Msaada: Naomba msaada wa kimawazo kuhusu suala hili, nahisi kuchanganyikiwa

Allydasmartboy001

JF-Expert Member
Jul 14, 2018
575
250
Habari za muda huu ndugu zangu naombeni msaada wa mawazo.

Ngoja nianze kwa maelezo mafupi kwanza nilimaliza A level - PCB miaka miwili iliyo pita na matokeo yangu hayakuwa mazuri kijumla nilikuwa na two ya 12 ambapo CHEM - C BIOS - C na PHY - S.

Nilijaribu kuomba Degree ila nilipataga Ualimu wa CHEM na BIOS. Wakati naomba degree niliomba pia na diploma ya medicine napo pia nilipata.

Kwakuwa ndoto zangu zilikuwa ni Udaktar ikanibidi niende diploma. Mwaka jana nilifanya mtihani wa NACTE na nilipata sup mbili ya clinical skills na patient care.

Nikaendelea kusoma level 5 sem 1 huku nikisubiria mwez wa 2 nichomoe supp zangu. Nikafanya mitihani ya level 5 sem 1 na supp zangu.

Juzi matokeo yakatoka level 5 sem 1 nilipata pass ya GPA ya 3.6 Ila level 4 clinical skills ikanikamata tena kwa hiyo nimepata RM ya clinical skills.

Jana Sir ametwambia wale wote wenye RM matokeo yao ya Level 5 sem 1 yatafutwa hvyo watabidi wasome tena upya baada ya kufaulu somo walilopata RM.

Kumbe waliletewa utaratibu kwanzia mwaka jana mwez wa 9 kuwa wenye supp wasiendele na level inayofuata mpaka watakapo chomoa masomo yao. Ila chuo chetu hawakutuambia kabisa hili swala awali na ada zetu walichokuwa bila kutuambia wanakuja kutuambia jana tena baada ya matokeo.

Naombeni msaada kwa haya mambo mawili la kwanza
"Kuna mtu aliniambia kwa hayo matokeo ya a level ambayo ni chem c bios c na phy s naweza pata chuo uganda hata kampala na weza pata ila inabidi nimtafute connection ya kunisaidia. Swali je kwa hayo matokeo ya a level naweza pata chuo uganda kusomea md au naweza pata nchi gani ila uwezo wa wazaz wangu mwisho ni mil 4? La pili.

"Je nifanye utaratibu gani endapo chuo kikigoma kunirudishia hela zangu au hakuna utaratibu wowote? (namaanisha hela yangu ya ada ya level 5 sem 1 ambayo ni 1.7m)".

Kama unaushauri wowote naomba unisaidie kwa kweli maana sielewi hadi muda huu na kikubwa ni muda tu ndio tatizo.

Asante sana na samahani kama nitakuwa nimetumia lugha vibaya na rm maana yake ni repeat module na supp maana yake ni supplementary
 

chimbo boy

Senior Member
Jul 20, 2020
127
250
Kama umeshinda kufaulu supp ni lazima urudie mwaka utaratibu ni kwamba unarudia somo husika tu..lkn pia kulipwa ada haiwezekani,hivi tumia chet chako cha advance kusonga mbele
 

Allydasmartboy001

JF-Expert Member
Jul 14, 2018
575
250
Kama umeshinda kufaulu supp ni lazima urudie mwaka utaratibu ni kwamba unarudia somo husika tu..lkn pia kulipwa ada haiwezekani,hivi tumia chet chako cha advance kusonga mbele
Sawa hilo na lijua lakn utaratibu component zangu si zinatakiwa zihifadhiwe
 

Fazz

Senior Member
Mar 14, 2019
150
250
Mkuu upo chuo gani ..na kwanini hawakuwaambia mapema manake utaratibu upo was lazima uchomoe sap ndo uendelee lakin Kama mliambiwa mkaforc Hilo ni tatizo lingine muhim hap ni kujiorganize na kuona chuo kitawasaidiaj hat kuwapunguzia ada kimtindo

Sent from my itel S33 using JamiiForums mobile app
 

Allydasmartboy001

JF-Expert Member
Jul 14, 2018
575
250
Mkuu upo chuo gani ..na kwanini hawakuwaambia mapema manake utaratibu upo was lazima uchomoe sap ndo uendelee lakin Kama mliambiwa mkaforc Hilo ni tatizo lingine muhim hap ni kujiorganize na kuona chuo kitawasaidiaj hat kuwapunguzia ada kimtindo

Sent from my itel S33 using JamiiForums mobile app
sisi hatukuambiwa waliombiwa ni hawa wa mwaka huu waliofanya nacte feb
 

Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Top Bottom