Msaada: Nasumbuliwa na tumbo sana, natumia dawa sipati nafuu

kipoma

JF-Expert Member
Aug 27, 2012
325
169
Habari wadau,

Naomba msaada wa ushauri, mawazo na namna ya kupata mtibabu ya tumbo maana linauma kama tumboni kuna moto fulani au kuna namna fulani ya mvurugano! Nimefika hospital juzi kupimwa na nikaambiwa nina typhoid! Natumia dawa lakini naona sipati nafuu. Msaada jamani!

Asante!!
 
Unachotakiwa kufanya ni kwenda tena hospitali, ila spitali tofauti ili ukapate second opinion.

Madaktari [pamoja na wauguzi wengine] nao huwa hawajui kila kitu.

Unaweza kwenda kwa huyu akakwambia kitu kisicho kabisa lakini ukaenda kwa yule na akabaini tatizo!
 
Habari wadau, naomba msaada wa ushauri, mawazo na namna ya kupata mtibabu ya tumbo maana linauma kama tumboni kuna moto fulani au kuna namna fulani ya mvurugano! Nimefika hospital juzi kupimwa na nikaambiwa nina typhoid!! Natumia dawa lakini naona sipati nafuu. Msaada jamani!
Asante!!
Kama umeambiwa unayo maradhi ya Typhoid na umetumia dawa za Hospitali hujana ujuwe kuwa hayo maradhi yako ya Typhoid kwa dawa za hospitali huwezi kupona itabidi ujaribu kutumia dawa za asili unaweza kupona.

Kwani Typhoid ya siku hizi haisikii dawa za Hospitali Typhoid imekuwa ni maradhi sugu yasiyosikia dawa za kizungu ushauri wangu tumia dawa za asili utaweza kupona maradhi yako dawa zipo za kuweza kukutibu maradhi yako dawa za asili uguwa pole.
 
Kama umeambiwa unayo maradhi ya Typhoid na umetumia dawa za Hospitali hujana ujuwe kuwa hayo maradhi yako ya Typhoid kwa dawa za hospitali huwezi kupona itabidi ujaribu kutumia dawa za asili unaweza kupona...
Mkuu mzizi mkavu izo dawa za asili za kutibu typhoid ndo kama zipi?
 
mkuu pole sana,yafaa ufike hospitali nyingine ukajaribu tena kwenda pina typhoid pia na vidonda vya tumbo maana vile umeeleza kunadalili ka kunashida nyingine kwenye tumbo
 
Jipe muda,dozi ikiisha kama huna nafuu basi,uangalie namna nyingine.Lakini chukua karafuu nusu kijiko cha chai,mdalasini kijiko kimoja cha chai, na tangawizi kijiko kimoja cha chai.

Vichemshe vichemke kama maji ya kupikia ugali.Ipua,acha viwe uvugu vugu,weka asali halafu kamulia limao.Maji ya kuchemshia yanatakiwa kuwa lita moja na nusu.

Kunywa hivyo kwa siku tano hadi saba unywe ikiwa vuguvugu halafu utaona matokeo mazuuuuri
 
Back
Top Bottom