Msaada; Natafuta perfume yenye harufu nzuri

Jamani kuna mkaka niliwahi kusafiri nae mwanza 2 bukoba alikuwa ananukia ki ukweli nilidata ....natamani nimuulize jina la pafyum aliyotumia nashidwa! Natamani nimuombe no nashidwa......kama yuko humu namtafuta
Kama wewe ulikuwa unanuka kikwapa isingewezekana kabisa jamaa kukukodolea macho
 
wana JF, kuna ile unakutana na mtu yaaan kwa jinsi anavyonukia tu unaanza kuwazia akilini "kama huyu si mtumishi wa bank basi atakuwa plan international ama kwenye wizara flan ivi serikalini" ila baada ya udadisi wa karibu unakuja kugundua kumbe ni mtu wa kawaida tu,

Naitaji kufahamu aina ya perfume murua ambayo nikiitumia itanifanya kuwa mkaka mtanashati ninaye nukia vizuri(itapendeza kama ukisema na bei yake).
mkuu kuna uzi wa perfume ukienda kule nadhan utapata hitaji la moyo wako kulingana na hitaji lako
 
husemi Budget yako shauri ako watu wote humu wanaishi mbele perfume utazotajiwa na uhakika hutonunua hata 1..mi nakushauri kiroho safi kanunue kikopo cha mafuta ya Skala kimeandikwa Pefumed petroleum Jelly dukan kwa mangi kinauzwa 500(jero) ila hata 400 anachukua...harufu yake ukipaka Huku mbezi beach mtu wa tandale anaskia.. Sema ndo ivyo inanukia ki beki tatu..Ila we si unataka kunukia Chomoka na hiyo...Mi mwenzako napambana na hali yangu.
 
laki 2.5 perfume tu, huu si mtaji wa mtu mwenye akiri timamu kabisaama huko kwenu south mambo yapo good, bongo watu tuna njaa yaan, perfume ya elf10 hapo mtu kajitahd sana!
Hatari huyu atakuwa sinyule alipanda basi ya kwenda Bukoba maana kwa bei hii alitakiwa kwenda kwa ndege.
 
Wanyama wameubwa kwa asili ya kutambuana kwa harufu zao asili.

1. Mwili hutoa arufu tofauti kama za mvuto wa kimapenzi kwa wote mwanamke na mwanaume kuna haruru ambayo kiasili ukiisikia inasisimua vichocheo vya mwili wako kwenye mapenzi

2. Kuna harufu ambazo mwili hutoa mtu anapokuwa na hasira na hivyo kama mtaalamu ukiisikiatuu hata kama muhusika anaziga anacheka waweza kujua kuwa ndani ya mwili anakaribia kupasuka hivyo ukae naye mbali

3. Kuna harufu zinatoka zikimaanisha ishara ya maginjwa mbalimbali , hivyo kwa tabibu mtaalamu anaweza kukunusa na kujua aina halisi ya uginjwa mgonjwa anaoumwa hata kama mgojwa mwenyewe hajui wala hawezi kujua ni kiungo gani katika mwili kinaumwa.

4. Marashi ,manukato, Perfume zimetengenezwa kwa ajili ya MAITI mbayo tayari mifumo ya arufu ya asili imeisha na sasa anaanza kuoza kwa kushambuliwa na bakteria hivyo harufu hizo kali hutumika kwa muda wakati wa kumuaga isiwe kero kwa wanaomuaga

5. Sasa wewe jitu zima kabisa tena sa nyingine dume kabisa umejitundika marashi ya harufu kali kuliko ya maiti tena unaingia sehemu za uma kama kwenye usafiri ama mikusanyiko na kutawala hali ya hewa na maarufu yako ya kero umekuwa maiti?

6. Unatakiwa uwe msafi tuu na kujipaka mafuta ya kawaida yasio na harufu kali ili kuupa mwili uwezo wake wa kutoa mawasiliano ya kibaolojia ya harufu.
.mmmmmh, Aiseee...
 

Similar Discussions

4 Reactions
Reply
Back
Top Bottom