Msaada: Napata hedhi isiyoisha!

Miss Worms

New Member
Jun 5, 2021
2
0
Habari Wataalamu!

Hedhi yangu huwa inachukua muda wa siku 4 hadi 5 kuisha, lakini kwa sasa imechukua siku 8 na bado inaendelea kutoka. Pia hedhi kwa kawaida huwa inaambatana na tumbo kuuma ila kwa sasa halijauma hata kidogo na hata dalili nyingine za kwamba nipo period sijapata.

Kuna muda inakuwa inatoka kidogo kama inaelekea kuisha na kuna muda inakuwa kama imekata kabisa halafu inaanza tena.

Naomba msaada/ushauri wenu wataalamu.
 
Unaumwa Abnormal Uterine Bleeding ambayo inasababu mbalimbali kulingana na Umri wako

Inaweza kuwa Uvimbe, Tatizo la Hormone, Ovary kushindwa kuachia hormone zake(Ovarian Failure), inaweza kuwa matatizo ya kushindwa kugandisha damu.

Njoo Hospitali tukufanyie Ultrasound kujiridhisha sio Uvimbe kama sio then ni shida ya kukuongezea tu vichocheo mwilini
 
Mkuu fuata ushauri ulioambiwa na nenda hospitali ukatibiwe, usipo pona nitafute mimi kwa wakati wako ili nipate kukutibia maradhi yako upate kupona.
 
Ongea na dk. luu atakupa ushauri na tiba tatizo lako litaisha. call 0687 439 333
 
Unaumwa Abnormal Uterine Bleeding ambayo inasababu mbalimbali kulingana na Umri wako

Inaweza kuwa Uvimbe, Tatizo la Hormone, Ovary kushindwa kuachia hormone zake(Ovarian Failure), inaweza kuwa matatizo ya kushindwa kugandisha damu.

Njoo Hospitali tukufanyie Ultrasound kujiridhisha sio Uvimbe kama sio then ni shida ya kukuongezea tu vichocheo mwilini
Mimi nimekuvulia kofia ulivyoujua umri wake wakati hajautaja...
 
Tatizo hili kitaalamu hujulikana kama ‘Menorrhagia’, na ni tatizo ambalo mara nyingi hutokana na homoni kutokuwa sawa, uvimbe kwenye kizazi, maambukizi kwenye kizazi, matumizi ya baadhi ya dawa za uzazi wa mpango nk.

Ikiwa unahitaji kufahamu namna ya kutibu tatizo hili la hedhi isiyoisha basi endelea kusoma makala hii kwani ina jibu la tatizo lako.

Nini husababisha kupata hedhi isiyoisha?

Sababu ya kupata hedhi isiyoisha au inayojirudia mara 2 au 3 ndani ya mwezi hutofautiana toka mwanamke mmoja hadi mwingine.
Ikiwa unatokewa na tatizo hili ni mhimu kuonana na daktari mapema kwa uchunguzi na msaada zaidi.

Sababu za tatizo hili ni pamoja na hizi zifuatazo:
1. Homoni kutokuwa sawa
2. Uvimbe kwenye kizazi
3. Ujauzito kutoka
4. Mimba kutunga nje ya kizazi
5. Baadhi ya saratani (saratani ya shingo ya kizazi)
6. Matatizo kwenye mirija ya mayai ya uzazi

Pendelea vyakula vifuatavyo ili kurahisisha matibabu yako:

1. Kula zaidi vyakula vyenye madini ya chuma
Madini ya chuma ni viinilishe mhimu mwili unavihitaji. Kutokwa na damu nyingi au isiyoisha wakati wa hedhi hupelekea kupungua kwa madini ya chuma mwilini na kukusababishia damu kupungua mwilini
Kula zaidi spinachi, karoti, maharage, samaki wa baharini, zabibu kavu, brokoli nk

2. Kula zaidi vyakula vyenye madini ya Magnesium
Kula zaidi ndizi, mtindi na unga wa mbegu za maboga. Kumbuka kuzidisha sana vyakula vyenye madini ya magnesium huleta tatizo la kuharisha hivyo usizidishe.

3. Kula zaidi vyakula vyenye Omega-3

Wanawake wanaopata tatizo la hedhi isiyoishawanapaswa kuongeza ulaji wa vyakula vyenye omega 3.
Omega 3 huhamasisha uzalishwaji wa homoni zenye umhimu na faida zaidi mwilini
Uongezekaji wa uzalishwaji wa homoni mbaya (bad prostaglandings) huchangia kiasi kikubwa kupata hedhi yenye damu nyingi na isiyoisha

Uongezekaji wa uzalishwaji wa homoni nzuri hupunguza damu kuganda kusiko kwa kawaida na kuondoa tatizo la damu ya hedhi isiyoisha.
Omega 3 hupatikana kwa wingi kwenye samaki wa baharini, nazi, mayai, mbegu za maboga nk

4. Kula zaidi papai

Papai lina kimeng’enya kijulikanacho kama ‘papain’ amabacho huidhibiti homoni ya progesterone ambayo hutumika kuandaa mji wa uzazi kwa ajili ya kushika na kuutunza ujauzito.
Kula papai kila siku kunasaidia kulainisha misuli ya tumbo na kuweka sawa kukazika na kutanuka kwa mji wa uzazi jambo ambalo hudhibiti utokaji wa damu ukiwa kwenye siku zako.

5. Kunywa chai ifuatayo kila siku asubuhi

Tumia chai iliyoandaliwa kutokana na kijiko kidogo kimoja kimoja cha unga cha dawa zifuatazo; tangawizi, unga wa majani ya mlonge, mdalasini na kotimiri (parsley) bila kuongeza majani ya chai na utumie asali badala ya sukari kwenye chai hii kwa matokeo mazuri zaidi.
Muunganiko wa chai hii huufanya mwili kuwa na joto na hivyo kupunguza maumivu wakati wa siku zako, kusaidia kukata damu isiyoisha, kuongeza kinga ya mwili na kuweka sawa homoni.

Mambo mengine mhimu ya kuzingatia ili kupona tatizo hili:
• Pata muda wa kutosha wa kupumzika
• Kula vyakula vyenye afya na vya asili zaidi
• Usitumia chai ya rangi, kahawa na soda yoyote au kinywaji kingine chochote chenye kaffeina
• Punguza kidogo chumvi kwenye chakula
• Usitumie vidonge au dawa yoyote ya hospitali ya kuondoa maumivu
• Onana na daktari mara tu upatapo tatizo hili kwa uchunguzi na msaada zaidi
 
Back
Top Bottom