Habari zenu wadau,
Kuna kitu nimekua nikikiona kimeandikwa mbele ya gari RS (hasa hizi gari ndogo). Na mda mwingine nimeona kwenye matangazo ya magari kwamba gari ina mfumo wa RS
Mkuu RS ni package tu katika brands za magari kama ilivyo LT, LX, LS au XLE. Sijajua uliona katika gari gani na ni katika body au katika front grill. Kama katika body ni package ya ndani ya gari ila kama katika grill, wengi wanaweka kama pambo tu.
RS kirefu chake ni Rally Sports au "Rennsport" in German. Utaona sana katika magari kama Audi, Posche na sports cars nyingine.
Toyota nae ana version za RS kama Vitz RS ambayo ni Vitz ya kawaida iliyokua modified na Toyota Racing Development (TRD).
JamiiForums uses cookies to help personalise content, tailor your experience and to keep you logged in if you register.
By continuing to use this site, you are consenting to our use of cookies.