Msaada: Nataka kuacha kazi ya kuajiriwa na nina mkopo benki niliochukua na kuweka mshahara wangu dhamana

Yaleyale

JF-Expert Member
Aug 21, 2011
1,787
2,372
Wasalaam waugwana.

Mimi ni mwajiriwa serikalini. Kama miezi 6 iliyopita nilichukua mkopo kwenye benki mojawapo hapa nchini na dhamana ilikuwa ni mshahara wangu.

Kutokana na sababu fulani fulani, nataka kuacha kazi na nifanye mambo yangu binafsi. Ninaweza kuwa nalipa benk kiasi kilekile wanachokata kwa mwezi lakini sio kwa kutegemea mshahara tena.

Je, natakiwa kufuata utaratibu gani ambao haitaonekana kuwa nataka kuruka mkopo?
 
Last edited by a moderator:
Jambo la kwanza nenda benki uliyochukua mkopo, wape taarifa kwamba unaacha kazi na kwamba utaendelea kuwalipa mkopo wao.

Lakini hapo inaweza wakakuganda hadi ukajuta, wengine wanaacha kwanza kazi ndio wanataarifu benki husika kuhusu adhma yao ya kuacha kazi.

Kikubwa uwe na shughuli ya kueleweka itakayokuingizia kipato cha kujikimu na kulipa mkopo.

Kila la kheri
 
Jambo la kwanza nenda benki uliyochukua mkopo, wape taarifa kwamba unaacha kazi na kwamba utaendelea kuwalipa mkopo wao.

Lakini hapo inaweza wakakuganda hadi ukajuta, wengine wanaacha kwanza kazi ndio wanataarifu benki husika kuhusu adhma yao ya kuacha kazi.

Kikubwa uwe na shughuli ya kueleweka itakayokuingizia kipato vha kujikimu na kulipa mkopo.

Kila la kheri
Wamgande kivipi, kwamba wamwambie asiache kazi au?
Kuacha kazi ni hiyari yake hakuna wa kumpangia.
 
Ugandaji nnaoongelea hapa, wanaweza kuanza kusumbuana na mwajiri wake wakati hajaacha kazi bado.

Kumbuka kuna suala la mafao na stahiki za mwajiriwa.
Hata wakisumbuana nae, bado haki ya kuacha kazi iko mikononi mwake. Hakuna namna wanaweza kuzuia nia yake kama kweli anataka kuacha kazi.

Maana taratibu ni zile zile. Haki zake ziko pale pale.

Kama ana nia ya kuacha kazi aache tu. Hakuna chochote kinaweza kuzuia nia yake.
 
Hivi umenielewa vizuri? Mie naongelea timing ( muda sahihi wa kutoa taarifa kwa benki inayomdai) wewe umejikita kwenye adhma na nia ya kuacha kazi.
Hakuna mahali nimesema watamzuia au wanamkataza kuacha kazi, jambo la msingi ni wakati gani muafaka kuwasiliana na mdai wake?
 
Nimekusoma mkuu. Shukrani
 
Write your reply...aisee kweli hapa duniani kila mtu anakula kwa urefu wa kamba yake! natafuta kazi mwaka wa tatu huu,bado nahangaika tu!!
 
Hivi umenielewa vizuri? Mie naongelea timing ( muda sahihi wa kutoa taarifa kwa benki inayomdai) wewe umejikita kwenye adhma na nia ya kuacha kazi.
Hakuna mahali nimesema watamzuia au wanamkataza kuacha kazi, jambo la msingi ni wakati gani muafaka kuwasiliana na mdai wake?
Hakuna wakati muafaka. Akitaka kuacha kazi anaacha muda wowote na wakati wowote. Hakuna perfect timing.

Hakuna kitakachozuia wala kuingilia mchakato wake wa kuacha kazi nje ya yeye mwenyewe. Hakuna cha timing wala nini.

Bado hujajenga hoja inayoeleweka.
 
wenzako wanatafuta kazi alafu ww unaacha kazi... ushauri wangu usiache fanya kazi huku unapiga mishe zako zingine..

kazi ya serikali ni security tosha if know what i mean

hizi semina za hawa motivational speakers zinawaponza sana watu daaaah
 
Mkuu aksante kwa ushauri wako. Kimsingi nimeshafanya maamuzi ninachouliza hapa ni safe exit bila kukwaruzana na taasisi za fedha wanaonidai.
Nimefanya kazi serikalini miaka 15 sasa hivyo naelewa ninachofanya. Unfortunately sijawahi kuhudhuria kwenye hizo semina kiongozi.
 
4 Reactions
Reply
Back
Top Bottom