Msaada naomba ufafanuzi katika hili la hedhi ya siku mbili na ujauzito

Osmokalu

Senior Member
Nov 13, 2015
183
143
Hivi mwamke anaetumia siku 2 tu kwa hedhi anaweza pata uja uzito na siku zake hatar kwa yai kushuka na kushika mimba ni zipi.
 
Hivi mwamke anaetumia siku 2 tu kwa hedhi anaweza pata uja uzito na siku zake hatar kwa yai kushuka na kushika mimba ni zipi.

Habari,
Moja ya kitu tunachotakiwa kuelewa ni kwamba:
1: Siku za yai kupevuka/hatari/nzuri kulingana na wewe unavyoweza kuziita kulingana na lengo, hazitokani na idadi ya siku ambazo mwanamke hutumika/kuwa kwenye hedhi.

2: Siku hizi hutokana na urefu wa mzunguko wa mwanamke husika/hapa tunazungumzia wale wenye mzunguko maalumu(idadi ya siku sawa toka mzunguko mmoja mpaka mwingine).

3: Mzunguko wa mwanamke yeyote unakubalika kuwa sawa kama una urefu wa siku kuanzia 21 mpaka 35.

4: Kwa wastani wanawake wengi wana mzunguko wa siku 28.

5: Kutokana na utofauti huo hapo juu, ni vyema kufahamu kuwa siku ya kupevuka yai itategemea unayemzungumzia ana urefu gani wa mzunguko wake.

6: Urefu wa mzunguko huesabiwa tangu siku mhusika anapoona tone la kwanza mpaka atakapoona tena tone la kwanza kwa mzunguko unaofuata.

7: Hii ndiyo inayoleta utofauti na mkanganyo kati ya akina mama mfano: mtu ana mzunguko wa siku 21, anategemea atapata ujauzito siku ya 14, kumbe kulingana na mzunguko wake yeye anapevusha yai siku ya saba (7) ya mzunguko. Hapa ndiyo tunapata mimba zisizotarajiwa au mkanganyo ndani ya ndoa mfano: mimi sikuwepo tarehe hiyo.

8: Fuatilia mzunguko wake kwa miezi 3, idadi utakayopata kama ni ilile ni vyema zaidi. Idadi hiyo toa siku kumi na nne, hapo utapata siku ambayo ni likely/ inayotazamiwa kuwa yai linachavuka/ linatoka.

Lakini pia, tunalimishana wakati wa kianganzi na kupishana na gari ya la mshahara.

Ahsante.
 
Back
Top Bottom