Msaada: nataka kulikomboa na kulirudisha jimbo la Ismani mikononi mwa wananchi

Kajole

JF-Expert Member
Apr 12, 2011
1,667
1,642
Habari waungwana?, jamani mimi nina nia ya kugombea ubunge jimbo la Ismani ili kuleta ukombozi kwa wanajimbo wenzangu. Kiufupi mimi ni mzaliwa na mkazi wa Pawaga,nkiumri nina miaka 29 na elimu ya masters niliyohitimu mwaka 2011. Ni mfuasi na mwanachama wa CHADEMA (mwenye kadi ya chama) toka mwaka 2005.

Nahitaji kugombea ubunge mwaka 2015 hivyo naomba wajuzi wanijuze jinsi na wapi nianze maandalizi yangu kujunuisha gharama na vitu muhimu ambavyo vitanisaidia mimi kushinda jimboni. Kati ya tarafa tatu za jimbo, mbili nina ushawishi kwa vijana na wazee na ninafahamika vya kutosha.

Nakaribisha michango na mawazo yenu
 
Kajole inapendeza na hongera saana kwa maamuzi yako.

Hata hivyo ni kitu gani unaweza eleza hapa jamvini kutushawishi kuwa upo tofauti na wa sasa? Umehitimu masters 2011, kama hutajali unaweza sema kazi yako ya sasa, ulikuwa graduate mwaka gani na toka hapo ama kabla ya hapo hadi sasa unajishughulisha na nini?

Hapa itapendeza utoe picha kamili na walau kutoa profile in brief juu yako ili walau kutujengea Imani kuwa kweli wafaa kwa hiyo nafasi. Ushawishi wa watu hautoshi.. Hata Nape alikuwa na ushawishi mkubwa kwa watu na sasa hivi analaumiwa kwa mengi..
 
Kila la kheri ktk UKOMBOZI,Mi ningekushauri ungeenda pale Makao makuu Kinondoni,ungepata msaada wa uhakika zaidi.
 
Ashadii,asante sana mi na mbunge wa sasa tuna tofauti kubwa sana:tukianza na elim yake tu,ameungaunga hvyo hana upeo wa kujua kipi kipewe kipaumbele kabla ya kipi?

Wana ismani wamesahaulika kabisa na huduma zote muhim hawapati ipasavyo pamoja na rasilimali nyingi zilizopo jimboni mfano maji,barabara,matibabu nk.

Huyu mbunge wetu ukimuona jimbon basi kuna kiongozi wa kitaifa amefika ndo atakuja na hataki wananchi wampe kero zake, wakithubutu atawakashfu na kuwatukana kama watoto.

Kuhusu kaz baada ya kugraduate 2008 nlifanya kaz kama muhasibu ktk bank fulan hapa nchini na sasa najishughulisha na kilimo hapa kijijini kwangu.
 
jamaaa atakuwa ameunganisha buku, hana ajira ndio anataka kufanya ujasiriasiasa, tutakuwa wengi sana 2015, umewahi sana kujitangaza wenzako bado tupo underground, tunazichanga kimyakimya
 
Karibu sana kamanda!mahali pa kujiimalisha ni Tarafa ya Isiman...pale kuna katibu Tarafa ni mjomba wake Lukuvi anaitwa Makendi..huyu anamsaidia sana kumuimarisha, kule Idodi jamaa hana nguvu sana...

ngome ya Chadema Isiman ipo sehemu fulan waita sijui Mgoli kama sikosei au Magoli...ktk kuimalisha chama pale tmepita tulikuta vijana wameamka sana, wamejenga ofisi yenye ukubwa unaolngana na Chadema makao makuu...

kiukweli Jimbo la Isman ni masikin na hawana mtu wa kuwasemea!Ebu tupe kwanza profile yako tujue tunakusaidiaje
 
Wewe ni kama ushapita tu, Lukuvi hakuna alilowafanyia wana Ismani zaidi ya kutetea ufisadi kwa kivuli cha Unadhimu feki.

Chukua jimbo Kijana
 
DSM sio kwamba nimekosa ajira hapana ningetaka ningerudi pale nlipokuwa nafanya mwanzo,nimeamua kubaki kijjin kufanya kaz zangu binafsi ili nipate muda wa kujua vzur matatizo ya wananchi na kufahamiana pia. Ngariba kuna nimejieleza hapo juu,pia nakushukuru kwa mchango wakn.
 
Huna jipya la kufanya Isimani? Kwani kipimo cha uelewa ni elimu?
DSM sio kwamba nimekosa ajira hapana ningetaka ningerudi pale nlipokuwa nafanya mwanzo,nimeamua kubaki kijjin kufanya kaz zangu binafsi ili nipate muda wa kujua vzur matatizo ya wananchi na kufahamiana pia. Ngariba kuna nimejieleza hapo juu,pia nakushukuru kwa mchango wakn.
 
Mawazo yako ni mazuri sana ninakushauri pesa sii kitu muhimu sana katika siasa kilichopo ni wewe kutumia muda wako katika kuujenga mtandao wa chama, saidia kuwajengea viongozi mbalimbali uwezo wa kiuongozi na hii ifanye kwa viongozi wa matawi,

msingi pia waandae ili waweze kuwa wagombea wa nafasi za vitongoji na vijiji 2014 pia waandae wagombea wa udiwani kwa kata zako zote, ni vizuri ukajua una vitongoji vingai kwa jimbo zima, ufaahamu vituo vyote vya kupiga kura na kama utaweza chukua daftari la wapiga kura anza kufanya due diligence ya wapiga kura kwa mawasiliano zaidi nitafute kwa email ya richmahoo@yahoo.com, nitakushauri zaidi pia fanya kazi ya chama ndani ya chama na kazi ya chama kwenye jamii utafanikiwa. anza maandalizi hayo sasa.
 
kajole, usimbeze lukuvi, na ninapenda nikubutushie kuwa elimu yako si kigezo cha kuchaguliwa kuwa mbunge. it takes more than elimu, to be elected an MP.

ndo maana kuna watu kama jah people -
darasa la 7 tu - lakini kawa mbunge. u need to dig deeper, kajole!

elimu na uelewa ni vitu viwili tofauti. lukuvi ni very smart na ni mwelewa.
 
Richome,ntakutafuta mkuu na asante sana kwa mawazo yako. Ludewa nadhan hujanielewa vizur hvyo soma post yangu vzur ndo useme kitu!.
 
Last edited by a moderator:
kajole, usimbeze lukuvi, na ninapenda nikubutushie kuwa elimu yako si kigezo cha kuchaguliwa kuwa mbunge. it takes more than elimu, to be elected an MP.

ndo maana kuna watu kama jah people -
darasa la 7 tu - lakini kawa mbunge. u need to dig deeper, kajole!

elimu na uelewa ni vitu viwili tofauti. lukuvi ni very smart na ni mwelewa.
Lukuvi ni smart kwa lipi? Kafanya lipi la maana jimboni kwake?
 
Nipe break kidogo nitakuja hapa ku-share experience na wewe kwani hata mimi nitagombea ubunge Iramba mashariki 2015.
 
Anza sasa kuonesha values ambazo utawaletea watu wa isimani, mbona kama bado hauko contented kushindana manake huko si ndio Lukuvi kaweka kambi na juzi kati Tractor kumi za kihindi ametoa kwa vikundi vya wakulima sasa kuwa na Masters na Chadema hakutoshi kupata ridhaa ya wananchi.

Kumbuka kuwauliza wapiga kura kwanza nini wanahitaji na mtu gani wanadhani atafaa kuwawakilisha bungeni na jipime kama unazo hizo quality, sisi tuwe wa mwisho.
 
Katika eneo hilo kuna mdau wangu na mshiriki mzuri sana hapa Jf na muda mrefu anaimarisha Mtandao maeneo mbalimbali kama mtaweza muungane kwa pamoja na mfanye makubaliano miongoni mwenu kwa sasa katika kutoa elimu ya uraia kwa sasa na muda ukifika mtajichuja wenyewe nani asimame,ukitaka ntaku PM hata namba zake,labda hili walionaje?
 
Usitutangazie sisi humu jf kwani naamini hamna wapiga kura wa ismani, nenda field huko vijijini ukafanye kazi.
 
Wewe mzaliwa wa Pawaga sehemu gani Itunundu Kimande Ndolela au ...? kuanzia hapo tuongee

Back
Top Bottom