Msaada: Naombeni msaada kuhusiana na soko la bidhaa za electronics | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Msaada: Naombeni msaada kuhusiana na soko la bidhaa za electronics

Discussion in 'Biashara, Uchumi na Ujasiriamali' started by Michael Amon, Apr 18, 2012.

 1. Michael Amon

  Michael Amon Verified User

  #1
  Apr 18, 2012
  Joined: Dec 22, 2008
  Messages: 8,741
  Likes Received: 707
  Trophy Points: 280
  Ninampango wa kuuza bidhaa mbali za electronics kama vile simu za mikononi, laptop, flash disk, camera n.k. Ili niweze kufanikisha hilo ninaombeni msaada wenu kwa yeyote mwenye ufahamu juu ya soko la bidhaa za electronics hasa zile za IT ambazo zinafanya vizuri katika soko la Tanzania na zinazouzika kwa haraka. Natanguliza shukrani zangu za dhati kwa yeyote ambaye atajitokeza kunisaidia katika hili.
   
 2. Trustme

  Trustme JF-Expert Member

  #2
  Apr 18, 2012
  Joined: Jan 7, 2011
  Messages: 1,172
  Likes Received: 9
  Trophy Points: 0
  Soko la hizo bidhaa za electronics lazima liwe maeneo ya mjini ambako kuna umeme. Kwa hiyo fanya utafiti wa soko kwenye miji midogo na mikubwa utapata soko. Kuna baadi pia ya vijiji vina umeme lakini kama unaanza biashara lazima uwalenge wateja wa mjini coz wao ndiyo wenye disposable income (pesa ya ziada kwa matumizi) kuliko wa vijijini.
   
 3. Michael Amon

  Michael Amon Verified User

  #3
  Apr 18, 2012
  Joined: Dec 22, 2008
  Messages: 8,741
  Likes Received: 707
  Trophy Points: 280
  Asante kwa maelezo yako mkuu ila lengo langu ni kujuabidhaa gani za electronics mfano simu za mikononi, laptops, tablet pc n.k vinauzika sana na vina soko zuri hapa Tanzania.
   
 4. h

  haki na usawa JF-Expert Member

  #4
  Apr 18, 2012
  Joined: Feb 26, 2012
  Messages: 476
  Likes Received: 6
  Trophy Points: 35
  Soko si hoja biashara matangazo na ubora kama laptop ni vyuoni zaidi na miezi mizuri ni ile ya kufungua vyuo vikuu (Sept/Oct kila mwaka)

  Kuhusu vifaa vingine vya electronic ni kazi kwani kila kifaa kinategemeana na kazi husika na ndipo upeleke na hakuna soko moja kwa bidhaa zote za electronic lakini sehemu kubwa ni katika tasisi za ELIMU YA JUU YAANI VYUONI
  Sehemu chache sana nje ya watu walioko chuoni kununua vifaa hivyo maana vingine vinahitaji uelewa wa jinsi ya kuvitumia
  Na lazima uwe na Ofisi ya Kudumu ili wanapopata tatizo juu ya kifaa ulichowauzia uwape maelekezo au uwape kingine/vingine kwa vyenye garantii
  Na pia ufanye market survey ili uuze bei pungufu na ili vitoke mapema badala ya kuuza kwa bei juu wanaweza aamua kufuata sehemu ya karibu na kwenda kununua mahitaji mengine ya electronics
   
 5. Michael Amon

  Michael Amon Verified User

  #5
  Apr 18, 2012
  Joined: Dec 22, 2008
  Messages: 8,741
  Likes Received: 707
  Trophy Points: 280
  shukrani sana mkuu kwa maelezo yako. Nitayafanyia kazi.
   
 6. Candid Scope

  Candid Scope JF-Expert Member

  #6
  Apr 18, 2012
  Joined: Nov 8, 2010
  Messages: 11,896
  Likes Received: 119
  Trophy Points: 160
  Nimefanya utafiti wa vifaa hivyo vya electronic unavyokusudia kufanya biashara, kwa upembuzi wangu yakinifu ni bora jaribu kufanya utafiti wa kutosha usije jutia kuweka mtaji katika biashara ambayo soko lake limeshakaliwa na wengi.
  Kila kona na hasa mitaa mingi mijini imejaza vifaa vya electronic kwa sana tu. Kariakoo ndo usiseme. Mwenyewe nilikuwa nafanya utafiti wa kuanzisha biashara hiyo nimeona ni kupoteza mtaji wangu bora nibuni kitu kingine. Wengi wenye biashara hiyo wana mikataba na makampuni husika, hivyo huuza vitu kwa bei ya chini, sasa we ukiamua kununua vitu kwa njia za panya unaweza kushtukia unawajibika kuuza kwa bei mbaya kuliko hao wanaoletewa na makampuni.

  Kwa ujumla vifaa vya electronics hakikisha umefanya utafiti wa kutosha na eneo gani linafaa vinginevyo ushindani ni mkubwa sana. Ila unaweza kupata eneo ambalo halina ushindani ukawa na biashara nzuri na hasa kama una bidhaa za kiwango ambacho wenye pesa wanataka unaweza kufanya biashara nzuri tu.
   
 7. Michael Amon

  Michael Amon Verified User

  #7
  Apr 18, 2012
  Joined: Dec 22, 2008
  Messages: 8,741
  Likes Received: 707
  Trophy Points: 280
  Nashukuru sana kwa ushauri wako mkuu. Nitaufanyia kazi.
   
 8. m

  majogajo JF-Expert Member

  #8
  Apr 19, 2012
  Joined: Oct 9, 2011
  Messages: 321
  Likes Received: 5
  Trophy Points: 0
  ok utakapo anza unitaarifu na mimi niwe mteja wako
   
 9. Michael Amon

  Michael Amon Verified User

  #9
  Apr 19, 2012
  Joined: Dec 22, 2008
  Messages: 8,741
  Likes Received: 707
  Trophy Points: 280
  Usijali mkuu. Nitakutaarifu.
   
 10. N

  Ndjabu Da Dude JF-Expert Member

  #10
  Apr 19, 2012
  Joined: Aug 29, 2008
  Messages: 3,653
  Likes Received: 409
  Trophy Points: 180
  Cha kutilia maanani ni voltage ya hivyo vifaa vya umeme na electronics. Tanzania wanatumia 220 Volts-240 Volts. Kwa tuliyo Marekani, ni disaster, kwani soko la vifaa kama hivyo ni kubwa sana.
   
 11. Michael Amon

  Michael Amon Verified User

  #11
  Apr 19, 2012
  Joined: Dec 22, 2008
  Messages: 8,741
  Likes Received: 707
  Trophy Points: 280
  Hilo nalifahamu mkuu ila nashukuru kwa ushauri wako. Nitalitia maanani.
   
 12. Manyanza

  Manyanza JF-Expert Member

  #12
  Apr 20, 2012
  Joined: Nov 4, 2010
  Messages: 4,446
  Likes Received: 21
  Trophy Points: 135
  Zingatia ushauri wa Candid Scope, mkuu usije ukaingia mkenge na ukajutia kwa kupoteza mtaji wako bure, tembelea jukwaa hili utaona thread nyingi zinazohusu jinsi ya kuanzisha miradi/biashara mbalimballi kwa mtaji mdogo sana
   
 13. Michael Amon

  Michael Amon Verified User

  #13
  Apr 20, 2012
  Joined: Dec 22, 2008
  Messages: 8,741
  Likes Received: 707
  Trophy Points: 280
  Asante sana mkuu kwa ushauri wako. Nitaufanyia kazi.
   
Loading...