Msaada: Nataka kufanya biashara Kariakoo (jumla), sijui pa kuanzia

Wasikukatishe tamaa hata hao wenye maduka na biashara kubwa hawakuanza hata na hiyo million..Cha msingi Anza chini komaa utafika...Kuna mtu alianza kupanga chini hana meza saiv kafika mbali sana...wafanyabiashara wakikuzoea ukiwa unaaza udogo mdogo urafiki siku utaanza kuaminiwa mizigo ya mamilioni...

Sent from my Infinix X657 using JamiiForums mobile app
Ahsante sana kwa ushauri wa kutia moyo
 
Mbona una makasiriko, nimeomba ushauri. Ni swala la kusema tu mtaji anzia kiasi flani ili biashara iende vizuri. Kuna watu wengine watanufaika humu
Unatutania milioni moja itasaidia nini!!?
hapo hujalipa rent!!??
jaribu kuwa na 50m....
ama 30m nje ya kodi ya pango
 
Mkuu wala hata TIN usiende kuchukua...
Chukua hela nenda saa 9 alfajiri karume pale kachague viatu vizuri,,, tafuta eneo vipange uuze...
Kama utakosa eneo,, nenda kwa ambao tayari wamenunua viatu,,piga picha post kwa groups na mitandaoni..mteja akikipenda ndio unaenda kununua unampelekea..

Kuna mbinu zingine nyingi tu ambazo zitakuza huo mtaji wako kutoka hio 1m uliyonayo...

Angalizo: Ukiendelea kukaa na hio hela, hutakuja kuanza na itaisha bila wewe kuelewa imeishaje......so bora ukae na Mali kuliko Cash.
 
Nina million 1
Jamaa yangu mmoja alitumia million 50 kupata fremu tu, ingawa magoli yanatofautiana.

Ila million moja na unachoplan hakuna uhalisia, anayekupa moyo anakudanganya tu huwezi kuanza biashara kariakoo kwa mtaji huo, labda biashara. Nyingine ya vyombo vya mchina.
 
Jamaa yangu mmoja alitumia million 50 kupata fremu tu, ingawa magoli yanatofautiana.

Ila million moja na unachoplan hakuna uhalisia, anayekupa moyo anakudanganya tu huwezi kuanza biashara kariakoo kwa mtaji huo, labda biashara. Nyingine ya vyombo vya mchina.
Kwa hiyo unasema bila 50-80million itakuwa story za abunuasi kufanya biashara kariakoo
 
Kwa hiyo nijipange kwa kiasi gani??
Hakuna kiasi maalum mkuu, ila k/Koo hata hiyo stoo ni Kodi kubwa kuliko frem ya mbezi. Min miezi 6 ukibahatisha. Nimeipenda Nia uliyoionyesha inaonekana ni mtu wa kuthubutu. Ongeza kidogo mtaji angalau 10m kaanze, kama una usafiri nenda na sample tafuta wateja kwanza, ukiwapata peleka. Gari iwe store yako.
 
Back
Top Bottom