Msaada: Nataka kuagiza gari toka japani trade car view

Kurunzi

JF-Expert Member
Jul 31, 2009
9,274
9,911
Wadau naomba msaada kwa wenye uzoefu kuna Gari aina ya RAUM ya mwaka 1997 nataka kuiagiza kutoka JAPAN kwa hawa jamaa wanaitwa TRADE CAR VIEW bei ya gari nimeona ni $ 785 CIF Dar es salaam with JAAI Inspection is US$2,248.

Kwa wale wenye uzoefu je bei hiyo iko sawa kweli? na je hawa jamaa wa TRADE CAR VIEW ni waaminifu? na ikiwa bei mpaka ifike hapa ni kiasi hicho, je mpaka iwe barabarani itanicost kiasi gani.

tafadhali naombeni msaada.​

06.jpg
 
ni waaminifu kupita maelezo..walilifikisha gari langu salama salimini..go for them
 
Nashukuru mkuu kwa kiasi hicho hapo je mambo ya ushuru itanicost kiasi gani?
 
Hao jamaa ni waaminifu at least 90%. Unachokiona ndo wanachokuletea.
Ila, usiikubali bei moja kwa moja kwanza. Bargain nao kwanza; waombe wakupunguzie bei. Anza nao kwa kuwakomalia nusu ya bei; then, mnasogeeeaaa, mpaka mahali flan; unawakomalia hapohapo.
Then, other procedures can follow.

Sent from my BlackBerry 9810 using JamiiForums
 
Nashukuru mkuu na vipi haya machages ya TRA kwa bei hiyo wanawza kunipiga ngapi mpaka liwe barabarani
 
Nimeagiza magari ma 3 kupitia kwa hao jamaa yote yalikuja km nilivyoyaona! hawana longolongo
 
Mimi nilitaka kuagiza gari kwao nilipouliza kwa wakala mmoja wa kuclear magari kutaka kujua ikiwa hao tradecarview ni waaminifu akaniambia nisithubutu kununua kwao kwani unachokiona online sicho wanachokuletea.

Nami nikaamini hivyo, lakini sasa nabadili mawazo kutokana uzi huu, ingawa nahitaji uhakika zaidi!
 
... haya bwana si mnataka bei ya chini' sawa tu! lakini ninawaomba msome masharti ya TradeCarView: mimi ninavyojua hiyo siyo kampuni ya kuuza magari' bali ni ubao tu wa matangazo ya kuuza magari. Wanaouza magari ni kampuni nyingine tofauti na tradecarview. kuweni makini wakubwa!!!!
 
Beforward.jp ndio mpango mzima ila magari yao yamekula millage na ni bei rahisi, Sbtjapan ndio mpango mzima wana magari mazuri sana na masafi.pia ni cheap!
NI PM Nikusaidie na Total cost za TRA.
 
Hao jamaa ni waaminifu kupita maelezo. Mwaka huu nimeagiza magari mawili Carina na Pajero na yote yamefika ya fresh kabisa. Na nina jamaa zangu wengi wanaagiza kupitia huko, magari yanafika bongo kama ulivyoyaona kwenye mtandao. Bei ni rahisi na ni waaminifu. Kwa uhakika zaidi uagize kupitia paytrade fee ambazo kwa gari yoyote ile haipungui 150usd kama gharama za huo mtandao maana hao ni mawakala wa makampuni yanayouza magari kupitia mtandao wao. Kuhusu gharama za kukufanya uliweke barabarani usipungue CIF ya gari hiyo na ikizidi au kupungua ni kidogo sana. Kila la kheri mkuu.
 
Nyie jichanganyeni tu mkutane na wa nigeria wawalize. 80% wamejaa mapopo wanasebiri wawapige. Tena kwa kukutamanisha wanaweza kukupunguzia bei hata 50%......na wanakuambia lipia haraka au kabla ya kesho
 
Unaongea kwa uzoefu wakupigwa au wa kinadharia?
 
Mimi nilitaka kuagiza gari kwao nilipouliza kwa wakala mmoja wa kuclear magari kutaka kujua ikiwa hao tradecarview ni waaminifu akaniambia nisithubutu kununua kwao kwani unachokiona online sicho wanachokuletea.

Nami nikaamini hivyo, lakini sasa nabadili mawazo kutokana uzi huu, ingawa nahitaji uhakika zaidi!

Mkuu nakuhakikishia utawafurahia mie nimeshaagiza kama mara mbili wao ni super ila unawalipa 3.9% ya CIF + $ 50 kima cha chini $150
 
... haya bwana si mnataka bei ya chini' sawa tu! lakini ninawaomba msome masharti ya TradeCarView: mimi ninavyojua hiyo siyo kampuni ya kuuza magari' bali ni ubao tu wa matangazo ya kuuza magari. Wanaouza magari ni kampuni nyingine tofauti na tradecarview. kuweni makini wakubwa!!!!

Hawana shida wewe unakubaliana na mteja kupitia web yao inabidi uwe na akaunti baada ya hapo unawatumia wao pesa wanakaa nazo mpaka wahakikishe gari imepakiwa melini ndipo wana mlipa muuzaji
 
hakikisha una tumia Pay Trade System tu mkuu ila ni waaminifu unachoona ndo unacholetewa hawana longolongo kabisa
 
Hao jamaa ni waaminifu kupita maelezo. Mwaka huu nimeagiza magari mawili Carina na Pajero na yote yamefika ya fresh kabisa. Na nina jamaa zangu wengi wanaagiza kupitia huko, magari yanafika bongo kama ulivyoyaona kwenye mtandao. Bei ni rahisi na ni waaminifu. Kwa uhakika zaidi uagize kupitia paytrade fee ambazo kwa gari yoyote ile haipungui 150usd kama gharama za huo mtandao maana hao ni mawakala wa makampuni yanayouza magari kupitia mtandao wao. Kuhusu gharama za kukufanya uliweke barabarani usipungue CIF ya gari hiyo na ikizidi au kupungua ni kidogo sana. Kila la kheri mkuu.
Je, ushuru ni kiasi gani kwa Toyota Dyna P/Up , Tani 1.5 ya mwaka 2006 ambayo CIF yake ni USD 11,000/= . TRA siwaelewi mara nasikia wanatumia depreciation, mara 80% ya CIF...hebu nisaidieni hapa????
 
Ndugu trade car view hawauzi magari ila, wanakutanisha makampuni mbali mbali yanayo uza magari, gari uliyoiona utaona iko kwenye kampuni fulan hiyo ndo utadili nayo.
Vitu vya kuangalia:
Kwanza: kuna rating za customers ambao wameshawah nunua gari katika kila kampuni ukichagua hiyo gari utaziona chini utaona ni kwa kiwango gani hao watu ni waaminifu
pili: bagain muelewane bei na kila kipengele kinacho jumuisha gharama
tatu: angalia kwenye mtandao wa TRA utaona kodi utatozwa kiasi gan ili upate estimation ya gharama
otherwise mimi recently nimenunua gari kutoka Real motors wamo humo tradecarview ilifika vizuri tu, longolongo ni chache
Kila la kheri
 
Similar Discussions

Back
Top Bottom