Msaada: Nasumbuliwa na tatizo la mwili kuchemka kama moto

PAZIA 3

JF-Expert Member
Jan 30, 2018
1,072
1,846
Huwa nasumbuliwa na tatizo la mwili kuchemka kama moto,haswahaswa tumbo na kifua,sometimes na mgongoni,pia mkono wa kushoto huwa unatetemeka sana nikishika kitu,wakati mwingine mapaja hadi kwenye magoti.

Huwa yanawaka moto,vidonda vya tumbo nilishapima hadi safari mbili,but nothing, mikono na miguu nikiilalia vibaya,hata kama ni kidogo tu,inakufa ganzi,,nimeshachoka na hali hii,ni zaidi ya miaka 5 naomba nisaidieni doctors japo ki-mawazo
 
Mkuu unajiumiza mwenyewe unaumwa halafu badala ya kuwaachia wataalamu wao wafanya diagnosis juu ya tatizo lako wewe unaenda pima vidonda vya tumbo!

Rudi hospital haraka elezea hizo dalili na tatizo zako then waachie wao wakupe results na dawa utapatiwa narudiaga hii kauli hakuna tiba on social media.
Nenda hospitali mkuu.
 
Siyo kwamba sijawahi kwenda hospitali ndo maana nikasema ni tatizo la zaidi ya miaka 5, nimepitia mengi tu,so nimeona niwashirikishe labda naweza pata wazo bora zaidi,namna nzuri ya mimi kupona
 
Siyo kwamba sijawahi kwenda hospital,la,ndo maana nikasema ni tatizo la zaidi ya miaka 5, nimepitia mengi tu,so nimeona niwashirikishe labda naweza pata wazo bora zaidi,namna nzr ya mimi kupona
Ulichukuliwa vipimo gani? Kama unakumbuka?
 
Mara nyingi ukielezea kwa doctors,wanafikiria nipime vidonda vya tumbo,stool na urine,
Inabidi urudi hospital ujielezee vizuri zaidi , au nenda hospital kubwa zenye wataalam.

Tafuta wataalam wa nerves. Pia chukua vipimo vya damu kuangalia kiasi cha vitamins, thyroid function, kiasi cha sukari kwenye damu, ufanyaji kazi wa ini pamoja na figo, maana vyote hivi vinaweza sababisha matatizo ya nerves. Unaweza kufanya MRI au CT scan kutambua tatizo.

Huu Ni ushauri tu, cha muhimu rudi hospitali yenye wataalam wakusaidie.

Kila la kheri.
 
Ahsante sana kwa ushauri mzuri,sema huwa sielewi,hivi unaruhusiwa kwenda hospital kubwa kama KCMC bila referal latter? wakati mwingine huwa naogopa kwenda moja kwa moja,,na je kwa kutumia Bima, inawezekana vipimo hivyo? Je unaweza mweleza dactari nataka nipime vipimo hivi na hivi akakubali? maana nilishawahi kwenda sehemu nikiwa nimepanga kupima kisukali,ila jamaa akaniambia,ngoja tukupime CBC/FBC majibu yakaja nipo normal,so huwa nashindwa kumpangia dactari,
 
Inabidi urudi hospital ujielezee vizuri zaidi , au nenda hospital kubwa zenye wataalam.

Tafuta wataalam wa nerves. Pia chukua vipimo vya damu kuangalia kiasi cha vitamins, thyroid function, kiasi cha sukari kwenye damu, ufanyaji kazi wa ini pamoja na figo, maana vyote hivi vinaweza sababisha matatizo ya nerves. Unaweza kufanya MRI au CT scan kutambua tatizo.

Huu Ni ushauri tu, cha muhimu rudi hospitali yenye wataalam wakusaidie.

Kila la kheri.
Asisahau kupima HIV pia
 
Huwa nasumbuliwa na tatizo la mwili kuchemka kama moto,haswahaswa tumbo na kifua,sometimes na mgongoni,pia mkono wa kushoto huwa unatetemeka sana nikishika kitu,wakati mwingine mapaja hadi kwenye magoti.

Huwa yanawaka moto,vidonda vya tumbo nilishapima hadi safari mbili,but nothing, mikono na miguu nikiilalia vibaya,hata kama ni kidogo tu,inakufa ganzi,,nimeshachoka na hali hii,ni zaidi ya miaka 5 naomba nisaidieni doctors japo ki-mawazo
Hii inawezekana ukawa na acid nying tumbon je ulishapata matibabu na je ulishawah kufanya endoscopy
 
Similar Discussions

Back
Top Bottom