Msaada nataka kujua matatizo au madhara yakutokula nyama

Nfumu

JF-Expert Member
Nov 13, 2016
610
698
kama kichwa cha thread kinavyojieleza hapo juu nahitaji kujua ni matatizo au madhara gani ambayo mtu anaweza akapata au akaja akapa endapo hatakuwa anakula nyama ya kuku ,mbuzi au nyama yoyote ile.
 
usipokula nyama unakosa protini, madhara yake unakosa nguvu unakuwa legelege
Protein unayopata kwenye nyama inaweza kuwa compensated kwa ulaji wa nuts kama karanga, korosho, almond etc, pia kama umeamua kutokula nyama ongeza sana ulaji wa mboga za majani hasa zile za kijani kama broccoli na spinach pia ulaji wa matunda yanye vitamin C kama machungwa, nanasi, kiwi ect.

In additional vyakula vya jamii ya maharage vina protein pia, kunde, choroko, maharage,
 
Protein unayopata kwenye nyama inaweza kuwa compensated kwa ulaji wa nuts kama karanga, korosho, almond etc, pia kama umeamua kutokula nyama ongeza sana ulaji wa mboga za majani hasa zile za kijani kama broccoli na spinach pia ulaji wa matunda yanye vitamin C kama machungwa, nanasi, kiwi ect.
kwahiyo hakuna madhara yoyote endapo mtu ataacha kula nyama
kama ataamua kuacha kula nyama ni vizuri zaidi. Mtu mwenye akili timamu hawezi kula nyama
ungejaribu kufafanua mkuu kwa faida ya wote ili tukuelewe vizuri kuliko kuandika kifupi.
 
kwahiyo hakuna madhara yoyote endapo mtu ataacha kula nyama
ungejaribu kufafanua mkuu kwa faida ya wote ili tukuelewe vizuri kuliko kuandika kifupi.
Mkuu hakuna madhara kama mwili utaendelea kupata protein na iron.
 
Ni somo pana kidogo ila kiujumla nyama sio nzuri kwa matumizi ya binadamu kuanzia kiafya sio nzuri, pia invibration mbaya kwa binadamu na pia sio busara kula nyama. Vipo vyakula mbadala wa nyama kama Sky Eclat alivyokwisha eleza hivyo kama unalengo la kuacha kutumia nyama basi umechangua njia sahihi sisi. kinachotugharimu ni ladha tuu protein hata kwenye mboga zingine inapatikana pia
 
Mimi hua napata shida sana kwa nyie mnaofundisha faida za kutokula nyama. Ati unasema SIO BUSARA kula nyama ARE YOU SERIOUS?? halafu unakaa kimya why dont you explain?

Mimi kwa mujibu wa Biblia nyama walianza kula kizazi cha Nuhu wale waliopona gharika ukisoma kitabu cha Mwanzo 6 nadhani kama sio 9 yaani habari baada ya gharika Mungu akifanya nao agano la rainbow ndipo alipowaruhusu wanadamu kula wanyama. Since then nyama imeliwa hadi leo hii. Je sio busara inatoka wapi??

Pia hata kama ni sayansi mbona hamuongelei mkizingatia jamii zanwafugaji ambao wamekua wakila nyama maisha yao yote? Mfano hapa kwetu tuna wamaasai, wamang'ati na wakurya hawa jamaa ni wafugaji na wanakula nyama si mchezo. Sasa mmewahi kufanya utafiti mkajua ni namna gani jamii hizi zimeathirika kwa kula nyama??

Najaribu kutoa changamoto ili mfanye study vzr muwe na ujasiri zaidi mnapotoa mada kama hizi.

Nakubali kusahihishwa
 
kama kichwa cha thread kinavyojieleza hapo juu nahitaji kujua ni matatizo au madhara gani ambayo mtu anaweza akapata au akaja akapa endapo hatakuwa anakula nyama ya kuku ,mbuzi au nyama yoyote ile.

ZIJUE HASARA NA FAIDA ZA KULA NYAMA




Kuna mjadala wa muda mrefu kuhusu suala la nyama nyekundu, ambapo makundi mawili tofauti yamekuwa yakitoleana hoja kuhusu faida na madhara ya kula nyama, hasa ile nyama iliyowekwa katika kundi la ‘nyama nyekundu’ (red meat).

Wakati wakereketwa wa masuala ya afya wanasema kuwa nyama nyekundu huchangia hatari ya mtu kupata ugonjwa wa moyo na saratani ya tumbo, wadau wa nyama wanadai kuwa hakuna uhusiano wa moja kwa moja kati ya saratani, ugonjwa wa moyo na nyama nyekundu.

Wakereketwa wa masuala ya afya wanaeleza kuwa ukweli uko wazi kwamba nyama nyekundu inaweza kusababisha ugonjwa wa moyo kwa mtumiaji, kwani baadhi ya nyama nyekundu huwa na kiwango kikubwa mafuta (saturated fat) ambayo huongeza kolestro mwilini na mtu mwenye kiwango kikubwa cha kolestro huwa hatarini kupatwa na ugonjwa wa moyo.

Kwa upande wa saratani, watafiti wanasema kuwa bado hakujawa na ushahidi wa moja kwa moja kuwa nyama nyekundu inaweza kusababisha saratani ya tumbo. Utafiti wa hivi karibuni uliofanywa na Taasisi ya Afya ya Taifa nchini Marekani, umebaini kuwa watu wanaopenda kula kwa wingi nyama nyekundu, hufa mapema kuliko wale wanaokula kiasi kidogo cha nyama hiyo.

Wapenda nyama ambao wako kwenye hatari kubwa ya kupatwa na saratani na ugonjwa wa moyo ni wale wanaokula kuanzia kiasi cha gramu 112 za nyama (karibu robo kilo) kila siku, lakini wanaokula kiwango kidogo (nusu ya robo kilo) hawako hatarini na badala yake watapata virutubisho muhimu vinavyopatikana kwenye nyama.

Ulaji wa nyama nyekundu wenye faida kwa mwili wa binadamu ni ule unaozingatia kiasi na aina ya nyama. Nyama inayopendekezwa ni steki isiyo na chembe ya mafuta (lean meat) na itakayoliwa kwa kiasi kidogo.

Nyama inahitajika kiafya kwasababu ina madini ya chuma ambayo ni muhimu kwa wasichana na wanawake wanaotarajia kuzaa. Pia nyama ina Vitamini B12 ambayo husaidia utengenezaji wa DNA na hujenga mishipa na seli za damu. Halikadhalika kuna madini ya zinki ambayo husaidia kuimarisha ufanyaji kazi wa kinga ya mwili. Bila kusahau nyama ina protini ambayo ni muhimu kwa ujenzi wa mifupa na misuli.

JE, NGURUWE NI NYAMA NYEKUNDU?
Katika majadala huu wa nyama nyekundu, kumezuka swali pia kama nyama ya nguruwe nayo iko kwenye kundi la nyama nyekundu, kwani kimuonekano ni nyeupe. Jibu ni kwamba nyama ya nguruwe nayo ni nyekundu.

Kwa mujibu wa Wizara ya Kilimo ya Marekani, kiwango cha protini aina ya ‘myoglobin’ kilichomo kwenye misuli ya nyama yoyote ndicho kinachoonesha aina ya nyama. Nyama ya nguruwe inahesabika kuwa ni nyekundu kwa sababu kiwango chake cha ‘myoglobin’ ni kikubwa kuliko kile kilichomo kwenye nyama nyeupe za kuku na samaki.

Kwa ujumla, nyama nyekundu ni muhimu kwa afya ya binadamu, lakini itakuwa muhimu kama itatumiwa kwa kiwango na kiasi kinachotakiwa. Siku zote epuka kula nyama yenye mafuta na badala yake pendelea kula steki isiyokuwa na mafuta ili upate virutubisho vyake muhimu kwa afya yako.

Kula nyama kinyume na mwongozo huu, ni sawa na kuamua kujiweka katika hatari ya kupatwa na ugonjwa wa moyo na matatizo mengine ya kiafya, ikiwemo ugonjwa wa miguu au kansa ya tumbo. Jiepushe na hayo kwa kuzingatia masharti ya ulaji sahihi.
 
kama kichwa cha thread kinavyojieleza hapo juu nahitaji kujua ni matatizo au madhara gani ambayo mtu anaweza akapata au akaja akapa endapo hatakuwa anakula nyama ya kuku ,mbuzi au nyama yoyote ile.
Mwanangu Mashinagu una umri gani? Kula nyama mkuu usiache hata kidogo, piga nyama mwanangu! Ukikosa nyama unajinyima mengi, kubwa kabisa utakuwa kilaz.a maana bichwa litakuwa dafu la kuhifadhi maji ya nazi! Kumbuka kwenye nyama kuna mafuta muhimu kabisa yaitwayo Omega-3 and Omega-6 ambayo yana mchango mkubwa katika kuupa ubongo akili! Pia kwenye nyama (hasa inayotokana na wanyama waliolishwa nyasi) kuna kitu inaitwa CLA (conjugated linoleic acid) ambayo ni anti-carcinogenic, anti-cardiovascular na pia inaboresha kinga za mwili. Tupige nyama mkuu usisikilize kelele za watu wasiokuwa na uwezo wa kununua nyama.
 
Back
Top Bottom