Msaada: Namtafuta Carlos Sendwa | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Msaada: Namtafuta Carlos Sendwa

Discussion in 'Matangazo madogo' started by Lekanjobe Kubinika, Jan 18, 2010.

 1. Lekanjobe Kubinika

  Lekanjobe Kubinika JF-Expert Member

  #1
  Jan 18, 2010
  Joined: Dec 6, 2006
  Messages: 3,067
  Likes Received: 18
  Trophy Points: 135
  Jamani naomba anayejua mtu huyu alipo anisaidie kumpata. Anaitwa Mr Carlos Sendwa, alisoma PCB sekondari ya Pugu STream G 1980-82. Wakati huo mimi nilikuwa PCB stream F, mwenyeji wa Mbeya. Wazazi wake walikuwa wanaishi Mikocheni (?), ni mhehe wa Iringa.

  Tulipoteana kiaina hata sielewi, enz hizo hakukuwa na urahisi wa mawasiliano kama sasa. He was a very good friend of mine. Siku moja nadhani 2002 niliwona maeneo ya Muhimbili akitoka kupitia geti la MUHAS, nilikuwa kwenye daladala na sikufanikiwa kumshawishi konda asimame nishuke kumwona huyu bwana, niliporudi nikakuta ameshaondoka, nadhani alipanda daladala.

  Why important now? Ihave remembered this friend so much that I feel it fair to start tracing him through this platform. Nikijua yuko wapi lazima tutafanya kila njia tukutane na angalau tusalimiane. Nimesoma nao watu wengi lakini this guy was special of his kind.

  Do me a favour, please. Namshukuru mwana JF mmoja aliyenielekeza njia ya wapi niweke hili - kama tangazo.

  Leka
   
 2. Original Pastor

  Original Pastor JF-Expert Member

  #2
  Jan 18, 2010
  Joined: Nov 14, 2007
  Messages: 1,256
  Likes Received: 10
  Trophy Points: 135
  Una bei gani mkuu. si unajua town hapa
   
 3. Lekanjobe Kubinika

  Lekanjobe Kubinika JF-Expert Member

  #3
  Jan 18, 2010
  Joined: Dec 6, 2006
  Messages: 3,067
  Likes Received: 18
  Trophy Points: 135
  Tumsifu Yesu Kristu.
  Kwanza wewe ni Paster. Tena Original basi. Unahubiri mapendo, sijakusikia ukihubiri uzuri wa tamaa ya pesa. Bei yake si unajua tena, utalipwa Mbinguni???

  Wewe toa tu ulicho nacho unajiongezea hazina Mbinguni. Niambie basi, unamjua huyu mtu?

  Leka
   
 4. Teamo

  Teamo JF-Expert Member

  #4
  Jan 18, 2010
  Joined: Jan 9, 2009
  Messages: 12,286
  Likes Received: 51
  Trophy Points: 145
  unamtaka wa nin?
   
 5. Lekanjobe Kubinika

  Lekanjobe Kubinika JF-Expert Member

  #5
  Jan 18, 2010
  Joined: Dec 6, 2006
  Messages: 3,067
  Likes Received: 18
  Trophy Points: 135
  Ebo! Simtaki, namhitaji. Tumepoteana siku nyingi mno na asa nimeanza kumkumbuka. Kumwona nikiwa kwenye daladala ndio kabisa kumeongeza kasi ya kutaka kuonana naye. Ni rafiki yangu na sina tatizo naye. Kwanza jamaa mwenyewe yule si mgomvi kiasi cha kuhofia kuniambia. Labda kama kabadilika. N mbali, tangu 1982!!! Najua pa kuanzia ni hapa.

  Geoff, au una mashaka gani nami au naye? JF si mojawapo ya raha yake ni kuwasiliana marafiki? Majina yenyewe sio rahisi kujua hapa, labda ni wewe? Nimeeleza kwa kina, kama ungekuwa ni wewe bila shaka ungevuta picha na ukakumbuka. Hata kama nitasema tuonane wapi kama sio wewe nitajua ntu, maana jamaa hajabadilika sana, hata mimi atanitambua upesi sana. Ni mtani wangu lakini tuliishi kama ndugu zaidi ya rafiki. JKT ilitutawanya.

  Leka
   
Loading...