Msaada: Nataka kuagiza simu nje na kutumia kwa njia ya USPS, Nifanyeje?

adriantz

New Member
Nov 1, 2016
1
20
Nataka kuagiza simu kupitia mtandao wa amazon na ninahitaji mzigo wangu niupokee kwa njia ya USPS, Tatizo sifahamu hii USPS inakuaje ila naona wengi wanasifia kua ni nzuri.

Naomba mnieleweshe. Je ili niweze kutumia hii Huduma ya USPS natakiwa kua na sanduku la posta au inakuaje?

Sina uelewa wowote juu ya hili hivyo nawaomba mnaofahamu mnieleweshe ili nijue kabla sijaagiza mzigo pia kuhusu GLOBAL MAIL nayo inakuaje?
 
Mwl.RCT

JF-Expert Member
Jul 23, 2013
8,731
2,000
Nataka kuagiza simu kupitia mtandao wa amazon na ninahitaji mzigo wangu niupokee kwa njia ya USPS, Tatizo sifahamu hii USPS inakuaje ila naona wengi wanasifia kua ni nzuri.
USPS ni kweli ni nzuli
1. simu itakuja kwa njia ya posta
2. Kuna uwezekano mkubwa kusiwe na kodi, Pia kwa USPS huwa hakuna assesment fee(TSH 60,000) na swisport fee(TSH 27,000) ambazo makampuni kama ARAMEX au FEDEX huwa nazo na kuongeza ghalama zisizo za lazima.
3. Ili mzigo wako usafirishwe kwa USPS ni vyema ukatumia EBAY badala ya amazon - Sababu amazon hatumi direct kuja africa
Je ili niweze kutumia hii Huduma ya USPS natakiwa kua na sanduku la posta au inakuaje?
Ndio ni muhimu kuwa na sanduku la posta. Maana wanatuma mzigo kwa P.O box

Iwapo hauna sanduku la posta huduma za Fedex / DHL/ aramex/ UPS zitakuwa zinakuhusu.
Sina uelewa wowote juu ya hili hivyo nawaomba mnaofahamu mnieleweshe ili nijue kabla sijaagiza mzigo pia kuhusu GLOBAL MAIL nayo inakuaje?
Global mail, ni huduma ya posta pia.

Kwa msaada zaidi tumia hii link ya hapa JF www.v.ht/buy4me
 
Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Top Bottom