Msaada: Namna ya kurudisha furaha inayopotea

Sigara Kali

JF-Expert Member
May 28, 2017
3,623
8,428
Wakuu salaam,

Kama mada inavyojieleza,

Miaka ya karibuni hasa kuanzia 2015 mwishoni nimekua mtu nisiyekua na furaha na nikiwa na furaha basi ndani ya siku chache huondoka
labda nieleze kinagaubaga jinsi maisha yangu yalivyo.

Wazazi wangu washafariki almost 16 years ago, tangu wakati huo ndugu ambao nilikua nawategemea wakaanza mizinguo so nikaanza kuishi ghetto tangu nipo form 1 hadi namaliza form 4, then nikachaguliwa kuingia advance so kipindi chote nasoma advance likizo zangu karibia zote zikiishia maghettoni kwa masela kwa sababu kule home sikua na watu ambao wa kuwategemea sana.

Ada nilikua nalipiwa tu na msamaria mwema mmoja.Nimemaliza form 6 nikafaulu kwenda chuo na Mungu si athumani nikapata mkopo kwa 90% nikaanza maisha ya chuo pale SUA, baada ya muda nikaamua kutoka hostel nikapanga ghetto maisha yakaendelea.

Wakati huu nikiri kwamba nilikua mtu mwenye furaha muda wote sikua mtu wa mawazo mawazo. Mwaka 2012 nikakutana na mwanamke barabarani pale mjini Moro yupo na mabahasha yake anatafuta kazi nikamwomba namba, nikaanza kumtongoza mtoto akakubali tukawa wapenzi.

Baada ya muda binti kapata ujauzito nikamwambia atoke kwao (kwa mama mdogo wake) nikaishi nae ghetto kwa amani na upendo. Wakati ana mimba akaitwa interview akapiga fresh, akarudi ghetto, maisha yakaendelea ya furaha, amani na upendo, binti kajifungua salama salimini.

Kumbukeni wakati ana ujauzito nilimfungulia biashara ndogo
baada ya mtoto kutimiza kama miezi 4 hivi mama yake akapata kazi kule alikofanya interview tena kwa mshahara mnono zaidi ya ule wa aupatae mwenye degree. Nikauza baadhi ya vitu vyangu mama na mtoto na ndugu yake wakasafiri hadi kituo cha kazi alichopangiwa.

Wakati huo mimi nishamaliza degree yangu nikaingia rasmi kitaa, kama mnavyojua nchi yetu ina changamoto za ajira, hapo ndo suala la kutokua na furaha likaanza. Nikasafiri hadi kwa mama mtoto nikakaa kwa muda then nikaingia mkoa jirani huku huku lake zone kutafuta mishe nikapata nikaanza kazi na nikapanga chumba, mwisho wa siku ikawa mtihani kulipwa basi kazi ikashindikana nikaondoka kurudi kwa mama mtoto.

Nimekaa kwa mama mtoto mwisho wa siku tukashauriane nikasome inshu ya ualimu ili nikimaliza niajiriwe moja kwa moja tusaidiane maisha. Nikaingia kusoma PGDE ile namaliza tu kusubiri ajira akaingia Rais Magufuli na roho yake mbaya akasitisha ajira za walimu hasa wa arts.

Nikaanza mdogo tena na hali ya kukosa furaha na msongo wa mawazo ikaanza upya, nikaona kukaa kwa mwanamke bila kazi ni noma nikaingia mkoa jirani tena kutafuta mishe nikapata chuo kufundisha, nikaanza maisha.

Sasa kitu kinachoniumiza na kutokua na furaha ni huyu mwenzangu yani sasa hivi naona mapenzi yamepungua sana, mawasiliano ni ya shida yani nisipomtafutaga hewani basi hana muda mimi japo ananisaidia kwa baadhi ya mambo manake mwenzangu ana kipato cha juu sana, lakini naona kunipa ile heshima na kunijali kama mzazi mwenzake haipo.

Nampenda ila anavyonipotezeaga nahisi kutengwa na walimwengu wote,
tangu mwaka Jana sina furaha na nakuwa na msongo wa mawazo ,nilitegemea huyu mwenzangu awe mtu wa kunitia moyo kunifariji katika mihangaiko yangu lakini hilo halipo hata kama ananisaidia lakini hanipi ile heshima yangu kama mwanaume hata kama sina hela naona kwangu ni sawa na bure.

Daily Mimi ndo nahangaika kumtafuta hewani, nilitembelea kwake suala la unyumba likawa la kusua sua hadi nikaanza kuwakumbuka michepuko yangu.

Sasa wakuu naombeni ushauri niishi style gani ili nisiweze kupoteza furaha yangu na nisiwe na muda tena wa kumuwaza waza huyu mwanamke na hata ile hali ya kumtafuta tafuta hewani ipotee.

Nifanyaje nisaidieni manake kila siku naona mimi ndo nahangaika juu yake halafu mwenzangu anaonekana hajali mawasiliano yangu .

Msaada tafadhali.
 
Pole sana ndugu,hizo ni changamoto tu za maisha,vumilia.

Kama upendo wake umepungua lazima kutakuwa na sababu cha msingi ni kujua hiyo sababu then chukua hatua kulingana na hiyo sababu.

Kumbuka ukitegemea furaha toka kwa mtu mwingine yawezekana mpk unaingia kaburini unaweza usipate furaha, furaha lazima itoke ndani yako,tafuta namna ya kujifurahisha pasipo kumtegemea mtu.

Kila la kheri.
 
Hahahaaa bro kwanza pole sana kwa yaliyokukuta pili natamani sana nikupe moyo wangu maana moyo wangu ni mgumu mithili ya miamba migumu, kwa sasa tafuta hela maana hela ndiyo itakuwa furaha yako, hayo mengine yanakuja " automatically "

Hakuna kitu kirahisi duniani ni lazima ukomae vya kutosha, wala usikate tamaa....
 
Mimi nakushauri Kama maisha unaona yanakupiga tuu haufanikiwi wekeza nguvu kwa mama mtoto wako kuwa Mario tuu, wekeza zaidi kwenye kupiga mashine piga mashine Sana huyo mwanamke mpaka apatwe na dege dege kuna vijana wengi Sana hapo Dar es salaam wamewekeza kwenye kupiga mashine.

Tafta vumbi la kongo umkarabati huyo mama watoto wako, mshahara wake mtagawana 50-50 mawasiliano yatarudi tuu utapigiwa simu masaa 24 Kaka.

Pia akikaa vibaya mchape mimba nyengine ndio kilichobaki hiko mkuu.

NB: Mkuu wa nchii alipohaidi viwanda hamkuelewa viwanda gani, hata kupiga mashine kisawa sawa kunaweza kuwa ni shuguli za uzalishaji kama viwandani tuu so wacha maneno mzee baba piga mashine, fokoa fokoa kabisa hiyo papuchi utapewa mawasiliano ya kutosha.
 
Pole sana...wanawake wakiwa na kipato kuzidi mwanaume ndo walivyo...
Kikubwa ni kwamba huwezi kummudu huyo mwanamke, kashakuona mzigo na uvumilivu wake umefika kikomo!!

Piga moyo konde anza maisha yako, sio ww tu wengi yamewakuta!!
 
Jitaid kuwa bze na kaz jichanganye na washikaj kweny mazoez jitaid kuiwazia sn hela na miangaiko yako utamsahau2 kwan kabla yake uliishije ucwe mdhaifu na mapenz yatakutesa yalishanikuta zaid ya hayo mbona saiz fresh yy kafulia atalee kuanza upya co dhambi
 
Wakuu salaam,

Kama mada inavyojieleza,

Miaka ya karibuni hasa kuanzia 2015 mwishoni nimekua mtu nisiyekua na furaha na nikiwa na furaha basi ndani ya siku chache huondoka
labda nieleze kinagaubaga jinsi maisha yangu yalivyo.

Wazazi wangu washafariki almost 16 years ago, tangu wakati huo ndugu ambao nilikua nawategemea wakaanza mizinguo so nikaanza kuishi ghetto tangu nipo form 1 hadi namaliza form 4, then nikachaguliwa kuingia advance so kipindi chote nasoma advance likizo zangu karibia zote zikiishia maghettoni kwa masela kwa sababu kule home sikua na watu ambao wa kuwategemea sana.

Ada nilikua nalipiwa tu na msamaria mwema mmoja.Nimemaliza form 6 nikafaulu kwenda chuo na Mungu si athumani nikapata mkopo kwa 90% nikaanza maisha ya chuo pale SUA, baada ya muda nikaamua kutoka hostel nikapanga ghetto maisha yakaendelea.

Wakati huu nikiri kwamba nilikua mtu mwenye furaha muda wote sikua mtu wa mawazo mawazo. Mwaka 2012 nikakutana na mwanamke barabarani pale mjini Moro yupo na mabahasha yake anatafuta kazi nikamwomba namba, nikaanza kumtongoza mtoto akakubali tukawa wapenzi.

Baada ya muda binti kapata ujauzito nikamwambia atoke kwao (kwa mama mdogo wake) nikaishi nae ghetto kwa amani na upendo. Wakati ana mimba akaitwa interview akapiga fresh, akarudi ghetto, maisha yakaendelea ya furaha, amani na upendo, binti kajifungua salama salimini.

Kumbukeni wakati ana ujauzito nilimfungulia biashara ndogo
baada ya mtoto kutimiza kama miezi 4 hivi mama yake akapata kazi kule alikofanya interview tena kwa mshahara mnono zaidi ya ule wa aupatae mwenye degree. Nikauza baadhi ya vitu vyangu mama na mtoto na ndugu yake wakasafiri hadi kituo cha kazi alichopangiwa.

Wakati huo mimi nishamaliza degree yangu nikaingia rasmi kitaa, kama mnavyojua nchi yetu ina changamoto za ajira, hapo ndo suala la kutokua na furaha likaanza. Nikasafiri hadi kwa mama mtoto nikakaa kwa muda then nikaingia mkoa jirani huku huku lake zone kutafuta mishe nikapata nikaanza kazi na nikapanga chumba, mwisho wa siku ikawa mtihani kulipwa basi kazi ikashindikana nikaondoka kurudi kwa mama mtoto.

Nimekaa kwa mama mtoto mwisho wa siku tukashauriane nikasome inshu ya ualimu ili nikimaliza niajiriwe moja kwa moja tusaidiane maisha. Nikaingia kusoma PGDE ile namaliza tu kusubiri ajira akaingia Rais Magufuli na roho yake mbaya akasitisha ajira za walimu hasa wa arts.

Nikaanza mdogo tena na hali ya kukosa furaha na msongo wa mawazo ikaanza upya, nikaona kukaa kwa mwanamke bila kazi ni noma nikaingia mkoa jirani tena kutafuta mishe nikapata chuo kufundisha, nikaanza maisha.

Sasa kitu kinachoniumiza na kutokua na furaha ni huyu mwenzangu yani sasa hivi naona mapenzi yamepungua sana, mawasiliano ni ya shida yani nisipomtafutaga hewani basi hana muda mimi japo ananisaidia kwa baadhi ya mambo manake mwenzangu ana kipato cha juu sana, lakini naona kunipa ile heshima na kunijali kama mzazi mwenzake haipo.

Nampenda ila anavyonipotezeaga nahisi kutengwa na walimwengu wote,
tangu mwaka Jana sina furaha na nakuwa na msongo wa mawazo ,nilitegemea huyu mwenzangu awe mtu wa kunitia moyo kunifariji katika mihangaiko yangu lakini hilo halipo hata kama ananisaidia lakini hanipi ile heshima yangu kama mwanaume hata kama sina hela naona kwangu ni sawa na bure.

Daily Mimi ndo nahangaika kumtafuta hewani, nilitembelea kwake suala la unyumba likawa la kusua sua hadi nikaanza kuwakumbuka michepuko yangu.

Sasa wakuu naombeni ushauri niishi style gani ili nisiweze kupoteza furaha yangu na nisiwe na muda tena wa kumuwaza waza huyu mwanamke na hata ile hali ya kumtafuta tafuta hewani ipotee.

Nifanyaje nisaidieni manake kila siku naona mimi ndo nahangaika juu yake halafu mwenzangu anaonekana hajali mawasiliano yangu .

Msaada tafadhali.
Duhhh leo sina ushauri wenye miguu wala kichwa.

Bad communication + No money = piga chini

Bad communication + No money + Child = Syntax error

Huyo Mtoto angetoka kwenye equation, jibu lingekuwa simple tu, achana na huyo mwanamke. But since there is a child, usikate mawasiliano. Mjulie hali mtoto.

Advice::: Tafuta kazi ya maana kwanza, huyo mwanamke muweke priority after your child. Hata ukimpigia wewe muulizie Mtoto tu. Kuwa mtu wa mazoezi au kama haupendi, tafuta hobby nyingine, etc playing music, programming au hata piga tuition. Hapo utamsahau tu.

Kwa uliyoyaandika inaonekana kakuona wewe mzigo kweli. Wanasemaga 'Money can't buy happiness' huu msemo wa wanyonge, wanajipa moyo. Ukweli ni kwamba Money makes happiness knock on your front door, kazi kwako kuufungua. Usimsahau mtoto.

-callmeGhost
 
Dah...Pole sana...me sina cha kukushauri mkuu.....maisha aya yametufundisha mengi magumu na changamoto zake....maisha yalinifundisha niwe napanda mnazi kwa mkono m1...goli la mkono kama maradona!dah....sitaki stress za mahusiano...!
 
Muombe sn Mungu kwa imani yako atakurudishia furaha. Tambua ktk mapenz hakuna kupendana ila kupenda au kupendwa. Tambua mapenz yanapo isha hasa mkizaa yanabaki majukum. Pole ndugu, tafuta pesa ili ukamilishe jukum lako la kulea, ipo cku Mungu atakupa aliekupenda au atamrudishia moyo wa upendo uyo mzazi mwenzio. Pole sn ndugu
 
Dah hii ni hatari sana inauma ila hamna namna ni kuwa mkeo hana tena hisia kali za mapenzi kwako na hakuthamini kama ilivyokuwa awali.

Wanawake tunawapenda sana ila pia ni viumbe wagumu sana kuishi nao maana hawanaga misimamo thabiti hata inapotokea mmetoka mbali kimaisha na mlipendana kiukweli mwanzoni. Huwa wanatamaa na kujisahau kirahisi mno na hawanaga utu wala huruma hasa akiamua lake.

Kiufupi tu ni hali ilivyo hapo ni mapenzi yake amehamishia kwa mtu asiyejulikana swala linalopelekea asiwe na hamu ya kukutafuta wala kukujulia hali kama ilivyokuwa awali. Hii hali inatokea sana hata mie imewahi nitokea, najua unavyoumia na kukosa raha ila cha msingi ni kujikaza tu.

Mwanamke akishaanza hizo tabia hafai tena labda aumizwe huko alikopeleka hisia zake ndio atakukumbuka. We cha msingi ni kujibidiisha na mambo ya utaftaji ili uweze kupata pesa na heshima pia kumuondoa akilini ingawa haitakuwa rahisi. Piga kimya fanya mambo mengine usimuwaze kaza roho chukulia poa tu maana hata ukilazimisha kumtafuta utaumia tu yeye hakuwazi.

Hii tabia ya baadhi ya wanawake imenifanya niamini kweli rafiki wa kweli ni pesa tu wazee. Investing in feelings za mapenzi is never paying ni sawa na kucheza biko tu. Pesa haiwezi kukusaliti hata siku moja,pesa huleta heshima, pesa huleta furaha,,,,it takes you to places, buy shit you want,,give you comfort el dinero motherfucker! You name it!!!
 
Kaka raha na furaha jipe mwenyewe, fanya kazi kwa bidii tengeneza pesa anza maisha upya .
Kila kitu kitakuwa sawa.
 
maelezo meeengi kumbe point ni mapenzi tu ndio yanakuchanganya.
kuishi mbali na mke ni kipaji, fanya namna muishi naye karibu maana huko aliko wahuni watajibebea kiulaini
 
2 Reactions
Reply
Back
Top Bottom