuacha:
Hii ni ile hali ya kuzuia msuguano pale unapoona unakaribia kutoa mbegu kwa kama sekundi 30 kisha unaanza upya. Hakikisha haufiki “point of no return”. pointi ambayo huwezi kujizuia tena kumaliza.

Kandamiza sehemu ya shingo la uume:
Hii sehemu ya shingo ya uume kwa chini ambayo ukiibana itakusaidia kuanza upya tena kihisia. Nimetumia shingo la uume kwasababu najua uume hauna mabega.

Tumia kilevi:
Unywaji wa pombe mfano bia mbili kwa siku kwa wanaume pombe hupunguza kidogo nguvu ya mishipa ya fahamu na kufanya mtu aliyekunywa kuchelewa sana kufika kileleni, [watu wanaokunywa pombe lazima mtakubaliana na hili] hivyo unaweza kunywa bia, wine au whisky nusu saa kabla ya tendo na kuondoa shida hii.

Matibabu ya kutumia dawa.
Hizi hupewa iwapo tatizo lako ni kubwa sana na hizo njia hapo juu zimeshindikana...

1. Serotonin reuptake inhibitors mfano paroxetine na clomipramine zimefanya kazi nzuri ya kuzuia kufika kileleni haraka.

2. anesthetic creams: hii hupakwa kwenye kichwa cha uume saa moja kabla ya tendo la ndoa kuzuia msisimuko na kufanya mwanaume achelewe kufika kileleni wakati wa tendo.
---
Mambo ya kufanya ili kutibu tatizo la kuwahi kufika kileleni
2. Mazoezi: Kufanya mazoezi, mwili wenye afya nzuri daima hufanya kazi vizuri, kwa hiyo kitu rahisi cha kufanya ni kujenga tabia ya kufanya mazoezi ambayo husaidia kukujengea afya njema na kukupa mzunguko mzuri wa damu. Kama una mwili wenye afya basi inaweza kukusaidia kwa namna ya kifikra ambazo huchangia kwenye suala zima la kuwahi kufika kileleni. Hii hutokana na kuongeza kujiamini na kujihusudu

2. Vuta Pumzi ya kutosha
Pumua vizuri na kikamilifu, kiungo chochote cha mwili huhitaji nguvu kamili ili kufanya kazi na ndivyo ilivyo kwa habari ya viungo vya uzazi! Unapopumua vizuri na kwa ukamilifu, kiungo hiki hupata nguvu za ziada. Jaribu kupumua kwa ufasaha ili mwili uweze kupata hisia kabla ya kuanza kufanya msuguano. Kwa mfano unapofanya mapenzi inapofikia hatua unataka kukojoa stopisha kufanya na vuta pumzi ya kutosha

3. Mazoezi ya kukojoa mkojo
Wakati unapokwenda kukojoa mkojo, fanya yafuatayo kojoa kwa sekunde mbili then stopisha mkojo, rudia tena kukojoa mjojo kwa eskunde tatu alafu stopisha tena. Fanya mara kwa mara kwa muda wa siku 14 hii pia yasemekana imesaidia baadhi ya watu LAKINI wa watu wenye tatizo la kibofu cha mkojo usijaribu hiii, may cause more problems

4. Team work
Mshirikishe mwenzako kikamilifu, kuridhika kimapenzi ni tukio ambalo wote wawili mnaridhika kikamilifu. Ili kujifunza kujizuia kufika kileleni haraka, ni vizuri kuwasiliana na mwenzi wako wa kimapenzi. Anaweza akakusaidia kushinda tatizo hili la kiaibu, kila unapohisi unataka kukojoa mapema, sema ‘ngoja’ na usitishe kwanza shughuli zote kwa muda kidogo

5. Maandalizi ya Kisaikolojia
Maandalizi kifikra ni mabaya sana, kwa mfano upo ofisini na unajua jioni unakwenda kufanya mapenzi basi jitahidi usiwaze hivyo kabisa. Hii ni mbaya saya maana hormones zinasogea karibu sana unaweza hata kuishia kwenye mapaja ya mwenzi wako. Hata kama una miadi na mwenza wako au unamwndaa mpenzi wako chukulia kama ni kitu ca kawaida sana. Au ukisha mseti mwenza wako jitahidi kusahau kama unakwenda kucheza huo mchezo siku ya hiyo.

6. Movie
Usiangalie movie za mapenzi yenye ‘style’ zenye kuchochea kufika kileleni haraka. Ungaliaji wa movie za namna hii huchochea zaidi kupandisha ashki na mukari wa kufanya mapenzi ambapo unapokutana na mwenza hata kuingiza ni shida na huishia kwenye mlango wa uzazi wa kike. Hii ni kwa sababu kuongeza ari ya kuwaza tendo la ndoa pia inaongeza msisimko kiasi kwamba ukimgusa mpenzi wako tayari umekwishaachia hata kabla ya kuingiza.

7. Thoughts Diversion

Hii techniques inamaanisha kuhamisha mawazo, kwamba unapofanya mapenzi inapofikia hatua unataka kuachia stopisha alafu hamisha mawazo yako kabisa kwenye hilo tukio. Unaweza kufikiria kitu kingine tofauti kabisa mfano unaweza kuwaza watu wanaokudai fedha na kadhalika, kuwaza kitu kingine cha kipumbavu ambacho kitakuondoa kwa muda kwenye eneo hilo just for one minute. Then unaweza kuendelea kama ile haali ya kukojoa imepotea, ni ngumu sana lakini just try

8. Style za Mapenzi
This is another killer for early ejaculation. Kuna baadhi ya style za mapenzi inapendekezwa kufanya baadha ya shoti ya kwanza ndo utumie. Kwa mfano unapoanza kufanya na style ye mbuzi kagoma au chuma mchicha hapo unatafuta balaaa aisee hasa kwa wale ambao wameadhirika na tatizo la kukojoa mapema, hii ni kwasababu style hiyo inakuwa na msisimko wa hali ya juu sana ikimabatana na constriction kwa wote wawili na haitakuchua hata dakika ushaachia wazungu weupe. Hii ni kwasababu shoti ya kwanza huwa ipo karibu sana uilinganisha na shoti ya pili, tatu na kuendelea.
Natumaini kwa leo hizi technieque nane zinaweza kukusaidia kwa namna moja au nyingine

Have wondeful controlled sex!
but remember
HIV is there and it KILLS!!!
---
Tatizo la kuwahi kufika kileleni
Kufanya unavyofanya haisaidii..

Swala la kukojoa haraka ni la ubongo..na ubongo huwa unatreiniwa..yaani kadri unavyorelax na kujizuia kukojoa haraka maybe kwa kuwaza vitu vibaya kadri muda unavyosonga utakuwa sawa..Pia goli la kwanza linatoka fasta,cha msingi make sure unamfikisha hata within that short time..

Nasema ubongo huwa unafunzwa na ndo maana mtu anaweza kusimamisha vizuri tu pale anapotaka kula zake nyeto lakini akashindwa pale anapokuwa na mdada..

Acha pupa na tafuta papuchi ya uhakika hili tatizo litaisha/litapungua kwa wewe kugegeda frequently..

Pia ingia youtube jifunze kitu kinaitwa KEGEL exercise
---

Ufafanuzi wa tatizo la kuwahi kufika kileleni
Habari zenu wakuu, natumai uko poa sana popote pale ulipo. Leo nina hamu na natumai kuzungumzia tatizo linalo sababisha kutoweka kwa furaha kunako wanaume wengi. Kukujoa mapema kabla ya kumridhisha mwenza ni tatizo linalowakumba vijana wengi na watu wazima pia, kitu ambacho kinapelekea ndoa nyingi kusambaratika. Leo nataka tuangalie ni zipi haswa sababu zinazopelekea habari hii. Tatizo la kukojoa mapema muda mwengine inakuwa sio tatizo kwasababu mara nyingi habari hii hutokana na akili.

1. HIGH SENSATION
Unajua, kuna watu wana sense kali sana katika mfumo wao wa hisia. Yaani unaweza kumkuta mtu hata hujamkaribia tayari ameshasanukia uwepo wako. Hali hii inaonesha uwezo mkubwa wa utendaji kazi wa akili yako na sio tatizo la kimwili wala katika akili. Hivyo unapokuwa na high sense pana uwezekano wa kumaliza tendo la ndoa kwa haraka zaidi kwasababu kila sexual sensation inapokuwa kubwa ndio kadri unapokuwa karibu na kukojoa. Hivyo, wenye hisia kali, wanahitajia mazoezi ya kudhibiti hisia zao. Mmi leo nitakupa zoezi moja ukalifanye halafu matokeo rudisha kwenye uzi huu. Unapotaka kufanya mapenzi safisha akili yako, ondoa kila kitu mpaka ujihisi mtupu, halafu wakati upomuingilia mwenza, fumba macho yako halafu fikiria jambo ambalo ni tofauti na sex, kama vile kazi, michezo, kumbukumbu za utotoni n.k, halafu anza kufanya kidogo then wakati unavyofanya chunguza hisia zako taratibu. Njia hii itakupa mazoezi ya kukontrol hisia zako. Ili njia iwe effective rudia kwa mara 21 katika siku tofauti. Mabadiliko ya kiakili hayatokei kwa siku moja yanahitaji muda sana.

2. HIGH EXPECTATION
Sababu ya pili ni kuwa na hamu ama matarajio makubwa ya kitendo hiko cha sex. Kwa mfano unaweza sema leo nikifanya nataka nimuoneshe game isiyo ya kitoto, au unapojiambia nitafanya mikao hii na style hile. Unajua unapofikiria hivyo unakuwa unahisi raha lkn bila ya kufahamu unatengeneza tatizo jengine ijpya. Kwasababu unapoanza kufikiria kabla ya kufanya unaifanya akili yako ithubutu kuamini kwamba upo katika tendo husika. Hivyo unavyoingia katika tendo la ndoa unajikuta ni dakika moja kama sio nusu sekunde umeshapiga bao. Kwani mchakato huo ulianza kabla katika mfumo wa akili, na akili ndio inayo control kukojoa ama kutokojoa yaani ejaculation. Hivyo ukienda chumbani ondoa kabisa mawazo ya sex, jiamini halafu ingia kwenye mziki.

3. PUU NYETO (MASTERBATION)
Huu mchezo unafanywa na vijana wengi sana pasi na kufahamu athari zake, Mchezo hu mara nyingi mtu huwa anafanya katika hali ya siri na kwa haraka tena huku akimfikiria mtu fulani na hivyo humpatia sense kwa muhusika kama anafanya kweli kitendo chenyewe. Athari ya kwanza unaiprogramu akili kuwa na mawazo ya sexual kupita kawaida, mtu anaefanya sana mchezo huu, sio ajabu akiona ziwa tu limetuna dakika hiyo hiyo ameshapiga bao. Kwasababu akili inarudi kule kule kwenye kuwaza, maana akili ishazoea kuachia mkojo wakati wa kufikiri kulikoni kutenda, Hivyo puu nyeto inamfanya muhusika siku anayomuingilia mwanamke kukojoa kabla hata ya kumgusa mwanamke au pengine sekunde 20 za kazi huwa tayari kesha kojoa, hii pu nyeto inakuwa ishajenga tabia ya kuachia mkojo kwa haraka na pia imeshajenga tabia ya imagination kuliko in reality. Hivyo solution ni kuacha michezo hii amabyo inapelekea sexual addiction.

4. KUKAA MUDA MREFU BILA YA KUFANYA MAPENZI
Unapokaa siku nyingi bila ya kufanya mapenzi ni lazima kutochukuwa muda mrefu kwenye kitendo husika, yaani utamaliza haraka na hii hutokana na mkusanyiko wa hisia nyingi ambazo hupelekea high sensation kwa hiyo kama ukiwa una muda mrefu haujafanya mapenzi, jaribu kufanya angalau mara 3 kwa week unaweza ukarudi katika hali yako ya kawaida.

5. MIKANGANYIKO YA MAWAZO AMA STRESS
Na hii ni sababu nyegine inayosababisha kukojoa kwa haraka, kwasababu unapokuwa na stress akili inakuwa haipo sawa, unafanya mambo kwa kurupuka na kwa haraka, hivyo sio ajabu kujikuta unawahi kumaliza papper test mapema.

6. MACHOFU
Machofu pia ni sababu ya tatizo hili kwasababu mwili na akili vinakuwa havifanyi kazi inavyotakiwa hivyo ni bora kupumzika kwanza halafu ndio uanze shughuli ukiwa umejipanga vya kutosha.

7. MAUMIVU YA MGONGO NA NYONGA
Kama unasumbuliwa na mgongo au nyonga basi kumaliza haraka kwenye mapenzi kusikushangaze, Kwasababu mgongo unapelekea uchovu na ndiko huo mkojo unakotokea, hivyo kukiwa huko hakuko sawa basi tatizo linaweza kuwepo, Unajua kiungo cha mwanadamu kikichoka na ukilazimisha kifanye kazi basi kitafanya kazi lkn akili italazimisha utendaji wake ufanyike kwa haraka ili kiungo hiko kipate mapunziko. Hivyo jaribu sana kulala chali kwa masaa kadhaa kabla hujafanya mambo yetu.


MATIBABU
Kama inakuchukua dakika moja mpaka kukojoa basi unatakiwa kutumia dawa zinazopungua hisia za mgusano ili kukufanya udumu kwa mda mrefu katika kitendo husika, Usitumie dawa mara zote. Siku nyengine fanya bila ya dawa uone kama kutakuwa na improvement. Jaribu kufanya meditation kila asubuhi ili kuondoa stress au mikanyiko sugu ya mawazo.
Pia unaweza kutumia condom kwasababu inapunguza hisia za mgusano.

Kama inakuchukua zaidi ya dakika moja mpaka kukojoa basi fanya sana mazoezi ili kuondosha stress na pia pendelea kufanya kegel exercise. Pia unatakiwa kufanya mazeoezi ya akili kama vile meditation. Lkn pia jaribu kujifunza kuzuia kukojoa kwenye kitendo husika. Kwa mfano unapohisi unataka kukojoa jaribu kusimama kwa sekunde chache au kubadilisha mikao mara kwa mara. Na pia ondoa fikra za sex wakati wa tendo husika, maana kuna watu wengine wakati wapo juu ya kifua cha mtu fulani wanamfikiria mtu mwengine hapo hapo. Usikate tamaa, kumbuka ulikuwa hata kuendesha baiskel haujui lkn kwa mafunzo taratibu ukajikuta unaelewa, hivyo najua itakuwa ngumu kuzi control hisia zako kwa siku za mwanzo lkn kadri unavyoendelea uatona matokeo mazuri


PIA UNASHAURIWA KUSOMA MADA HII
= > Shuhuda za namna watu walivyopona tatizo la upungufu wa nguvu za kiume

= > Tatizo la upungufu wa nguvu za kiume: Chanzo cha tatizo na ushauri wa jinsi ya kukabiliana na tatizo hilo

= > Je, ni lipi suluhisho la mwanaume kufika kileleni mapema?
 
dawa nzuri ni kutumia hiyohiyo punyeto. unapopiga punyeto na kukaribia kukojoa minya kichwa hadi ukihisi ukiachia huwezi kumwaga. rudia tena na mwaga wakati unaoona unafaa.
Samahan kiongoz HV punyeto aiwez kukusababshia matatz kama kukosa kabsa nguvu za kiume?
 
Yes zinatambulika na zinapatikana pharmacy kubwa kubwa
najua hizi dawa ni za depression/sonona na other mood disorders na moja ya side effects zao ni kushusha libido/nyege. nauliza kama zimepitishwa na wizara au FDA kutumika kwenye prematture ejaculation?
 
No kila dawa ukiizidisha inakuwa sumu njia nzuri in kufata maelekezo ya madaktari/mafamasia kuhusu miti shamba kama jina lako wengi tunaziogopa hazina maelezo wala udhibiti wa mda pia hazina guarantee doses.
Dawa zetu ni nzuri sana ila tunatakiwa tuziboreshe
Dawa zangu ninazo tibia zina uhakika wa kutibu maradhi karibu yot unayo yajuwa na hazina madhara kwa afya yako. Tangu nianze kutibia miaka 30 iliyopita hakuna hata mtu mmoja aliye lalamika kuwa dawa zangu zimemdhuru nina shukuru Kwa Mungu Dawa zangu zinasaidia sana.

FOOD AND NATURAL REMEDIES THAT WORK BETTER THAN THE MOST PRESCRIBED DRUGS IN THE WORLD.jpg
 
Dawa zangu ninazo tibia zina uhakika wa kutibu maradhi karibu yot unayo yajuwa na hazina madhara kwa afya yako. Tangu nianze kutibia miaka 30 iliyopita hakuna hata mtu mmoja aliye lalamika kuwa dawa zangu zimemdhuru nina shukuru Kwa Mungu Dawa zangu zinasaidia sana.

View attachment 438149
Ok asante kwa taarifa wahusika watakupm kupata huduma
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom