Msaada: Naomba kujuzwa jinsi ya kupata uraia kwa msichana anayetoka nje ya nchi ili kuolewa na kuishi Tanzania

Mkuu Hongera kwa kuopoa kifaa. Vema pia kwa mrembo wako kuchagua kuja kuishi Tanzania. Inahitaji moyo ujue.

Cha kufanya, mlete aje Tanzania. Funga naye ndoa halali inayotambulika kisheria. Kisha ndiyo muanze mchakato wa kumpatia uraia.

Kwanza, tambua kuwa nchi yetu bado haijaruhusu uraia pacha. Hivyo itambidi aukane uraia wa nchi yake ya Australia.

Mtaenda kwenye ofisi za Idara ya Uhamiaji katika mahali ulipo. Iwe wilayani, mkoani au Makao Makuu pale Kurasini.

Mtapewa fomu maalum ya kujaza. Mtajaza kwa umakini na kuirudisha. Mtaambatanisha vithibitisho kadhaa ikiwa ni pamoja na;
A)Kithibitisho cha Uraia wa mume
B)Cheti cha ndoa
C)Passport size za hivi karibuni
D)Kibali cha kuwepo hapa nchini
E)Makorokocho mengine

Mtajaza hiyo fomu na kuiambatanisha na kiasi cha Dola 1500 (USD). Kama imebadilika mtaambiwa.

Mkishajaza muhusika atatoa Tangazo mara mbili kwenye Gazeti la Serikali juu ya nia yake ya kuomba Uraia wa Tanzania.

Baada ya hapo ombi litapelekwa kwa Kamishna Mkuu wa Uhamiaji. Kama hakutakuwa na mapingamizi Baadae nae atapeleka kwa Waziri husika kwa kuhalalishwa uraia wenyewe.

Kila la kheri Mkuu.
Akipata na katoto akape jina la kikabila.
 
Halafu siku mkiachana huyu Mwanamke itabidi aingie kitaani peke yake kuanza life la kibongo? Hakuna mwanamke wakufanya kosa kama hilo,Mkuu naona kabisa kua unaingizwa cha Kike na imebakia tu utume nauli,

Jaribu kumwambia kua anaonaje kama wewe ndio uende huko Australia ili muanzie maisha huko? akikutolea nje jua kabisa kua unaingizwa mkenge mchana kweupee!
 
Vijana wa Lagos wako kazini.
Mkuu unakaribia kuliwa kichwa na Yahoo boyz! Utaleta mrejesho hapa hivi karibuni.
Mie mwenzio hadi video calls zilihusika nikajua nimepata mpenzi wa kidachi kumbe laaah nachazeshwa na akina Yahoo boyz toka mitaa ya Lagos!! Nilikuja kuokolewa na ki anko changu na zile pesa nikaona bora nikanunue shamba.
 
Vijana wa Lagos wako kazini.
Mkuu unakaribia kuliwa kichwa na Yahoo boyz! Utaleta mrejesho hapa hivi karibuni.
Mie mwenzio hadi video calls zilihusika nikajua nimepata mpenzi wa kidachi kumbe laaah nachazeshwa na akina Yahoo boyz toka mitaa ya Lagos!! Nilikuja kuokolewa na ki anko changu na zile pesa nikaona bora nikanunue shamba.
Duh
 
5 Reactions
Reply
Back
Top Bottom