Msaada: Naomba kujua kuhusu course ya Bachelor of Science in Biology’ kuanzia kwenye usomaji hadi kupata kazi

Mbagala stendi

JF-Expert Member
Nov 8, 2020
289
266
Habarini wadau wote wa elimu.

Nina mdogo wangu kapangiwa hiyo course hapo UDOM

Napenda kujua changamoto za course ndani ya chuo na nje ya chuo, hususani katika soko la ajira kwa sababu course za biology pale UDSM zimevunjwa.

Na katika ushindani hivi ni kweli anaweza kufiti sehemu nyingi kwasababu wawo wanasoma biology in general.

Na pia napend kujuzwa field gani za graduaters wa hii course wanaweza kufanya kazi hukiachana na taarifa za mtaani ya kuwa hakuna jingine zaidi ya kuwa mwalimu wa tuition.

karibuni kwa ushauri.
 
Kwa ushauri wangu, ingawa sio wakitaalamu sana, kama ufaulu wa Chemistry upo vizuri, akifika afanye kuhamia BSc. Chemistry. Ni rahisi kuhama kwasababu kozi zote mbili zipo ndani ya College moja.

College anayoenda ni College of Natural and Mathematical Sciences (CNMS). Kozi za hapo ni:-
BSc. Biology (School of Biological Sciences)
BSc. Chemistry (School of Physical Sciences)
BSc. Physics (School of Physical Sciences)
BSc. Mathematics (School of Mathematical Sciences)
BSc. Statistics (School of Mathematical Sciences)
Na BSc. Education, ualimu amboa hauna Minor (With Education). Unamajor masomo yote mawili.

Hali ya ajira ni tete lakini hata kabla hatujafika huku, watu wa Biology, Mathematics na Physics tayari walikua wanaipata joto ya jiwe.

Watu pekee wenye unafuu ukiachana na walimu wenye Physics ni watu wa Chemistry wakifuatiwa na Statistics.

Isisahaulike kua hakuna jambo rahisi, kwahiyo lengo lisiwe kufata urahisi. Pia ifahamike kua ufaulu dhaifu hauvutii, hivyo licha ya soko zuri linaloendelea kukua la watu wa Chemistry, akihamia hapo ahakikishe anatoka na ufaulu unaoridhisha.
 
Kwa ushauri wangu, ingawa sio wakitaalamu sana, kama ufaulu wa Chemistry upo vizuri, akifika afanye kuhamia BSc. Chemistry. Ni rahisi kuhama kwasababu kozi zote mbili zipo ndani ya College moja.

College anayoenda ni College of Natural and Mathematical Sciences (CNMS). Kozi za hapo ni:
Asante kiongozi kwa ushauri. Nitajaribu kumshauri ahame kozi hata mimi naona kwenye chemistry kuna ajiri nyingi sana hukilinganisha na biology. Kuhusu ufaulu sina shakha kabisha kafaulu vizuri.
 
Bsc biology huyu siyo mwalimu hana education anatakiwa aende sijui hata wapi sijui mambo gani ambayo huku tz ni ngumu fanya utafiti vizuri mkuu angeenda dip ya nursing
 
Lakini kiongozi nimepata fununu ya kuwa mtu ambaye kasoma Bsc biology au chemistry au physics ana qualifications za kwenda popote kwenye sekta ya afya ikiwemo MD, nursing, pharmacy.....so hakuna haja ya kurudishana nyuma kuanza diploma kama una lengo la kusoma degree. Tena sio tanzania tu nchi zote wanafanya hvyo.
 
narudia tz ni ngumu sana pia fanya utafiti wa kutosha...kuna thread huku ya mtu wa Bsc physics itafute hizo fununu kuwa huenda si kweli
 
Nina ushahidi na ninachokiongea jaribu kuangalia entry requirement utajionea mwenyewe chuo kama muhas, kcmco, cuhas, st francis.....
 
Jidanganye tu...

Huu ndio upuuzi mkikutana wakati mnatafuta coarse za kusoma ndio mnadanganyana hivi...

Huyo mtu wa pharmacy tu hawez kufanya kazi za nursing sembuse wewe ulisoma biology..

Kasome diploma ya nursing au clinical officer hakuna mjadala tena...
Lakini kiongozi nimepata fununu ya kuwa mtu ambaye kasoma Bsc biology au chemistry au physics ana qualifications za kwenda popote kwenye sekta ya afya ikiwemo MD, nursing, pharmacy.....so hakuna haja ya kurudishana nyuma kuanza diploma kama una lengo la kusoma degree. Tena sio tanzania tu nchi zote wanafanya hvyo.
 
Lakini kiongozi nimepata fununu ya kuwa mtu ambaye kasoma Bsc biology au chemistry au physics ana qualifications za kwenda popote kwenye sekta ya afya ikiwemo MD, nursing, pharmacy.....so hakuna haja ya kurudishana nyuma kuanza diploma kama una lengo la kusoma degree. Tena sio tanzania tu nchi zote wanafanya hvyo.
Kwa hiyo mkuu, unataka kusema "Ndugu yako asome Miaka 3, then aombe kwenda Degree yoyote ya Afya?"" Kwa hiyo hiyo Miaka mitatu atakuwa ni kama alikuwa anakua tu kiumri na kiakili??

Embu pima pia na kama angeitumia hiyo Miaka Mitatu kusoma Diploma ya Pharmacy au Nursing au Radiology au Clinical officer (hii Miaka mitatu akimaliza anaweza kuajiriwa, na Baada ya Miaka kadhaa akarudi kujiendeleza tena huku akiwa na Mshahara wake na pengine akiwa kapanda daraja la Mshahara kabisa).

Au Labda unataka hiyo Miaka 3 aitumie kula Bumu la Serekale...akimaliza...nimekumbuka kitu..ANAWEZA KUSOMA HIZO KOZI ALIZOCHAGULIWA, AKIMALIZA AKASOMEE MASTERS YA MAMBO YA AFYA (kuna Masters za microbiology etc kutoka Vyuo vya Afya) halafu baada ya hapo kama kuna njia ya kupata ajira huko anaweza kupata (Hii nakutaka ufatilie, uulizie..inaweza kuwa nzuri pia)

Ila pia kama kwenu mna mshiko, pia Dogo anaweza kusoma hizo Kozi alizochaguliwa, ale boom, afaulu vizuri, baada ya hapo ajiunge tena na Degree za afya mumlipie Ada, amalize fresh (future kwake iwe green)...Hii nayo nzuri kwa wenye Hela.

TAFAKURI .
 
Umetisha bro ushauri mzuri sana.
Kwa sasa dogo ana ufaulu wake ni mdogo 2.10 PCB, so imekuwa ngumu kwenda direct to the field that he love.

Ukiangalia diploma 3 pia degree 3 wote ni sawa kwa miaka ya kukaa shule.
Competition diploma to degree competition huwa kubwa sana anaweza kupotesa pesa kama alivyopotesa mwaka huu. Pia GPA za NACTE kuzipata ni shida kidogo .

Na ukiangalia degree atakuwa na chance kubwa kuchaguliwa kwa sababu waombaji degree to degree ni wachache vyuo kama muhas na kcmco hawatakuacha.

Hapo nahisi changamoto labda pesa lakini kama maandalizi ya kiwa vizuri haitasumbua.
 
Mbona alifaulu vizuri tu...Alikosa hata Degree ya Medical Lab CUHAS, KCMC? Alikosa hata Bsc Nursing??? Alikosa Bsc Pharmacy, Nursing St John????
 
Back
Top Bottom