MSAADA: Namtafuta baba yangu Charles Muyumbilwa

Kwanza nitoe shukrani kwa member wote wa JF kwani kupitia uwanja huu wengi wamerudisha tabasamu baada ya kuonana na wapendwa wao.

Kama kichwa cha habari kilivyo ni kwamba.
Mimi UMBO CHARLES MUYUMBILWA(ke 26age) ninayeishi Mbeya Uyole ninamtafuta baba yangu ambaye kwa taarifa za mama ni kuwa waliishi Tanga muheza kijiji cha Maduma kwa kaka wa baba ambaye alikuwa askari.

Baba aliondoka kwenda masomoni dar mwaka 1994 akamuacha mama kwa bibi mzaa baba aliyejulikana kwa jina la SEKIDUMBA kijijini hapo MADUMA huko Tanga. Baba alimwacha mama akiwa na ujauzito wangu hapo kwa bibi.

Baada ya miezi kadhaa mama alijifungua mimi January 1995 na miezi michache mama aliondoka akarudi kwao Mbeya Usangu Mlangali kijiji cha Kutulo na kuendelea kuishi huko hadi sasa.

Nimesoma huku Mbeya nikilelewa na Mama yangu aitwaye Mariam Mjagala.

Inasemekana baba aliwahi kuja Mbeya kumtafuta mama ila aliishia mjini hakujua vijiji ambavyo tupo hivyo hakufanikiwa.

Naomba kwenu watanzania wenzangu mnisaidie kumuona na kumjua baba yangu hata kama alikufa basi nijue ndg zake na alipozikwa na kama ni mzima basi anione mwanaye nami nimuone.


Mawasiliano 0747 525 891 UMBO CHARLES MUYUMBILWA.
Huyo mama aliondoka Tanga kwenda Mbeya kwa utaratibu upi? Aliacha maelekezo ya lini atarudi? Au wapi Mbeya anaenda ili huyo jamaa akirudi toka masomoni ajue pa kumpata?
 
Back
Top Bottom