Msaada: Nataka kuacha kazi ya kuajiriwa na nina mkopo benki niliochukua na kuweka mshahara wangu dhamana

Acha kazi uchwekwe, Mwana kulitafuta mwanakulipata. Usikute hujawahi kuuza hata mahindi ya kuchoma, unakurupuka kwa motivation Speaker anakudanganya kuajiriwa Ni utumwa, Kumbe katoka kusoma kitabu Cha CEO wa KFC

kilichoandikwa miaka 40 iliyopita Tena ulaya siyo hapa kusini kwa jangwa la sahara. Mkopo unakupa wenge ushajiona tajiri.
 
  • Thanks
Reactions: amu
Kama huna background ya business usikurupuke kuacha kazi nchi hii kujiajiri kuna changamoto na vikwazo vingi sana tu, usione watu wanakomaa na kuajiriwa ingia mtaani uone tena awamu hii waliojiajiri wanapata tabu sana, ukitaka kuacha kazi anza kitu chako taratibu kikiwa kikubwa ndo uache
Utaifanya vp kuw kikubwa wkt bado unafanya kazi za watu, ameshindwa kuifanya iwe kubwa kwsbb ya kukosa uhuru na mda, na kw taarifa yko kuna biashara zingine bado hazilipiwi hata kodi, kwhy biashara ndo inachangamoto, kuna biashara karibia 150 kuna mengine hailipiwi kodi, sema kila biashara watu wanataka wafanye Dar, sasa Dar TRA wapo kila sehemu
 
Nakwambia si mchezo ukijaribu hili uzibe na urasimu mwingi, na sasa hivi uchumi ulivo hali ndo mbaya kabisa kibiashara.
Biashara gani mbaya sema hauna mtaji, au umeng'ang'ania biashara moja, mbona hatujaona wafanyabiashara wote wamefunga baishara zao
 
Kujiajiri sio mchezo mkuu
Jiandae kuichukia serikali yako kama ukijiajiri
Wafanyakazi ndo wanaichukia kuliko maelezo sema tu Hali zao mbaya, wanapata ya kulipa kodi na kula na chakula chenyewe siyo chakula bora, ni bora chakula ilmradi watoto wavimbe tumbo
 
Habari za majukumu

Naombeni ushauri ndugu zangu.
nataka kuacha kazi kwa sababu zifuatazo
1.Mshahara mdogo
2.kiinua mgongo serekali ime zuia
3.Sielewani na huyu boss msukuma

Tatizo kinacho nizuia kuacha kwa sasa nina mke ila mtoto sina.

Ndugu wa mke nao wana nitegemea wapo nyumbani kwangu. Nifanyeje jamani.
Ujaja duniani kulisha watu Kama hauna uwezo, Angalia familia yko kwanza,hao wengine hawana ulazima Sana, cha msingi tumia kauli ya wachina, mtu akikuomba ugali mpe jembe, mbegu, panga na mbolea akalime, kwhy usiwape chakula
 
Piga kazi acha masihara na maisha. Kama umewekeza vya kutosha it's okay vinginevyo endelea na kazi huku ukitafuta mtaji wa kujiajiri.
Wengi hatujawaelewa hawa walioomba ushauri wa kuacha kazi sijui kwsbb hawajenga hoja, ila naamini walioajiriwa wanaelewa waajiriwa wenzao pindi wanapoamua kuacha na kwssbb tuko mchanganyiko umu hatutaelewana, mtu anasema wekeza vya kutosha na utafute mtaji, hayo yote yangewezekana sidhani Kama kuna mfanyakazi angeacha kazi au angekuja umu kuomba ushari
 
Wasalaam waugwana.

Mimi ni mwajiriwa serikalini. Kama miezi 6 iliyopita nilichukua mkopo kwenye benki mojawapo hapa nchini na dhamana ilikuwa ni mshahara wangu.

Kutokana na sababu fulani fulani, nataka kuacha kazi na nifanye mambo yangu binafsi. Ninaweza kuwa nalipa benk kiasi kilekile wanachokata kwa mwezi lakini sio kwa kutegemea mshahara tena.

Je, natakiwa kufuata utaratibu gani ambao haitaonekana kuwa nataka kuruka mkopo?
Unapokopa benki, mkopo huo wanauwekea bima.

Kuacha kwako kazi, kufa, kutoroka hakuwasababishii hasara yoyote na wala hawana 'time' na wewe.

Unapoacha kazi, mafao yako hukatwa na mwajiri ambaye ndiye mdhamini wako kuziba pengo la deni lako.

Niseme tu kwamba kuacha kwako kazi hakuhusiani na hasara inayoweza kusababishwa na deni lako benki, hivyo endelea na mchakato wako wa kuacha kazi.
 
Acha kazi uchwekwe, Mwana kulitafuta mwanakulipata. Usikute hujawahi kuuza hata mahindi ya kuchoma, unakurupuka kwa motivation Speaker anakudanganya kuajiriwa Ni utumwa, Kumbe katoka kusoma kitabu Cha CEO wa KFC

kilichoandikwa miaka 40 iliyopita Tena ulaya siyo hapa kusini kwa jangwa la sahara. Mkopo unakupa wenge ushajiona tajiri.
Kama hauna malengo hata kwenye kazi iyo ukifanya hata miaka 100 hutatoka, ila ukiamua kwenda kujitumikisha Kama ulivyotumikishwa kwenye kazi za watu unasonga mbele, Mm ndg zangu wametoka kwenye kazi watu tena serikalini, walikuw hawana biashara na mtaji waliokuw nao hata milioni kumi haikufika na wengine wameenda kulima, Leo hii wko mbali sana, Mtaani ugumu wke mtaji, lkn kwkuw mitandaoni watu tuanashauriana kulingana na jinsi tulivyoshindwa biashara au maisha kwhy uaamini hata uyo atashindwa, mtu Kama biashara yke alijifanya bingwa wa kuonga wanawake na kunyea bia alafu anakuja kuwatangazia watu mitandaoni biashara ngumu kumbe mchawi wa bishara yke ni yy.
 
wenzako wanatafuta kazi alafu ww unaacha kazi... ushauri wangu usiache fanya kazi huku unapiga mishe zako zingine..

kazi ya serikali ni security tosha if know what i mean

hizi semina za hawa motivational speakers zinawaponza sana watu daaaah
Ushaur wako mzuri, mtoa maana nakushaur uzingatie utakuja juta.
 
Lkn mbona idadi ya wafanyabiashara ni wengi kuliko walioajiriwa na maisha yanakwenda tu siyo wote wafanye biashara kuna uwekezaji wa aina nyingi ufagaji na kilimo
Wengi wanatumia ndagu, ukiingia kweny biashr neutral utalia machozi.
Ingia ukiwa na Mungu kweli kweli au ndagu mi nashaur ingia ukiwa na Mungu san
 
Hakuna shida me nliacha nikiwa na deni la mill 11 equity walinisumbua mwanzoni lakini hawajanisumbua tena
 
wenzako wanatafuta kazi alafu ww unaacha kazi... ushauri wangu usiache fanya kazi huku unapiga mishe zako zingine..

kazi ya serikali ni security tosha if know what i mean

hizi semina za hawa motivational speakers zinawaponza sana watu daaaah
Nonsense ukiajiriwa akili inadumaaa
 
Unapokopa benki, mkopo huo wanauwekea bima.

Kuacha kwako kazi, kufa, kutoroka hakuwasababishii hasara yoyote na wala hawana 'time' na wewe.

Unapoacha kazi, mafao yako hukatwa na mwajiri ambaye ndiye mdhamini wako kuziba pengo la deni lako.

Niseme tu kwamba kuacha kwako kazi hakuhusiani na hasara inayoweza kusababishwa na deni lako benki, hivyo endelea na mchakato wako wa kuacha kazi.
uko vizuri chief
 
Back
Top Bottom