Msaada nataka kuhamia Kampala

mkosa shingo

Member
Jan 26, 2021
93
125
Habari wana Jamii Foram.

Nahitaji msaada wenu niko kwenye wakati mgumu msongo wa mawazo.Mimi ni mgeni humu.Mama wa watoto wawili wasichana. Hapa napoishi nimejenga sababu inayonipelekea kuhama hapa ni kwamba nimezungukwa na family zote mbili upande wa baba na mama.

Hizi family ni shida upande wa marehemu Mama yangu wanatabia mbaya kuchukuliana wanaume bila kujali hata wanaume kuchangia wake upande wa Baba magonjwa, dhulma yaani ni mambo mengi nahofia wanangu kukua katika mazingira haya. Mikoa nilio taka kuhamia napo wamejaa naona bora nje ya nchi.

Naombeni ushauri jinsi ya kupata kazi
 
kampala starehe ni kuanzia j3 mpaka j3 japo hili halina umuhimu kwako
 
Una fani gani?

Una pesa inayokutosha kuhudumia watoto wawili kwa mda gani kama hutapata kazi?

Kuna issue za work permit?

Inconveniences ni nyingi sana nakushauri baki bongo, hama mkoa tu, mbona ipo mingi tu
 
Fani ya hotel.Nina milion mbili tu kwa sasa.lakini nilikua nataka nipangishe nyumba yangu hiyo kodi ndio nipange huko.Yaani nataka nipotee kabisa mtu asijue nipo wapi sitaki wajue nipo wapi nahisi huko mbali moyo wangu utatulia
 
Upo mkoa gani? Usikurupuke kwanza. Ungekuwa peke yako milioni mbili n nyingi ila kwa kuwa una watoto wawili hiyo hela haitoshi.
 
Yaani nimechoka kila kitu hakiendi.nashinda nimelala.hii sehem nimechoka.Nahitaji kwenda mbali ambapo watu siwajui kabisa nianze moja
 
Fani ya hotel.Nina milion mbili tu kwa sasa.lakini nilikua nataka nipangishe nyumba yangu hiyo kodi ndio nipange huko.Yaani nataka nipotee kabisa mtu asijue nipo wapi sitaki wajue nipo wapi nahisi huko mbali moyo wangu utatulia
Tafuta kazi Zanzibar kwa hiyo fani.. ila kwa kipindi hichi cha Covid19 risk ni kubwa sana.. halafu hiyo hela ndogo..

Nenda Zanzibar mkuu achana kuvuka border sahiv tena na family
 
Upo mkoa gani? Usikurupuke kwanza. Ungekuwa peke yako milioni mbili n nyingi ila kwa kuwa una watoto wawili hiyo hela haitoshi.
Milioni mbili labda angekuwa mwenyewe hakafu ana uhakika tayari wa ajira huko.. lasivo hii decision sio optimal
 
Fani ya hotel.Nina milion mbili tu kwa sasa.lakini nilikua nataka nipangishe nyumba yangu hiyo kodi ndio nipange huko.Yaani nataka nipotee kabisa mtu asijue nipo wapi sitaki wajue nipo wapi nahisi huko mbali moyo wangu utatulia
Njoo ifakara tulime mpunga hutojutia huku unakutana na wapogolo na wandamba tu .
 
Fani ya hotel.Nina milion mbili tu kwa sasa.lakini nilikua nataka nipangishe nyumba yangu hiyo kodi ndio nipange huko.Yaani nataka nipotee kabisa mtu asijue nipo wapi sitaki wajue nipo wapi nahisi huko mbali moyo wangu utatulia
Mkuu pole sana kwa yanayokukumba,ila nadhani unaugonjwa furani unaitwa the fear of the unknown, plus stress, tuliza akili Tanzania kubwa sana haina haja ya wewe kwenda Kampala.

Huu ugonjwa Wa the fear of the unknown uliwahi kumfanya jamaa Yangu akaacha kazi ya ualimu eti kisa kuna watu wanataka kumuua kumbe wapi

Sent from my TECNO KB7j using JamiiForums mobile app
 
Back
Top Bottom