Msaada,nataka kulishtaki bunge lililopita

kirengased

JF-Expert Member
Jan 10, 2016
6,260
6,992
Kwakuwa haki hupatikana mahakamani,mimi nimetafakari sana juu ya kutotendewa haki na watu niliowaamini.
Wabunge wakiwamo mawaziri wote walituaminisha na kula kiapo kulinda mali ya umma lakini tumeona mali zetu nyingi zikiishia mikononi mwa watu wachache.
Bunge limeahidi kuisimamia na kuikosoa serikali lakini halikufanya hivyo matokeo yake tumekosa huduma muhimu Kama afya,elimu bora,maji,umeme kwa kisingizio cha mapato madogo.
Tumeingia hasara na kupoteza matrilioni ya pesa kwa uzembe wa bunge kushindwa kufanya kazi yao ya kuisimamia serikali.
Tumewalipa pesa nyingi,wameunda makamati mengi,wanakula maposho na kwenda nje(ulaya) eti kujifunza alafu leo tunagundua tumeibiwa kila mahali.
Mh. Z.K ntamtanguliza mbele kwenye hii kesi maana alikua mwenyekiti Wa kamati ya mahesabu ya mashirika ya umma.
Waheshimiwa mmetuponza kwa imani yetu kwenu sasa ngoja tukutane mahakamani. Embu Tanganyika Law Society nipokeeni kesho ofisini kwenu but Lissu asiwepo.
Kwanza ninyi TLS mlitakiwa kufanya hii kazi, mnataka kuwa Tanganyika LOW society Sasa.
 
Back
Top Bottom