Msaada: Nataka kuagiza gari toka japani trade car view

Nyie jichanganyeni tu mkutane na wa nigeria wawalize. 80% wamejaa mapopo wanasebiri wawapige. Tena kwa kukutamanisha wanaweza kukupunguzia bei hata 50%......na wanakuambia lipia haraka au kabla ya kesho

Wewe ndo unajichanganya, watu tumeagiza magari kutoka huko yamefika yakiwa salama na tunaendelea kudunda nayo mtaani. Sasa sijui unasema kwa reference ipi?
 
Je, ushuru ni kiasi gani kwa Toyota Dyna P/Up , Tani 1.5 ya mwaka 2006 ambayo CIF yake ni USD 11,000/= . TRA siwaelewi mara nasikia wanatumia depreciation, mara 80% ya CIF...hebu nisaidieni hapa????

Ebu jaribu kuchek na hawa jama wa gariyangu ili kupata estimates www.gariyangu.com, au kwenye website ya TRA. Ila nilichokiona kwa gari ndogo, gharama ya kodi na malipo mengine jumla yake inakuwa karibia sawa na CIF.
 
Asante prof. nimekiona. Ila hii dumping fee (kwa non utility vehices) ina maana gani kama mtu aliyenunua gari la chini ya miaka 10 analipa zaida ya yule aliyenunua gari lenye umri wa zaidi ya miaka 10? Inavyoonekana ili ulipe ushuru kidogo gari lako liwe na miaka 10 tu.
 
Dumping fee unalipa kwa gari yenye umri wa zaidi ya miaka 10 na chini ya hapo hamna dumping fee. Ila nilichokiona kwenye magari ni kwamba jumla ya kodi zote kwa gari ya aina moja lakini matoleo ya miaka tofauti, unaweza kujikuta unalipa kodi kubwa sana kwa yenye umri mdogo kuliko iliyokaa hata zaidi ya miaka 10. Na sababu huwa wanadai inajifidia kwenye depreciation ya gari hiyo kwa customs value wanayotumia.
 
Similar Discussions

0 Reactions
Reply
Back
Top Bottom