Nitampata wapi Daktari na hospitali nzuri ya macho mzuri?

klorokwine

JF-Expert Member
Nov 4, 2014
378
27
Habari wakuu,
Ninasumbuliwa na macho, ni hospital gani ya private naweza pata daktari mzuri wa macho siku ya leo?
Msaada wenu kwa anayefahamu tafadhali.
 
CCBRT kuna foleni kweli ila wapo vizuri sana, mimi nimepata huduma hapo ya macho
 
nenda pale kona ya kigogo kuna hospitali ya prof mtanda wa muhimbili ni mzuri sana
 
Uko utaratibu pale CCBRT wa kufanya appointment unamuona eye specialist katika muda na siku utakayopangiwa hii haina foleni . Mwaka jana ilikuwa consultancy peke yake ni TSH 50,000/= kwa sasa sina hakika
 
Salaam,

Je wajua kliniki mzuri ya kupima macho na kupeo wa miwani hapa Dar?

Tafadhari nijulishe.

Ahsanteni.
 
nisaidie nahaitaji kupimaa macho yananiumaa snaa na kuwa mekundu na ukakasi kma mchanga pia kichwa huuma kwa mbali, naombaa kufahamishwa hosp nzur yenye specialist wa macho ili aweze nisaidia.tafadhali.
 
CCBRT ila ikifika kipengele cha miwani kama wewe ni mwenye bima utapewa,
kama ni mtegemezi unanunua ila vingine bima inafanya kazi
 
Habari za majukumu wazee wangu,

Nina shida ya macho imeanza mwezi mmoja nyuma, nikisoma sms za kwenye simu au nikisoma maandishi kichwa kinauma na macho yanawasha sana.

Ninahisi pengine matumizi ya simu na laptop ndio sababu mojawapo ila sina uhakika maana mimi sio mtalaamu.

Nilikuwa naomba kujua clinic nzuri ya macho ya sisi wananchi wa kawaida ila service iwe ya kiwango cha kuridhisha.

Nitangulize shukrani zangu za dhati kwenu wakuu.
 
Habari ya usiku huu wapendwa.

Kama kichwa cha habari kinavyojieleza hapo juu,nimekuwa nikisumbuliwa na kichwa mara nyingi sana.

Juzi kilinizidi mpaka nikahisi ni corona Wallah😂😂😂 (maisha kweli matamu) ikabidi niende kufanya vipimo nikakutwa na nilichokutwa na dawa nikapatiwa lakini bado kichwa kinaniuma sana.

Kuna kipindi mtu alinigonga na kiwiko kwenye jicho bahati mbaya siku iliyofuata nikashindwa kufungua macho kabisa. Nikaendea hospital nikapatiwa dawa likakaa sawa. Baadae tena likaanza kunisumbua nikaenda hospital nikapatiwa dawa nikatumia likakaa sawa.imepita mda kidogo.

Wiki kama mbili tena limenianza kuuma nikilifungua kunakuwa na vitu kama vinachomachoma.na upande jicho linalouma,ndipo na kichwa kinauma mno upande huo huo.

Asanten
 
Mimi nafanya kazi medewell health center ipo Kibaha tunayo huduma hiyo, unaweza ukaja kutembelea tuna kitengo cha macho kizuri ambapo tuna fanya operation ya mtoto wa jicho bure bila garama yoyote endapo utagundulika na tatizo hilo.

Pia gharama ya kumwona Daktari wa macho elfu 5. Pia gharama hizi haziambatani na za dawa. Pia tu kwanini tunafanya cataract bure. Ni bure kwakuwa ni charitable center hivo kama na ndugu jamaa rafiki mlete asaidiwe na hawa wahusika wa macho wenye shida ya mtoto wa jicho.

Medewell ipo Kibaha Mpakani Mezani ya zamani. Ukishuka hapo utaona bodaboda wengi tu watakufiksha mpka kituo cha hudumua bodaboda ni shiling elfu moja tu. Hivyo siku za huduma za macho kuanzia j3 hadi alhamisi. Unashauriwa kuwah alfajiri sana ya saa kumi na mbili na nusu hadi saa moja kamili uwe umefika. Pia unaanza mapokezi utawaeleza umekuja kwenye huduma ya macho utapewa namba.na utaelekezwa wapi pa kwenda kulipia hiyo elfu 5 yako.

Unashauriwa kuwahi kuchukua namba ili kuwa miongoni mwanaotakiwa kumwona daktari kutokana na idadi iliopangwa ndan ya siku hiyo.

Hivyo bas kama utagundulika na shida ya ya mtoto wa jicho utaandikwa kwenye kitabu maalumu kukuweka kwenye orodha ya watu wa kufanyia upasuaj huo mdgo. Kisha utaambiwa ukae karibu na simu yako watakupigia simu ndan ya week mbili.
 

Similar Discussions

0 Reactions
Reply
Back
Top Bottom